The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Naitumia benki hii kwa muda mrefu lakini siwaelewi kabisa wanaoiendesha.
Huduma zao haziridhishi kwa namna nyingi hadi nahisi watumishi/waendeshaji wake hufanya kusudi ili iwe na sifa mbaya miongoni mwa watumia huduma za benki!
Kwanza jaribuni kufuatilia ukongwe wake na muda inaotumia kuingia kwenye huduma mpya zinazojitokeza katika soko kama "mobile banking"
Mabenki kama CRDB, NMB na benki nyingine nyingi tena changa zimeingiza huduma hiyo katika mifumo yake siku nyingi tu.
Kumekuwa na malalamiko mengi tu juu ya muda uliokuwa unatumika kumuunganisha mteja na huduma NBC Mobile. Unaweza kujaza fomu lakini ikapita muda mrefu kabla simu haijawa "activated" hii nayo haijakaa vizuri.
Utatuzi wa matatizo ya wateja unachukua muda mrefu kuliko inavyopaswa. Mfano ikitokea ukahamisha fedha kwenda mtandao wa M-Pesa na kwa kasoro zao wenyewe fedha isifike na wakati ilishatoka kwenye akaunti inakupaswa kusubiri siku 21 ndo upewe jibu kama utarejeshewa hiyo fedha au uambiwe vinginevyo. Jamani katika dunia ya sasa kuna haja ya kusubiri muda wote huo kweli?
Au wana upungufu wa fedha na sasa wanalazimisha fedha za wanyonge zikae huko muda mrefu ili wapate za kukopesha matajiri?
Anaejua matatizo ya benki hii naomba awasaidie watu wasioridhishwa na mambo ya benki hii.
Naomba kuwasilisha.