NCCR wahaha kumvua Ubunge Kafulila

Relief

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
254
47


Kufuatia kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, chama cha NCCR Mageuzi sasa kinahaha kumwondoa kwenye ubunge baada ya kumshinikiza Spika Anna Makinda amwengua katika uwakilishi wa jimbo hilo.

Taarifa zilizopatikana mwishoni mwa wiki, zilisema NCCR Mageuzi imemwandikia barua Makinda kumtaka atekeleze uamuzi huo wa Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho wakisisitiza kuwa hakuna amri ya mahakama iliyomzuia kumfukuza ubunge Kafulila. Barua ya chama hicho ya Januari 17 ambayo nakala imepelekwa kwa W/Mkuu Mizengo Pinda yenye kumbukumbu namba NCCR-M/MM/BJMT/10/21, imeituhumu Ofisi ya Spika Makinda kwamba inatumika kumlinda Kafulila kwa lengo la kukidhalilisha chama hicho.

''Mheshimiwa Spika, inasikitisha na inafedhehesha sana kwamba ofisi yako haijatutendea haki. Pamoja na kuwapo shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya NCCR-Mageuzi, bado hakuna amri yoyote ile inayokuzuia wewe kutekeleza majukumu yako kama mhimili mmojawapo wa dola'' inasema sehemu ya barua hiyo.
Barua hiyo yenye kichwa cha habari: ''Taswira Dhalili ya Chama Cha National Convention for Construction and Reform-Mageuzi kwa Ofisi ya Bunge, imesisitiza kuwa kumfanya Kafulila aendelee kuwa mbunge, Ofisi ya Bunge imekusudia kukidhalilisha chama hicho''

Tendwa
Msajili wa vyama alipoulizwa alisema mgogoro huo asingependa kuuzungumzia kwa kuwa yupo safarini.

Kafulila
Kafulila alipoulizwa juu ya suala hilo alisema hana taarifa na barua hiyo, ila anatambua kuwa yeye bado ni mbunge kwa sababu ya amri ya mahakama. ''Mimi nilipofukuzwa tu, nikaenda mahakamani kupinga uamuzi na kuzuia utekelezaji wake. Mahakama imeitaka NCCR isitekeleze chochote mpaka kesi imalizike na ndio maana sasa pia ninawasilisha ombi mahakamani kutaka niendelee kutambuliwa kama mjumbe halali wa vikao vya chama hicho'' alisema.

Spika Makinda/Dk Kashililah
Spika Makinda alipotafutwa jana azungumzie suala hilo hakupatikana baada ya simu yake ya mkononi kuita muda wote bila kupokelewa.
Lakini Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema ''Hatuwezi kufanya lolote kwa kuwa Mbatia amefungua kesi mahakamani''
''Muulizeni Mbatia mwenyewe kwa kuwa amefungua kesi mahakamani dhidi ya Bunge na Serikali kuhusu suala hili hili''

Lakini juzi Jaji Alice Chingwile wa Mahakama Kuu anayesikiliza kesi hiyo alisema hawezi kuendelea nayo kwanza mpaka amalize kusikiliza kesi ya msingi iliyofunguliwa na Kafulila kupinga uamuzi wa kufukuzwa uanachama mwaka jana Desemba.

Source: MWANANCHI

Kazi ipo!
Hivii, Nccr mi naomba kuwauliza, ni kwamba mmefikia mahali hamuheshimu tena amri ya mahakama au ni hofu yenu kwa huyu jamaa ndo inasababisha mtape tape kiasi hiki?
 
Hiyo barua waliandika january. Huu ni mwezi march. Waliona pinda na makinda wanawapuuza. Wakamua kwenda mahakamani kumshitaki spika na katibu wa bunge. Kweli dr mvungi anajidhalilisha sana. Yani dr wa sheria unakuwa zezeta kiasi hiki?
 
Back
Top Bottom