Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,325
- 152,136
Naanza kuyakubali maneno ya Waziri mmoja mstaafu kuwa Magufuli anawasimamisha kazi maofisa wa serikali kwa tuhuma mbalimbali kwasababu hakuwateua yeye hivyo inakuwa rahisi kuwatimua.
Kwa mtazamo wangu,Waziri huyu mstaafu bila shaka alimanisha kuwa atakaowateua yeye mwenyewe itakuwa vigumu kuwawajibisha kirahisi kama anavyofanya kwa hawa aliowakuta maofisini.
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa hali hii imeshaanza kujitokeza kwani mpaka leo hii teyari kuna wateule wake kadhaa teyari wametuhumiwa kwa mambo kadhaa lakini ni wazi kuna kigugumizi cha wao kuchukuliwa hatua.
Kwa mfano,kuna waziri mmoja ametuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya mwaka jana mwezi wa 9 katika sakata la kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi wakati huo akiwa waziri chini ya Kikwete ila mpaka sasa anapeta.
Waziri mwingine alituhumiwa kuvujisha siri kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo kabla ya Ziara ya Waziri Mkuu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uongozi ila naona nae amepeta!
Waziri fulani kijana kutoka Tanga nae alipata tuhuma ikimuhusisha yeye na dada yake kumtapeli fedha raia wa nchi fulani kashifa ambayo ilizua mijadala mitandaoni lakini akaishia kukanusha na sasa kimya!
Kuna mwingine anatuhumiwa kuteua raia wa Uganda na kumpa ulaji katika Taasisi fulani ya umma huyu nae sijui maamuzi yake yalikuwa sahihi au laa mimi sijui ila naona nae anapeta tu!
Hivi sasa kuna mjadala unaendelea kuhusu mteule wake mwingine aliekuwa CEO katika Taasisi moja kubwa tu ambapo Taasisi hiyo inatuhumiwa kwa ufisadi wa mabilioni ya shilingi ila naona mpaka sasa hakuna kinachoendelea huku mteule huyo akisubiri mahali atapopangiwa.
Naamini kadri siku zinavyosonga mbele orodha inaweza kuongezeka na hivyo Waziri yule mstaafu akawa sahihi kabisa.
Tukumbuke hawa wanaowajibishwa hutakiwa kukaa pembeni mara moja kupisha uchunguzi wa tuhuma juu yao sasa sijui labda hawa wengine tuhuma zao ni story tu za mtaani mimi sielewi!!