G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,772
- 36,664
Mbunge wa Kishapu ndugu Suleiman Nchambi ni msukuma, hivyo nimtoe shaka mbunge wa Mlimba (Chadema) bi Suzan Kiwanga kwa kusema kuwa "tuna shaka na uraia wako" leo mapema bungeni akichangia mjadala! Kwa sasa uraia wake hauna mushkheri yoyote ile! Ni raia halali wa Tanzania!
Vilevile mbunge wa Bababti ndugu Jituson Patel ni mbulu 'piwa' anajua kimbulu na ni mtu wa kule kaskazini! Hana shaka yoyote ile na hivyo vijiasili vya kule kwa 'wadosi' vimetokea bahati mbaya tu! Usishangae raia mweusi zaidi ya Chris Lukosi kuzaliwa China!
Harbinder Sethi ni mnyalu wa Iringa! Amezaliwa pale na kukulia pale!
Hawa watu wakitaka kujijua kuwa ni raia halali ama lah! Basi isiwe kazi nzito sana! Waanze kuwapinga Wathibitishaji wa raia halali wa Tanzania (CCM). Hiki chombo ndicho kikisema kuwa wewe siyo raia basi hautakuwa raia kweli!
Kabla Husein Bashe kuwa raia aliyehalalishwa kuwa ni Msomali na hiki chombo (CCM) alikuwa raia halali kabisa wa Tanzania! Alikuwa mnyamwezi! Kabla Jenerali Ulimwengu hajawa raia aliyethibitishwa na CCM kuwa ni mnyarwanda, alikuwa raia halali kabisa wa Tanzania! Kabla Maalim Seif Sharif hajawa 'chotara Hizbu' alikuwa mpemba safi kabisa!
Hawa watu wasipate shida sasa kwani ni raia safi kabisa! Huwa wanasema "every dog has its day"