NBC Bank hawana maana kabisa

Labda Naelewa vibaya lakini nafahamu ukiwa unachukua hela nyingi kama above 3m...huwa wana confirm na brach yako au...unaambiwa nenda Nje kwenye ATM.
Print Risit ambayo itakuwa na jina laki na balance iliyopo...then unapata kiwango chako unacho taka.

The same na CRDB..Kama account yako iko Kahama na wewe unataka kuchukua pesa mbeya.Lazima wa confirm na brach yako Kahama au the same way kwenda kwenye ATAM machine...print that ka risit.Barclays wao ni ndani card yako na kitambulisho chako cha kazi au mkazi...ili uweze pata vijisent.

I wish ingekuwa rahisi hivyo.

Hakuna mtu anawakatalia wasi-confirm na branch yako. Tatizo ni mda unaowachukua kufanya hivyo.

Kuna mshakaji wangu juzi hapa akaambiwa asubiri fax irudi. Baada ya saa moja hivi machale yakamcheza. Akawaambia basi shughulikieni hiyo fax ntarudi kesho. Kesho yake asubuhi anaibuka anaambiwa fax bado haijajibiwa ... tehe tehe ... it takes a few minutes to communicate na ki-robot kilicho mars ... hata kwa kutmia fax.

Baada ya kusubiri fax mpaka kesho yake ndio wanamwambia branch yako wanataka wakuone wenyewe. So ikabidi afunge safari kwenda kuchukua pesa zake... 3 days gone. Hata dili aliyokuwa anataka kuifanya ilisha-expire, akasema bora tu akakombe pesa zake aeke nyumbani.
 
hahahahaaa! mimi nshawaandikia barua! nilifungua acount Lindi, baada ya 1 month nikaondoka lindi, nikaenda mbeya, mbona nilikoma.
Siku moja niakenda moshi, nilikaa 6 good hrs nangoja fax kutoka lindi, sijui ya nini, lakini hela niliweka mbeya.

nikaamua kubadilisha kiasi nilichokuwa nataka kutoa, nikatoa hela yote nikaacha 10,000, na sijawahi kuweka hela tena huko, ni 4 years sasa.
 
Salamu hizi zimfikie manager wa tawi la Unguja Baada ya ku-complain kwa muda mwingi basi alitumia nusu saa kunielewesha ati sababu ya security.Inauzi sana mashine mbovu na balance wanayotambua ni ile ya kwenye ATM hivi hawa wana akili timamu.Mfanyakazi mmoja wa Cooperate branch aliniuma sikio na kusema masharti yote hayo yanaletwa na makaburu hata wao kama wafanyakazi wanajisikia kumsumbua mteja kwenda kujua salio nje kwenye mashine.Yote kwa Yote NBC wamebaki kama jina tuu.Kwani Baclays kesha mnunua Absa na Absa ndio alikuwa amemnunua NBC kwa hiyo lawama zote ziende kwa Baclays kwani nasikia kuwa wanalazimishwa kutumia jina la NBC wakati wao wamekwisha nunua hivyo wanataka matawi yote ya NBC yaitwe Baclays.

Wakatabahu.
 
Hao ndio MAKABURU kaka! Walinunua benki bila kulipa kitui! Lengo lao ni kuua uchumi wetu ! angalia utendaji ulivyo hovyo kwamfano ukitaka kuchukua kiwango kikubwa kwenye account yako sharti kwanza upane foleni kwenye ATM ukisimamiwa na mtu wao , uchukue balance, then uingie ndani , upange tena foleni kuchukua pesa kwa teller! Jamani hii ni benki au? Kuna mtindo wamezua siku nizi wa kudai Server iko down! Na inasemekana hiyo Server iko South Africa! Hawa ndio waliyakataa baadhi ya matawi ya iliyokua National Bank of Cormerce kwa kudai ni 'machafu' lakini baada ya kuwa yamesaishwa na kuimairishwa wakataka eti wauziwe! Na ajabu na kweli huyu ambaye sasa hivi 'anasafishwa' akawa tayari anawazawadia hiyo NMB mpaka ilimtia hasrra mkurugunzi mkuu aliyesota kukarabati na akaamua kubwaga manyangana kurudi kwao!
Makaburu haohao waliizika KIBO BREWERIES na kukosesha ajira na mapato ya serikali pamoja na kwamba ilikuwa infanya vizuri! sasa hivi ndio wanamliki KONYAGI, CHIBUKU!
Yaani mpaka hapo nia na madhumuni yao hamjawasoma?
 
Nafurahi kuwa wanaJF mumeliona hili la NBC kwani the same day nlipotoka ndo nilipost hii thread, nkaona kimya nkadhani mi mapepe kuona hawafanyi sahihi, thanks much. pia kuhakikishia watu nimetuma mails zao zote ktk web yao hakuna hata moja iliyosomwa au kujibiwa, contact us tAB ni mapambo tuu KTK WEB YAO. sasa bank kibao tz why unyanyasaji tena? what is the way foward? au incompetent people wameajiriwa? Duh tutakuwa kichwa cha mwendawazimu hadi dunia iishe ikianza upya ndo may be! hela yako then aah!! yatia hata hasira
 
kaka tuliwafukuza na kuwaimba sana makaburu tukiwa primary, but sasa ndo wameshika nguzo za uchumi wa nchi hii count!!
1. Banks
2.Viwanda muhimu, breweries,
3. Migodi
4. Simu za mikononi
5.shopping malls
6.Extra akina dada zetu mamis kwa wamis wote wapo kwa makaburu na wanagombea kwenda huko
b.nkapas alisema tunawaonea wivu nao wamepata pembe!! uliza matusi yao ktk maofisi!!dharau!! low payment!!duh kazi tunayo vijana!! so la NBC nalo mlemle
 
Mnataka kucheza mduara sasa, kumbukeni benki zilizo na akili bongo zinamilikiwa karibu na mtu mmoja. Kama atc inavyokufa kunufaisha shirika fulani la ndege ndo general tyre, reli, na hata nbc. Kumbuka pia nbc ipo owned na absa, na hii absa ipo ina hisa standard chatered na stanibic. Na hii absa ipo owned na bacrays, basi tunakukaribisha benki ya makabwela nmb, lakini huku hakuna mikopo ya maana.
 
Ondokeni huko -kwani mmelazimishwa?? Mimi nipo CRDB ni poa tu..hakuna longolongo kama za NBC!!!

Watu bwana! Kwa kulalamika tu!
 
NBC wanamatatizo sana, wafanyakazi wao wengi hawajui kuongea na wateja vizuri, ATM nyingi mbovu, foleni kupindukia wakati kaunta nyingi hazina watoa huduma.
 
Back
Top Bottom