NCCR: NEC ndio kiini cha Vurugu Igunga


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
81
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 81 145
[h=3]
[/h]

Rachel Balama na Anneth Kagenda

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema vitendo vya vurugu vinavyokumba kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga ni matokeo ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kushindwa kuweka sheria ya maadili ya uchaguzi.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es salaam jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw.Samuel Ruhuza, wakati akitoa tamko la NCCR Mageuzi kuhusu matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Zambia kwa waandishi wa habari.

Bw. Ruhuza alisema kuwa NEC inawajibika kwa vitendo vyote viovu vinavyoendelea kutokea Igunga kutokana na kutoandaa sheria ya maadili ya uchaguzi ambapo kila chama kinaamua kufanya kinavyotaka.

"Uchaguzi uliopita Tume kwa kushirikiana na vyama vya siasa viliandaa sheria ya maadili ya uchaguzi, lakini kwa uchaguzi huu mdogo na ule wa madiwani katika kata 22 kwenye majimbo mbalimbali ya Tanzania Bara Tume imekataa sheria hiyo kutumika kwa madai kwamba ina makosa," alisema.

Alisema kutokana na Tume hiyo kutoandaa sheria hiyo watanzania wanashuhudia vurugu kila wakati huku kukiwa hakuna mtu wala chama anayechukuliwa hatua zozote za kisheria.

"Uzembe na ukiritimba wa NEC ndio maana watu wamekuwa wakidiriki hata kupanda majukwaani wakiwa na bastola kiunoni kwa kujua kwamba hakuna hatua yoyote ya kisheria watakayo chukuliwa," alisema.

Bw. Ruhuza aliongeza kuwa ipo haja ya kuwepo kwa Tume huru ambayo itakuwa na idadi ya watu, vigezo vya wafanyakazi hata kama itateuliwa na rais.

Alidai kuwa hiviu sasa Mkurugenzi wa NEC yuko juu ya sheria na kwamba hali hiyo imekuwa ikichangia kutokea kwa vurugu katika hcaguzi ndogo.

Hata hivyo kwa mujibu wa Katiba ya nchi na sheria hakuna aliye juu ya sheria.

Katibu huyo alitoa pongezi kwa Tume ya Uchaguzi ya Zambia kwa kuepusha taifa hilo kuingia kwenye vurugu kwa kuzingatia sheria ya uchaguzi hatimaye kumtangaza Bw.Michael Chilufya Sata kuwa rais kutoka chama pinzani.

Alisema Tume hiyo inastahili pongezi kwa kuepusha vurugu kwa kuwa nchi nyingi za kiafrika zinaingia katika vurugu wakati wa uchaguzi kutokana na matokeo.

Alisema sio jambo trahisi kuona tume iliyoteuliwa na mtawala ikitangaza aliyeiteua kushindwa.
 
mashikolomageni

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
1,566
Likes
10
Points
135
mashikolomageni

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
1,566 10 135
Tume hii ni ya magamba haina mandate ya kuwabana hao ccm ila pale nguvu ya umma inapokuwa kubwa sana ndio huwa inasalim amri. Inawezekana imefanya kwa makusudi ilikuwe na loop hole ya appeal watakapo shindwa kuchaguliwa wagombea wa chama cha tume
 
mmbangifingi

mmbangifingi

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Messages
2,857
Likes
25
Points
135
mmbangifingi

mmbangifingi

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2011
2,857 25 135
Mojawapo ya kitu katiba mpya inatakiwa ianishe ni muundo wa tume ya uchaguzi. hii ya sasa pamoja na msimamizi wa chaguzi kuwa mkurugenzi ambaye ni mteule wa rais pia, nadra sana kutoa maamuzi firm bila kupendelea upande wa aliyewateua
 

Forum statistics

Threads 1,238,281
Members 475,878
Posts 29,314,868