NCCR yapinga rushwa muda huohuo wakitoa rushwa hapohapo

NCCR yapinga rushwa muda huohuo wakitoa rushwa hapohapo

kinyongo

Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
39
Reaction score
9
Chama cha Siasa cha NCCR MAGEOUZI kimejikuta kikiwa katika hali ya kutoeleweka baada ya kuilalamikia Rushwa iliyopo katika chama Mwenzake CCM kwa kusema kuwa itawashugulikia viongozi wake walioingia madarakani kwa Rushwa baada ya miezi sita wakati huohuo NCCR ikatoa Rushwa kwa waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo leo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano huo, Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Bw, Faustine Sungura, amesema kuwa hawapo tayari kuvumilia Rushwa kwa miezi sita kama ilivyo ahidiwa na Makamu wake Mangula.

Sungura amesema kuwa wanatoa siku saba kwa CCM kuhakikisha kuiagiza Serikali yake kuikomesha Rushwa na matendo yanayoendana nayo ndani ya siku saba kuanzia sasa.
"enzi za mwalimu Nyerere tulikuwa tunapata tabu sana kuwabaini wala rushwa tofauti na sasa ambapo wala Rushwa wote wanajulikana", amesema Sungura
Chakushangaza baada ya Makamu mwenyekiti kuongea na kuonyesha jinsi alivyokerwa na Rushwa iliyopo katika CCM, Afisa habari wa chama hicho Bw, Florian Lutayigwa alianza kuwagawia Baadhi ya waandishi waliokuwemo katika mkutano huo shilingi 5000 kila mmoja ambazo wengi tulitafsiri kwamba ni Rushwa ili waandishi wakaiandike habari hiyo kama ilivyo.
Na wakati akitoa pesa hizo alikuwa anawaambia waandishi hao kuwa wahakikishe wameandika story kwani kesho atanunua magazeti kuona kama habari imetoka.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
IMG_0248.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Hawa ni waandishi wa habari waliokuwemo kwenye mkutano huo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
IMG_0270.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Hapa Bw, Florian Lutayigwa akitoa pesa kwa waandishi waliohudhuria katika mkutano huo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

SOURCE: maasinda.blogspot.com
 

Attachments

  • IMG_0270.JPG
    IMG_0270.JPG
    39.2 KB · Views: 48
hahahahhaaha huyu bwana kanichekesha eti "hakikisha mnaandika habari... nitanunua gazeti kesho nicheki..." NCCR kinaenda kufa tu kama mkuu zitto alivyosema...
 
Waandishi wa habari inaonekana pia wameathiriwa na Rushwa wakiitwa sehemu kwa ajili ya kupewa habari wanatarajia kupewa posho pia.
 
hahaha! Hii inatokea tanzania tu.
hivi mtu unaweza kuwa akili imelala alafu hujijui kabisa unachokifanya na unachokiongea?
 
Nawaonea huruma majembe Machali, Kafulila nk. wameingia choo cha kike pale NCCR.
 
1. Kama kweli si posho ya kazi ni rushwa, TAKUKURU na Polisi wapo, wakawakamate mtoaji na wapokeaji
2. Waandishi wa habari mna la kujibu hapa?
3. Mwenye blog; ni pro-ccm, picha anazopost na jinsi alivyoandika habari hii ni uthibitisho wa hilo. Blog yake full ziara za Kinana, Spika, na Rais
 
Waandishi mnazidi kutia aibu posho Tshs. 5,000/=? halafu mtu anatoa komand mkaandike hiyo taarifa Mh! kweli waandishi wa nchi hii njaa kali ndo maana hata msimamo mliokuwa nao baada ya kuuwawa Mwangosi hamna tena mmeisha nyamazishwa.
 
Back
Top Bottom