Naziogopa ajira za Serikalini kama ukoma

Naziogopa ajira za Serikalini kama ukoma

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,734
Ndizo ajira zilizo nilea, wazazi wangu, wajomba na mashangazi wote wamekulia na kuzeekea katika ajira za serikalini.
Lakini enzi zao zilikuwa peace. Mathalani, bosi akifanya kosa Dar Es Salaam, adhabu yake anahamishiwa (transfer) Lindi au Mtwara, akishajifunza 'kuishi na wakubwa' ndio anarudishwa mjini.

Lakini cku hizi nyakati za ari na nguvu mpya (japo imefifia) Ukibugi step kidogo, wanakutoa 'kafara' kesho na kesho kutwa mahakamani then unapelekwa Keko au Segerea kunyea debe! Yani ni shidaa. Kwa ajira za sasa za serikalini zinatia sana uoga kufanya maamuzi mapya. Nasikia mkuu wa chuo fulani huko Arusha kapandiswha kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka ya uma kisa wamemunua kajenerata! Si bora wakina 'Kayumba' walio tafuna pesa ya 'BOTI' hata wakifikishwa kwa pilato wanakuwa wamefaidi kweli kweli. Yani tukio la huyo mkuu wa chuo ndio limenitia uoga kabisaa wa kazi hizi...​
 
Ndugu kibao wanakula na kuhamishwa tu wewe unajidanganya bure hata huyo kanyaboya hiyo kesho na kesho kutwa mzigoni nenda kampuni uone wao direct wanakufilisi hawasubiri hata kwenda mahakamani
 
Mkuu Usedcountrynewpipo acha woga, halafu huyo mkuu wa chuo uliemsema hakununua kajenereta, bali anatuhumiwa kwa kujiuzia kifaa cha kuzalisha umeme wa sora mali ya chuo.
 
Last edited by a moderator:
mimi sijamuelewa huyo jamaaa anataka kuiibia serikali arafu aamishwe au kama enzi zamani? au
 
Back
Top Bottom