GE2025 NCCR Mageuzi: Reforms zimeshafanyika, uchaguzi utafanyika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Chama cha NCCR-Mageuzi kimefanya uchaguzi wake mkuu na kumchagua Evaline Munisi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo, Machi 30, 2025, katika Ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Evaline Munisi alipata kura 34, akimshinda Saganda Khalid, aliyepata kura 19 kati ya kura 53 zilizopigwa.

Wengine walioshinda ni Martin Bernad, aliyepata kura za "Ndiyo" 40, na kuchaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Shindani Ally, aliyechaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Zanzibar, na Suzan Masele, aliyechaguliwa kuwa Mweka Hazina wa chama hicho.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Evaline Munisi, Katibu Mkuu mpya wa NCCR-Mageuzi, ameahidi kurejesha hadhi ya chama hicho kwa kuhakikisha wanashinda katika Uchaguzi Mkuu ujao, huku akisisitiza kuwa hawana hofu na Chama Cha Mapinduzi (CCM). kwa sababu mabadiliko ya mfumo wa Uchaguzi yaliyokuwa yakipiganiwa tayari yalishafanyika kupitia Baraza kuu la vyama vya siasa kwa kushirikiana na Kikosi kazi kilichokuwa kimeundwa.

"Tunayo imani kubwa na mchakato wa uchaguzi kwa sababu tayari mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi yameshafanyika kupitia Kikosi Kazi. Tunaiomba serikali isiruhusu watu kuvunja Katiba, kwani uchaguzi upo kwa mujibu wa Katiba, na sisi NCCR-Mageuzi tunafuata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," amesema Munisi.

Huyu kichekesho ametoka wapi? Watakamata dola gani hawa wapumbavu? Walevi nao wana mambo yao....Mjinga huyu.Anaongea kama anaumwa hivi. Hao wasimamizi hao wamebadilishwa, Maafisa waandamizi hao wa serikali ambao ni makada. Kweli watu wengine hawana akili.
 
Cdm anapambana na ccm, vyama vingine vinapambana na cdm.
 
Tunaifurahia tanzania yetu ni nchi nzuri. Ila hawa chawa na wapumbavu flani hakika ni mbaya sana.
 
Back
Top Bottom