Sina hakika kama Tanzania kuna Benki yoyote inayotoa credit card, ila ninachojua karibu benki zote zinatoa debit cards ambazo zinaweza kuwa mastercard, visacard au UnionPay. Karibu card zinazotolewa na benki zote either ni mastercard au visacard au UnionPay kwa hiyo unaweza fanya manunuzi mtandaoni.
Ila kama shida yako ni kufanya manunuzi tu na malipo mtandaoni nakushauri utumie airtel mastercard, ni rahisi maana ukiwa na airtel money tayari una airel mastercard ni ku request tu namba za card na CVV na expire date. Pia ina makato cheap kabisa.