Guacamole
JF-Expert Member
- Mar 19, 2019
- 6,230
- 16,490
..
Ilikuwa ni siku ya ijumaa, maeneo ya kariakoo.
Ni baada ya kumaliza kipindi cha mchana pale chuoni, nikaona niingie mjini kariakoo maduka ya chini kucheki nguo kadhaa kisha nigeuke mtaani niianze weekend kibosi kabisa.
Nikiwa ndani ya gari za T/Segerea, siti ya nyuma kabisa karibu na dirisha nikiwa nimejiinamia kutokana na uchovu wa safari na mwendo mule mjini. Nikapachika earphones masikioni taratiibu zikinibembeleza huku nikiuvutia kasi usingizi.
Baada ya dakika kama 5 hivi gari lilikuwa almost linakaribia kujaa huku kukiwa na baadhi ya nafasi nyuma.
Hivyo ikawa sio kesi, dereva akaanza maandalizi ya kuinua.
Dereva aliwasha ndinga na kuanza kuchomoka taratibu.
Gari haikutembea sana, mara ikakanyagwa breki kuchukua abiria mwengine aliyekuwa akisubiri usafiri njiani.
Nilipoinua macho, sikuamini nilichokiona. Alikuwa ni mrembo mmoja machoni alionekana ni wa moto sana, chuchu ndizi na moja kwa moja macho yalishuka mpaka chini kujiridhirisha kwenye kipengele kilichobaki.. haah!! Nilihisi moyo umeishiwa nguvu.
Akilini nikawa najiuliza, inawezekana vipi mwanamke kukamilika kuanzia uzuri wa sura mpaka maumbile?! Maana yule duu alikua amechanika ipasavyo.
Basi buana!
Kutokana na uhaba wa siti pale mbele ilimlazimu yule dada aje kusiti nyuma, right beside me! Nikazidi kuchanganyikiwa.
Akili yangu iliniambia nikaze lakini kuna nafsi ya pili ikaniambia niache ujinga.
Kwahiyo baada ya kujifikiria sana ikabidi nianze kusalimia na kuanza kujitambulisha.
Na kweli nilifanikiwa na story zilinoga na mwisho kabisa nikafanikiwa kuchukua namba zake za mawasiliano.
Usiku wake tulichat sana japokuwa hakuonekana mchangamfu.
Ikabidi tukubaliane kuonana kesho yake, ambayo ndio jana jumamosi.
Mida ya saa 8 mchana, tukakutana tena kwenye mgahawa mmoja hivi maeneo ya Baracuda.
Tukapiga misosi na vinywaji huku story zikiendelea. Mwisho kabisa, nikamuelezea lengo la kumuita pale kuwa ningependa sana kuwa nae.
Ulipita ukimya, takribani dakika 1 yule msichana hakuongea. Kwa haraka haraka tu, nilihisi kuwa ni lazima atakuwa kwenye mahusiano.Kwahiyo sikutaka kwenda huko, ikabidi nimuulize kama kuna tatizo jengine lolote.
Ndipo mwishowe akaja na jibu chungu ambalo liliharibu pozi lote kwa wakati ule.
Mrembo akanifungukia kuwa AMEWAKA, kiswahili kizuri ni kuwa ameathirika!!
Sikuwa na hamu tena kwa muda ule! Sikuamini kama kuna warembo wa namna ile walioathirika.
Story hazikuendelea tena, ikabidi tumalizie vilivyobaki kisha tufunge maongezi kila mmoja arudi kwake.
Bado naendelea kuchat nae mpaka sasa. Anasema alijua kuwa baada ya kuniambia ukweli, nisingekuwa na hamu tena naye. Lakini kwake ndio best option ever! Ameona ni bora kuongea ukweli.
Nahisi nimeanza kumpenda, ila nina swali muda wote zinazunguka kichwani mwangu kwamba..
NAWEZAJE KUANZA MAISHA NA MUATHIRIKA?