NBC na huduma ya Sim Banking

nasssen

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
483
508
Habari za jioni wana JF na poleni kwa mihanfaiko ya wiki nzima.

Mimi ni mtumiaji wa huduma za kibenki za NBC na ninapendelea sana hii huduma yao ya Sim Banking kwani ni rahisi sana na haraka pia unapotaka kutoa cash mahali popote.

TATIZO: Yani hivi karibuni imekuwa ni kero ya kupindukia, kwani unaweza ukajaribu kupiga namba yao *150*55# hata mara 20 pasipo mafanikio. Kwa mfano siku ya leo nimejaribu tangu asubuhi lakin inaniambia "External application down".

Je, kuna mteja mwingine wa NBC anayepata tatizo kama la kwangu?
Au kama iliwahi kukutokea ulifanya kitu gani kutatua hili tatizo?
Au ni system yao haipo vizuri kwa upande mwingine?


Nakaribisha hoja....Ahsanteni!
 
Back
Top Bottom