NBC Bank hawana maana kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NBC Bank hawana maana kabisa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by RealTz77, Jul 28, 2009.

 1. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naomba nitoe vioja na upumbavu wa technology unaofanywa na bank ya NBC. Yani ukitaka kuchukua hela counter(ndani namaanisha) lazma uende kwenye tawi lako, km huwezi unasubiri watume fax then wajibiwe ndo km vipi wakupe mshiko, sasa najiuliza:

  1. Nini maana ya kunetwork system?
  2. Fax kama tuijuavyo ni taarifa gan wanaitaka, au kuipata toka branch yako? Na hii fax unaweza kusimama hadi 8hrs!!
  3. Je, ni uvivu au bureaucracy tu ya Management?
  4. Wataalamu naomba msaada hii inasaidia nini? Kama ni wizi sasa taarifa gani inatumwa kwa fax? Picha zipo ktk network, information yote ipo!
  5. Imagine unatoka mkoani unakuja draw hela ya kuchukua biashara then siku nzima unasimama kusubiri fax ijibiwe from Mwanza!??!!

  Is this not stupidity at its best? Kama kuna mtu wa NBC ktk JF atusaidie hili, linakera sana!! Basi mtu uweze toa ABOVE 1m FROM ATM km ushenzi wenyewe ndo huo.

  Shame on you NBC!! hamna lolote, na ntawahama, na wengine watafuata!!
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kati ya Bank zenye system mbovu na zilizo pita na wakati hii ndo inaongoza.
  Nimesha hamisha fedha zangu zote huko pesa yako alafu unateseka kuchukua pesa yako yanini ujipe shida hama mkuu mimi nilikuwa mteja wao mzuri walicho nifanyia nikaamua kuchukua pesa zangu zote.
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Angalia software wanayotumia (FlexCube) version yake ni ya mwaka gani kama hutakuta ni ya 1997! Yani ovyo afadhali ya Fax mkuu!

  Hiyo ndiyo NBC bwana, halafu ukiwambia ukweli hawapendi wanaishia kufungia wafanyakazi wao wasiweze ku-access JF.

  Wakati mwingine nashindwa hata kuelewa vichwa vya watu vina nini ndani yake!
   
 4. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hujui unaloliongea wewe..nadhan wala hujui jinsi pesa zinavyoibwa siku hizi ktk bank kwa kutokuwa makini..
   
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Hakuna umakini wowote, wewe usubiri fax na hela zako mwenyewe kwa 8hrs! This is too much! Mimi mwenyewe wameniudhi kweli kweli, hebu fikiria kuna cheque imelipwa na kuwa deposited kwao tangu tarehe 16/7, hadi naandika hapa iko uncleared wakati ni local cq tena kutoka Sister co, ambazo signatories ni hao hao.
   
 6. W

  William John 67 Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi bank nazo sijui kama tutafika.
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  hawa jamaaa hawako serious na biashara,ukienda kwenye branch zao unakuta kaunta zipo 6 alafu inafanya kazi kaunta 1 hivyo utakaa mpaka ukome hata hivyo wanajinafasi kwa kuwa benki zetu hazifanyi kazi kwa ushindani zimewekeana mipaka we angalia nikisusa nbc afu niende nmb cheki hii picha si ntaamua kurudi tena NBC kwnai benki zingine ambazo ziko efficiency zipo dar tu ngugu kazi tunayo.
   
 8. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Wewe ndio hujui unalo liongea kaka......Pesa kama ni zako huna haja ya kusubiri fax masaa hayo zaidi ya nane... NBC wanatakiwa wawe na technolojia ya haraka ya kumtambua mteja wa account husika na si kutumia fax. Hiyo ni teknolojia ya zamani sana. KUSEMA KWELI NBC WANABOA SANA NA HUDUMA ZAO, NA PIA WANADHARAU SANA. Toka tuanze kulalamika kuhusu huduma zao ni siku nyingi sana, kama wangekuwa ni watu wanowajali wateja, wangeshajirekebisha...... KWA KWELI NIMEAMINI MSEMO USEMAO, MAKABURU NI WATU WENYE DHARARU SANA....

  SHAME ON NBC, AND ITS ALL MANAGEMENT TEAM
   
 9. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Bravoooooooo,
  Baelezeeeee baelewee hawo.
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi haya malalamiko yanawafikia?, inatakiwa pia ukipata usumbufu uchukue email uwaandikie. Nadhani kama kila mtu akilalamika na kuandika watasikia kilio cha wengi, japo hata kama wachache wanatakiwa kusikiliza wateja wao.
   
 11. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Ni kweil kabisa mkuu, Fax is totally outdated kwa issue ambazo ni urgent na sensitive kama pesa.

  Wawaige wenzao EMS MoneyFax, pamoja na kwamba wanajiita moneyfax lakini wanatumia internet kwa sasa, labda kama mkoa husika hauko connected. Zamani likuwa ukituma pesa inabidi hadi fax itumwe lakini toka ushindani wa M-Pesa, Z-Pesa na Scandinavia bus, huduma ya EMS kutuma pesa imebadilika sana, yaani ukishatuma tu ni mwendo wa yule dada wa counter ku-PLACE ENTER, unageuza mgongo pesa ziko mwanza tayari, I real like this kind of business competition! NBC mmebweteka sana, au ni kiburi????????????????????
   
 12. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #12
  Jul 30, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kwa hapa iringa naona kidogo wapo poa kwani mimi nilifungulia acount yangu dar es salaama, na niliweza kuchukua hela nyingi counter bila hata ya kuambiwa kuwa subiri fax toka dar es salaam. na nimekubaliwa kuchukua hela zaidi ya mara nne bila tatizo lolote. kwa pale dar es salaam panakera sana hasa yule mtu ambaye ndo anashugurikia fax na kuidhinisha kuweza kupewa hela.
   
 13. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Labda Naelewa vibaya lakini nafahamu ukiwa unachukua hela nyingi kama above 3m...huwa wana confirm na brach yako au...unaambiwa nenda Nje kwenye ATM.
  Print Risit ambayo itakuwa na jina laki na balance iliyopo...then unapata kiwango chako unacho taka.

  The same na CRDB..Kama account yako iko Kahama na wewe unataka kuchukua pesa mbeya.Lazima wa confirm na brach yako Kahama au the same way kwenda kwenye ATAM machine...print that ka risit.Barclays wao ni ndani card yako na kitambulisho chako cha kazi au mkazi...ili uweze pata vijisent.
   
 14. l

  lufuuo New Member

  #14
  Jul 30, 2009
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana sio system tu, ila watu ndio wenye shida. mana nafikiri katika bank ambazo watanzania wamejisau kuwa wao sio makaburu ni NBC. Hata wao wenyewe kwa wenyewe wananyanya sana mie nishuhudia ni uonevu tu. Nikujisahau tu,

  Nawashauri tu wafanyakazi wa NBC msijishau sana dunia ni kijiji hujui nani kesho atakutoa na wala Hujua Mungu anaweza kukushusha na wewe
   
 15. F

  Fechee2001 Member

  #15
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa usubiri wakianza kulipa wastaafu ndiyo utaudhika mpaka basi. Na ndiyo maana wazee wetu wakija chukua vihela vyao na wezi wako nyuma yao maana wanakuwa wamechoka mwanzo wa saa 12 asubuhi wako kwenye foleni mpaka network ya kichwa na halmashauri yote inachoka kufanya kazi, wanarudi hoi na kuibiwa juu! labda waende na watoto wao.
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  ndio ma graduate wa SUA hao......
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
 18. l

  loree New Member

  #18
  Jul 30, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli NBC wanaboa mbaya,
   
 19. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Assumming and hoping wanaangalia email ... :)
   
 20. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  hapana tena hapana mkuu NBC hawasomi kabisa email zao......ile anuani yao ya @nbctz.com ni pambo......
   
Loading...