NBA lock up - mchezaji awa utingo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NBA lock up - mchezaji awa utingo

Discussion in 'Sports' started by Candid Scope, Sep 30, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG][​IMG]
  Boston Celtics guard Delonte West, pictured above with another player
  who wasn't at Wednesday's lockout negotiating session, is ready to lug around his own set of heavy things.
  Furniture-type things. Complete with tightened screws; or at the very least an included Allen Wrench.
  [​IMG]


  Ligi ya basketball nchini marekani kutokana na kutoanza muda wake kwa sababu ya kutokufikia maafikiano kati ya wamiliki wa timu na wachezaji kuhusu mapato, msimu wa ligi umesitisha na hivyo hii lock up imesababisha baadhi ya wachezaji kukosa pesa za kuishia hadi kufanya kazi ya utingo kwenye malori.

  Ninachoshangaa hawa wanapata pesa nyingi sana, starehe wanavyoziendekeza bila kufikiria savings, sasa tangu wamalize ligi ni miezi 5 tu wengine wako hoi bin taabani.


  Picha ya chini: Employment application form aliyojaza mchezaji wa Basketball
  kupata kibarua cha utingo wa kupakia na kupakua furnicha kwenye lori amana picha ya juu inavyoonyesha
  [​IMG]
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  raha mbele kuliko kujihifadhi..
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Pato la mwaka mmoja kwa mchezaji wa NBA kiwango cha kati hata Rais wa Marekani hakamati. Wakati huo huo wakati wa msimu wa ligi hawatumii pesa ya mshahara wao ila timu inawagharimia. Sasa hizo pesa wanazimalizia wapi muda mfupi hivi hadi wachache kiasi hiki?

  NBA inatakiwa kuwapa darasa wachezaji kuishi kiuchumi badala ya aibu hii.
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu nyie hamuelewi Delonte ni kama ana paly a game na media na watu.The guy hata angekuwa vipi asingeweza kuwa broke kwa kipindi kifupi hicho.He has traded for $12.7Mil.Kama Hasheem anakula bata na $4mil huyu na mahela hayo sio kweli kauwawa.

  He's playing,fungua accont yake ya twitter soma tweet zake utajua he is serious au la
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Not true.
  Majuzi tu imetangazwa kwenye vyombo vya habari kwamba Kobe Bryant anakusudia kuwakopesa pesa zake baadhi ya wachezaji wenzake kutoka kwenye bank acount yake kutokana na wengi sasa hivi kuwa na hali mbaya. Hii ndiyo hali halizi, kwani wale wachezaji wenye majina ndio wanaopata nafasi ya kupeta ulaya sasa hivi wakati wakisubiria mlango kufunguka.

  Wachezaji wengi kwenda kustarehe kwenye mahoteli ya kifahali kulipia chumba tu kwa usiku mmoja zaidi ya $600, pamoja na gharama nyingine na starehe nyingine unafikiri pesa hiyo itabaki.

  Jambo la msingi kiasi kinachotajwa si ndicho anachopata mchezaji. Kuna kiasi kinachokatwa kwa ajili ya agent wake, makato ya shirika la NBA, kodi serikalini, kodi ushirika wa wachezaji nk. Kwa wastani kiasi anachobaki nacho mchezaji ni wastani wa 60% tu ya mapato yake. Na kuna tofauti ya kipato NBA kutokana na umaarufu wa mchezaji, kwani kila unapotumbukiza kikapuni ni pesa, sasa mwenzangu mie anayetumbukiza wastani wa point 2 tu kwa kila mchezo utamlinganisha na anayetumbukiza wastani wa over 25 points per game?

  Na ile mikumbo ya kwenda kufanyia starehe kule Holywood kwa mastaa, mwenye kipato cha chini ya kiwango chao utashtukia wiki pato lako umeshamkabidhi aliyewekeza pale na kujilaumu imekuwaje ati. Wengine wanakwenda kule wakati wamewekeza na wanachotumia ni profit, lakini mwezangu unaenda kustarehe kutokana na pazo lako lenyewe, maana yake ulaji wa mtasji siyo?

  Marekani si jambo geni hilo kwani miezi michache ilipigishwa la mgambo kumnusuru mchezaji wa football ya kimarekani, aka mpira wa sare ya helmet, pamoja na kutumbua ma $$$$ kwa miaka kadhaa, aliishia mansion yake kuweka rehani na kubaki homeless na hivyo kuomba mashabiki kumchangia.

  Wengi wa wachezaji wanatoka katika familia za kimaskini, hawana msingi wa kuishi kwa mfumo wa kiuchumi, na ndio unaona mtu anaenda nunua jumba la mlima wa kilimanjaro, utunzani wake tu kwa mwaka ni gharama ya bajeti ya wizara moja ya Tanzania. Na papo hapo michezo ni kama kamari, leo umebahatika na kesho utaona kibarua kimeota mbawa. Haya ndiyo yanayojilia kwa sasa. Tyson pamoja na mamilioni aliyopata kwa nafasi kadhaa ameishia bankrapt.

  Kuna umuhimu wa kuwafunza maisha ya kiuchumi wachezaji, maana starehe inawaharibia future na wenge elimu waliipa kisogo ndo maisha yanawaendesha kuliko mlalahoi wa kipato cha chini.
   
 6. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,346
  Trophy Points: 280
  Ngongoti hasheem thabit atajutia pesa alizokuwa anachezea.
   
 7. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,346
  Trophy Points: 280
  hilo bata hashem si anakula akiwa huku bongo..ajaribu kufunga bar pande za New york au hollywood kama ajafulia ndani ya wiki moja.
   
 8. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Delonte mzush anataka kusikika hawezi kulost hivo
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  [​IMG]
  Kuna vimwana kule Hollywood kazi yao moja kuchomoa pochi za wenye nazo, ndiyo yanayowapata vijana wengi wakishaanza tengeneza pesa bila kupima kesho itakuwaje.

  [​IMG]

  Hawa jamaa wako professiona kwa kazi yao, usipokuwa mwangalifu utashtukia kama huna akili vile ukawa una panga visarari visivyoisha. Wao kazi yao na kipato chao hutegemea ufundi wa kuwanasa wenye nafasi na pesa nzuri, ukafikiri umewapagawisha kumbe wanakupagawisha, ni ufundi tu. Na wengi wao ni wale wenye kofia mbili za umoja wa wanawake na shughuli za kujinafsi.

  Miaka miwili ijaya mambo yanalipuka WikiLeakis, kwamba mchezaji ameishiwa pesa anazolipwa na NBA sasa anahitaji msaana na msaada wa kwamza aliopata ni wa mjasirimali kuwa utingo kwenye lori.
   
Loading...