NCCR Mara wamtetea Mbatia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR Mara wamtetea Mbatia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by February, Dec 2, 2011.

 1. February

  February Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Harakati za kinacho onekana kama kujivua gamba ndani ya chama cha nccr mageuzi zimetoa sura mpya leo baada wajumbe watatu kati ya watano wa mkutano mkuu kutoka mkoa wa mara kutokubaliana na mapinduzi dhidi ya mwenyekiti taifa james mbatia. Kikao hicho kilichohudhuriwa pia na madiwani wawili wa mkoa huo kupitia nccr kilitawaliwa na mvutano mkali hali iliyopelekea wajumbe watatu kusema mbatia avumiliwe mpaka uchaguzi pamoja na mapungufu yote huku wajumbe wawili wakiweka msimamo kuunga mkono azimio la NEC ya chama hicho kuwa makosa yake yanatosha kumsimamisha na kuitisha uchaguzi. Miongoni mwa hoja zilizotanda katika kikao hicho ni pamoja na hoja ya mbatia kushindwa vibaya uchaguzi wa kawe akiwa mwenyekiti taifa hata kuwa nafasi ya tatu baada ya chadema na ccm, hoja ya kwanini mbatia amshataki mpinzani aliyeshinda bi halima mdee ilhali hakuna uwezekano wa kushinda jimbo hata ikiwa uchaguzi utarudiwa na hoja ya mwenendo mbaya wa matamko ambayo amekuwa akiyatoa mbatia hata kukifanya chama hicho kitafsiriwe kuwa ccmB. Baada ya kujadiliana kwa kina wajumbe walikumbushwa na mwenyekiti wa nccr mkoa wa mara kuwa mbatia amekitoa chama mbali na hivyo pamoja na mapungufu yote ni muhimu asamehewe hasa kipindi hiki baada ya kupata wabunge na ruzuku. Msimamo huo uliungwa mkono na wajumbe pamoja na mgawanyiko uliokuwepo na kukubaliana kuwa bado mbatia aendelee kukiongoza chama hicho. Na hivyo wajumbe wa halmashauri kuu washauriwe kutomsimamisha kama ilivyo azimiwa. Kikao hiki ni mwendelezo wa vikao ambapo mpaka sasa mikoa ya mbeya, kusini unguja, mikoa yote na pemba na kigoma tayari wametoa msimamo wao kuunga mkono azimio la nec la mbatia kuenguliwa mara moja kufuatia udhaifu unaotafsiriwa kukifanya chama kionekane wakala wa ccm. Source radio free
   
 2. February

  February Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyu ndio mbatia. Ukitaka kujua uwezo wake mulize matando.
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mbatia ni tatizo, ajipunzishe kulinda heshima yake na heshima ya chama
   
 4. i

  ibange JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kiongozi mzuri ni yule anayeweza kuwajibika. Mbatia baada ya kushindwa angepaswa kujiuzulu hata Lipumba pia. Wapinzani lazima tuonyeshe demokrasia
   
 5. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wana NCCR-Mageuzi, hususan viongozi wa mikoani na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama. Kabla ya kuwapa tahadhari, naomba niwashirikishe kisa kifuatacho;
  Wakati Nabii Musa akiwa bado anahesabika kwamba ni mwana wa Binti Farao (kabla ya ukweli kujulikana), alishtakiwa na Mwana wa Mfalme aitwaye Ramsa, kwamba Musa ameonekana akiwa na ushirika wa karibu na watumwa (yaani wana wa Israel, ambao walikuwa watumwa nchini Misri). Basi Farao akamfuata Musa ili amhukumu. Alimwuliza maswali yafuatayo kuhusu tuhuma zake;
  1. Musa, kuna mtumwa alikandamiza na jiwe la kujengea piramid ukamwokoa asife?
  Musa akajibu; Ndio Mtukufu Farao
  2. Musa, watumwa walilalamika kwamba hawana chakula, ukawagawia chakula toka hazina ya taifa?
  Musa akajibu tena; Ndio Mtukufu Farao

  Basi Farao akakasirika, akawa tayari kumhukumu Musa, lakini akampa fursa ajitetee.

  Ndipo Musa akajitetea hivi;
  Mtukufu Farao,
  watumwa waliokufa hawatengenezi tofali hata moja
  watumwa walio na njaa wanatengeneza matofali machache sana
  bali walioshiba wanatengeneza matofali mengi, na wamefanya hivyo hata wamekujengea miji mizuri sana Mtukufu Farao.

  Ndipo hasira ya Farao ikayeyuka, badala yake Musa akawa kipenzi cha Farao hata akatamani angekuwa mrithi wake.

  Mantiki ya kuwasimulia hili, ni kwamba; mpeni James Mbatia Nafasi ya kujitetea, pimeni ukweli wa yale mnayomtuhumu. Linganisha na kazi alizokifanyia chama.
  Kamwe hamtafisha ukweli, kwamba mchango wa Mbatia kufanya NCCR kiendelee kuwepo hadi sasa, hasa baada ya mtafaruku wa miaka ya 90, ni mkubwa hakuna mfano.

  Nimemfahamu Mbatia kama kiongozi aliyeuza mali zake ili chama kiendelee kuwepo, wakali ule akipati hata senti tano ya ruzuku (nani mwingine kati yenu alifanya hayo?).
  Nimemfahamu Mbatia kama kiongozi aliyetoa mali zake hususan magari binafsi kwa ajili ya kampeni za ubunge mikoani (nani mwingine kati yenu kafanya hayo)
  Nimemfahamu Mbatia na utayari wake wa kuacha uongozi ili akaiendeleze taaluma yake, lakini baadhi yenu mlimg'ang'ania ili aendelee kuwepo (hata katika uchaguzi wa 2009 ilikuwa hivyo hivyo)
  Nawambieni ukweli, tuhuma zimeletwa kwenu, nanyi mnazikurupukia bila kutafakari kwa kina, mtauona mwisho wake.

  Si nia yangu kumtetea, kama anatoa kauli zinazoshabikia CCM, mwambieni akome kufanya hivyo, la asipowasikiliza awajibike kwa kweli.

  Kama ni kushindwa ubunge, basi fukuzeni viongozi wote ambao waligombea wakashindwa;
  Makamu mwenyekiti Bara alishinda?
  Makamu mwenyekiti Zanzibar alishinda?
  Katibu Mkuu kule Ngara alishinda?
  Naibu katibu Mkuu alishinda?
  Huyo Rungwe anayetaka huo uenyekiti, alipogombe Kinondoni 2005, alipata nafasi ya ngapi na kura ngapi? Alipogombea Urais, si hata ndugu zake wa Kigoma walimwambia NOPE?
  Mkitumia kigezo cha kushindwa uchaguzi sidhani kama mtapata hata wagombea hiyo 2015, maana kila atakayetaka kugombea ataogoba kushindwa kisha afukuzwe uongozi katika chama.
  BUSARA ZIWAONGOZE.
   
 6. February

  February Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimependa sana uchambuzi wa waridi kuhusu mbatia na chama chake cha nccr. Na mfano wa mussa kuwasaidia wale watumwa na kukiri alipohojiwa na farao ni kwasababu wale watumwa ni ndugu zake. Hivyo waridi unawaelekeza wana nccr wasimuhukumu mbatia kwa kauli za kutetea ccm kwakuwa ccm wamemwaga pesa nyingi nccr hata kuifanya iendelee kuwepo bila ruzuku kwa kazi moja tu ya kukisemea ccm dhidi ya wapinzani tangu kule zanzibar walipoweka mapingamizi na kuinyima cuf majimbo sita kipindi cuf ikiwa ngangari na hata badae mbatia kupambana na slaa alipotangaza orodha ya mafisadi ambao ni vigogo wa serikali kisha mbatia kwa hasira za mafisadi kudhalilishwa akaja na hoja kuwa watz wote ni mafisadi isipokuwa tunatofautiana viwango tu. Kazi hii ya mbatia kuwa kibaraka wa ccm na serikali yake ndio vimeifanya nccr iendelee kusikika hata kama kwa ubaya. Lakini ipo. Nisichokubaliana na waridi ni kwamba mbatia amejitolea pesa na kuuza mali zake kwajili ya chama. Hapana. Hiyo kazi ya kuwatetea watuhumiwa na ccm ndiyo vimemfanya mbatia aendelee kuishi mjini. Anaishi nyumba nzuri na maisha ya juu kwa kuwa mwenyekiti wa chama kisicho na ruzuku. We hujifunzi kitu hapo? Kwa sisi tulio kwenye media tunajua vizuri mambo haya. Kuna wakati ccm wanakupigia simu wakiomba mbatia aulizwe kuhusu suala fulani ukimuliza mbatia anatoa majibu yanayowapendeza ccm. Hapa ndipo nilimdharau huyu jamaa. Kuhusu kushindwa chaguzi ni kweli sio hoja kubwa kwa chama zaidi ni hoja kubwa kwake na dhamira yake mwenyewe kwamba anajisikiaje kushindwa na wanawake wawili katika afrika yenye mfumo dume? Lakini zaidi katika hali ya kawaida hivi mbatia anaweza kuwa na uhalali ya kumnadi mgombea ubunge ikitokea uchaguzi mdogo? Atasemaje? Kwamba yeye ni kamanda? Kamanda aliyepigwa na wanawake na kukimbilia mahakamani? Tuseme ukweli jamani mbatia anaweza kubaki kwa kichwa ngumu tu lakini heshima yake kwa umma imeporomoka mpaka sifuri. Hebu jiulize. Inakuwaje ameshindwa kura na mdee kwa tofauti ya zaidi ya kura elfu30 afu anakwenda mahakamani? Hivi akimshinda mdee na uchaguzi ukarudiwa afu ccm wakapora jimbo nccr kitaweka wapi sura yake? Kama mdee alimchafua kwenye uchaguzi si rafu za kawaida hizo kisiasa. Lakini pia kama hoja ni kuchafuliwa kwann aisifungue kesi ya kuchafuliwa jina badala yake anafungua kesi kupinga matokeo? Jamani huyu mtu hasaidiki. Ccm wamemtumia mpaka ame expire akili. Kama anabaki abaki kwa mana asaidiwe kupata kinua mgongo bada ya ruzuku hii kuanza kupatikana mana kwa mazingira ya sasa hawezi kuitumikia sisiemu vizuri bila hawa madogo wabunge kumpinga.
   
 7. k

  kulunalila Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Apewe muda
   
 8. February

  February Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli apewe muda mana cuf wameshindwa kazi ya kuishambulia cdm. Kwanza akamilishe kazi ya kumtoa mdee bungeni ccm washindwe wenyewe kutumia fursa
   
 9. February

  February Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli apewe muda mana cuf wameshindwa kazi ya kuishambulia cdm. Kwanza akamilishe kazi ya kumtoa mdee bungeni ccm washindwe wenyewe kutumia fursa
   
 10. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135

  February!!
  Ati wewe ni mwandishi wa habari? Michango yako ya JF inafanana kabisa na style ya uandishi ya mtu ninayemjua ambaye si mwandishi wa habari
  Ati Mbatia hajauza mali zake kwa ajili ya chama? Tafuta ushahidi wa nilichosema toka kwa wanachama wa chama hiki. Kawaulize ile ardhi inayomilikiwa na chama kule Bagamoyo ilipatikanaje?
  Ati Mbatia anaishi nyumba Nzuri? Kafuatilie ili ujue kwamba nyumba anayoishi ni ya shirika ambalo mkewe ni mwajiriwa.
  Ati mfano wa Musa na watumwa wa Israel ni sawa na Mbatia na CCM? Umenisoma lakini hukunielewa. Hoja yangu ni kwamba atendewe haki kwa kuhojiwa katika tuhuma zake.
   
 11. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyie wote ni NCCR msituzingue hapa!
  inaonyesha kati yenu kuna ambaye anafaidika na uwepo wa bwa'mkubwa na mwingine hafaidiki ndo maana mnazozana tuu hapa, hebu jadilini vitu vya maana msijadili mtu hapa, alaa!
   
Loading...