Duuh harsh words umempatatizo ni ulishategemea mumeo ndio mtu wa kuendesha maisha yako, duka, maisha ya home na kila kitu.
Duka halikujiendesha kibiashara, kashindwa kukuletea bidhaa za wizi/ magendo duka limefilisika.
biashara ni art na ni profession, sio wizi. anza kuendesha bishara zako kwa kufuata professionalism na utaona matunda bila kutegemea tapeli (husband) wako
Tangu mume wangu apigwe stop job kwa kesi za ajabuajabu sasa hivi ni miezi 3, maisha yamekuwa magumu hadi nachanganyikiwa kupata mlo mmoja kwa siku nikushukuru, namimi duka langu limekombwa kila kitu yaani nimefulia kishenzi nadaiwa benki kama 5mln na baadhi ya watu wananidai pia sina amani sina raha nimeuza simu sipatikani hewani maana naona haya kila nikipokea phone ni deni nakumbushiwa nanimeshaangaika kutafuta kazi sipati na my hubby nae hapati nikuangaika huko na huko ilimradi maisha yasonge.
Sasa naombeni ushauri wenu wenu maana nimekata tamaa kabisa nawaza kwenda kujiuza labda ndio utakuwa msaada wangu ila nataka niwe naenda kwenye mahotel makubwa tuu nazani nitapata watu wenye fweza nyingi maana nachohitaji ni mshiko tuu nasio mapenzi maana nina mume nasitatamani anibambe japokuwa hili wazo langu nilipolitafakari kwakina nilijikuta nikilia kwa uchungu sana siamini kama maisha yamefikia hapa sina namna nafamilia inanitegemea kodi za nyumba na majukumu mengine pamoja na hayo madeni sijui pakuanzia.
Naombeni ushauri niende hotel gani kubwa ambayo nirahisi kujitegesha nikapata vichwa? sitaki mabuzi wala wapenzi ni biashara tuu ili nijikim kimaisha hadi hapo mambo yatakapo kaa sawa msinielewe vibaya sina tabia hii mbaya hizi ni changamoto za maisha nataka kupambana nazo hivyo sina budi kujisacrifirz
Mama, ya leo kwangu imekuwa mpya kabisa. Ukaja na wazo lako timilifu kabisa kuwa tukuelekeze Hoteli nzuri ya kupatia vichwa vya kupeleka kule baharini usiku kucha ili asubuhi uwahi kurudi home kabla watoto hawajaamka uwape chai na maandazi uliyochuma kwa kuuza mwili wako. Oh! Poleeee
Mama sikiliza vizuri sana; Kama huyo mumeo akithubutu kukutuma ukajiuze ili mje mle, huyo si mwanaume! Ni boya tu. Haiwezekani athubutu kukuambia; Ongeza mboga hapa. Utamjibu nini??
Pili, kudaiwa mbona kawaida tu?? Serekali yako yenyewe inadaiwa mpaka rais anaona aibu kwenda kuomba tena mkopo. Iwe ni weye mtu binafsi?? Mabenki yoote unayoyaona, yanaendesha shughuli zao kwa kukopesha watu kama weye. Ukitaka kupata shida duniani, Toroka deni la benki yeyote. Wanaambiana warushi na matapeli. Hutakopa popote. Ila, ukimwendea mdai wako, ukamweleza tatizo lako, mbona watakuongezea mtaji ili uweze kurudisha hiyo fedha yao?
Mumeo naye achacharike, asione aibu.
Mie ni shuhuda live; Niliwahi kusahau kisomo changu, nikaacha cheti changu cha chuo kikuu ndani, nikabeba mwiko wa kujengea na karamala nikaenda mitaani kutafuta kibarua cha kujenga. Baada ya miaka 2 nikipitapita mitaani kama fundi ujenzi ndipo nyota yangu ikawaka tena. Nikapata nami contract. Hunijui hivyo nikikuambia nina magari na ofisi huwezi amini. Nikikuambia leo naajiri nami watu huwezi amini. Kile kipindi kilikuwa ni shule yangu ya maisha.
Mke wangu, ndoa yetu ni zaidi ya miaka 35 hajaenda kujiuza mwili ili nile. Miezi hiyo 3 tu tayari umeona mtaji pekee ni pichu yako; we vipi. Kaa na mumeo, zungusheni akili, nendeni kwenye hizi taasisi za fedha wala msiende kwa watu, mtadhalilishwa huko.
Ukimwendea shem anataka uvue pichu, ukimwendea dadako anasema unamletea wanga uje umwue umrithi. Nenda kwenye hizo taasisi zilizokuzunguka weye. Ni kaushauri tu
we vumilia mtihani huo utapita tu..usifanye ufuska mana utaharibu maisha yako jumla na ndoa yako utaivunja..
madeni hayauwi wala hayafungi mtu, ilimradi unajua unadaiwa we vumilia utapata kazi na utayalipa..
labda nikuulize kwani hamna hata ndg wa kuwasaidia japo kamtaji kengine ili muanze tena biashara? mana kweli hali ilivyo kuishi bila kazi ngumu sana..
umesoma mpaka wapi? chuo/ sekondari au? jishushe uanzie chini, uza mandazi, ndizi n.k na huyo mumeo asilale ndani atoke aende kutafuta riziki popote kwani waswahili wanasema mtembea bure sio sawa na mkaa bure..
kuna vijana huku posta wanaosha magari tu, au wanaelekeza watu pa kupaki magari wanapata hela ya mboga lkn wangekaa nyumbani wasingepata..apige hata kiwi/kuuza magazeti ilimradi wtt wasife njaa..mwanaume haoni aibu kutafuta riziki