Nazama, naombeni ushauri wadau


Nashukuru kwa maswali yako yenye akili na pia utangulizi wako pale juu ni mzuri.
1. Nilienda kusoma sasa nimerudi na tupo mkoa mmoja ila kila nikimwambia kuonana anataka out za usiku na mimi siziwezi kutokana na mazingira ya nyumbani.
2. Muda umefika nadhani wa kuyaacha mapenzi ya simu.
3. Hapo sijui ulikuwa unamaanisha kuonana au kuoana?
kama kuona hapana,tulisema baada ya miaka kadhaa na haijafika bado na kama ni kuonana ndio kama hivyo mkaka anataka mambo ya night.
4. Kila nikitaka kumwambia nashindwa, naishia kuongelea swala lingine...:thinking:
5. Maumivu makali ni kua na mtu anae kuignore
 
Hii nchi hii sijui kama tutafika kwa mtaji huu yaani mtu anafall in love kwenye picha na hawezi kuachana na huyo mtu mmmmhh. Pole sana dada muombe Mungu atakusaidia
 
Does online dating amount to cheating?
 
hizi hadithi za MMU sasa zinachosha mpelekeeni shigongo mana ziko very unrealistic
 
This is where you see the difference in social networks, as in africa and developed countries though hata uzunguni wasiojielewa wapo. Mtu kaomba ushauri ni swala la kuamua ujibu sahihi au kama waona ni fix usijibu, pita tu au soma comments ucheke. Sio mbaya ni forum kila mtu anaruhusiwa kujadili, ahsanteni sana. Kuna jamaa alisema hongera kwa kurelease stress. Ahsante nimerelease and I feel much better than before. Think rationally/ act rationally......
(Stolen from human-computer Interaction theories)
 
2 years na bado hamjaonana na bado tu unamatumaini ya hayo mapenzi...Aasee kuna watu wameumbwa na subira zao....
 
Mambo ya imani usifananishe na tamaa zako za mwili.

Unampenda mtu kwa muda wote huo haujawahi kuwa naye walau hata mara moja mkiwa pamoja halafu bado unamuwaza labda ninachokiona hapa ni kwamba huna mtu wa kukugegeda ndo maana unamuwaza na kumuota usiyemjua.
 

ume kosa cha kupost bwahahahahahahahahaha ila pc2 washa kusaidia wenzio
 
una roho ya paka weye eti uta liasana acha ulimbuken miaka mwl hujaonana naye duh hiyo noma sana
 
Pole sana dada, hiyo ni dalili ya mvua yaani mawingu. Bila shaka uko nchi ya Wasukuma (sengerema), basi rejelea usemi wao maarufu kwa fasri isiyo rasimi"Jiongeze kama Bodo".
 
mi pia ni msomi na mtanashati,wiki ijayo nakuja senerema hebu nichek tuweze onana niweze kukushauri kwa kina kuhusiana na tatizo lako hili
 
we humpendi mungu wako?
 
Jibu maswali unayoulizwaili upewe ushauri kama ulivyoomba habari ya Kumpenda Mungu tusiye muona kulingana na iman Mungu yupo na anatenda kazi hata wewe kuomba ushauri ni kwa mapenzi yake hayo ya Mungu muachie yeye mwenyewe,

1. Umesema huwa mnawasiliana tu na hamjawah kuonana na mpaka sasa mnamiaka miwli ni sabab zipi zimewafanya kutoonana?
2. Huoni kutoonana kwenu kunatoa mwanya kwa mmoja wenu kuwa na mahusiano mengine na malengo yenu yakoje maana kwa miaka miwli kama haua malengo yoyote unapoteza muda?
 
Thanks Mariana kwa majibu yako.
Bahati mbaya nilikuwa mapumziko kwa ajili ya sikukuu hivyo sikuweza kukujibu kwa wakati.

Nilimaanisha kuoana hivi karibuni lakini umeshajibu kuwa mmewekeana muda (miaka kadhaa) ndipo muoane.
Ninaelewa ugumu wa mahusiano ya namna hiyo.Napenda kukushauri mambo machache

1. Unadhani huyo jamaa ni mtu sahihi wa kuja kuwa mume na mlezi wa familia? Kama jibu ni ndio tafuta muda mkae mzungumze na kumaliza tofauti zenu, uwe huru kumueleza aina ya mahusiano unayotaka,kama haupo huru kueleza hisia zako ni wazi kuwa hayo si mapenzi.

Kama jibu hapana,chukua hatua stahiki mapema,sijui una umri gani lakini kufanya mambo kwa wakati sahihi ni vyema zaidi.

2. Fanya jithada kuboresha maisha yako kwanza, kama ni kazi fanya kwa bidii kama ni biashara pia fanya kwa bidii. Mahusiano ni sehemu ya maisha lakini sio maisha yote. Maisha ni zaidi ya mahusiano.

Kwa jinsi navyoadika bila shaka wewe ni mtu mwema na unayejielewa.

Mwisho,you deserve the best dont settle for less.

Happy New Year.


 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…