Naweza Kumjibu Muhongo

Naweza Kumjibu Muhongo

Bado hajaongea Werema na PM nadhani hao watatoa majibu ya maswali uliyoyauliza. Yeye amejibu kwa maeneo yanayomhusu yale yanayomhusu mwanasheria mkuu yatajibiwa wakati muafaka utakapofika. Uwezo wa kujibu hoja bila jazba wala papara na kwenye upinzani mkali ndio weledi tunaoutaka kwa wabunge wetu hasa wale wanaoishia kuzomea pale wanapoishiwa hoja.
 
Com'on, what are you trying not to say here?

IPTL ipo inadai au PAP ndiye IPTL? Nani anatakiwa kulipwa hizo fedha unazotaka kuzileta hapa?

BTW, source ya taarifa ya PAC ni CAG, PCCB na TRA. Wewe source yako ni ipi?

Uwizi wa watumishi wa serikali kupitia PAP, ndiko kulililpa deni unalolisema la IPTL?

Hao kina Chenge, Tibaijuka, Ma jaji 3, mfanyakazi wa tRa, Kilaini, Ngeleja na wengine wote, ndio IPTL ama ndio walikuwa wanaidai IPtL?

Please brother, you must be kidding!.

:boxing:

IPTL also they need there Money back.

TANESCO na IPTL kufanya Reconcillation ya fedha iliyokuwa kwenye Akaunti ya Escrow

Mheshimiwa Spika, TANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki (reconciliation) tarehe 9 Oktoba, 2013 ili kujua madai halali ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Takwimu za Mfilisi wa Muda wa IPTL (RITA) wakati akikabidhi mali na madeni ya IPTL, ilionesha kwamba deni lote alilokuwa akidaiwa TANESCO na IPTL kama Capacity Charges ni Shilingi bilioni 370.70, sawa na Dola za Marekani milioni 224.30. Katika majadiliano kati ya TANESCO na IPTL, gharama zilizokubaliwa kama Capacity Charges zilizokuwa zinadaiwa ni Shilingi bilioni 275.20. Fedha hizi ni pungufu kwa Shilingi bilioni 95.50 ya madai ya IPTL. Hadi kufikia tarehe 25 Novemba 2013, fedha iliyokuwa katika Akaunti ya Escrow ilikuwa jumla ya Dola za Marekani milioni 22.20, sawa na Shilingi bilioni 36.72 na Shilingi bilioni 161.39.

Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum umeonesha pia kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow wakati wa kuifunga ni Shilingi bilioni 182.77 na kuwa na upungufu wa Shilingi bilioni 123.90 wa madai ya IPTL.
 
Umejitahidi kwa uchambuzi jadidifu.. Pitia Rose Garden upate bia zako mbili maana umewaelimisha wengi!!
 
Kabla sterling wa Tegeta Escrow Account Saga, Zitto Kabwe hajarudi kusambaratisha majibu ya serikali yaliyosomwa leo na Waziri wa Nishati na Madini, sospeter Muhongo.

Au kabla komando David Kafulila hajashuka na ile style yake ya kushambulia kama tumbili, hebu kwanza nami nimjibu Muhongo kwa kifupi...

Utetezi kwamba Tanesco inadaiwa sana, eti wakaona fedha za Tegeta Escrow zitolewe kwa PAP ni pumba.
HOJA: Kuchotwa kwa fedha za Tegeta Escrow, hakusaidii madeni yaliyotajwa na Muhongo kufutwa.

Yataendelea kuwepo, vilevile Tanesco itaendelea kudaiwa. Msingi wake ni kwamba zile pesa zilitolewa kwa PAP kama fedha zake stahili baada ya kughushi nyaraka za kujihalalisha umiliki wa IPTL.

Hata kama ingekuwa hivyo, wapi yalipo maandishi kuwa kuchotwa kwa fedha za Tegeta Escrow, kutasidia kuondoa madeni ambayo ameyataja? Au aliyataja kama stori ya kutapatapa?

Ukweli unabaki kuwa fedha za Tegeta Escrow ni za Watanzania. Zilichotwa kifisadi.
Utetezi kwamba waliamua fedha za Tegeta Escrow zitoke ili kujinasua na mzigo wa kuwalipa mawakili ni dhaifu sana.. tena sana!

HOJA:
Ni mtu asiyejali peke yake ndiye anaweza kuruhusu hazina ya taifa ichotwe, eti kwa sababu ya kuona mawakili wanaoitetea Tanesco dhidi ya tozo kubwa la IPTL, wanalipwa fedha nyingi. Yaani umenunua bidhaa dukani, baadaye unagundua mwenye duka alikutoza fedha nyingi kinyume na uhalisia.

Unamtuma mtu akakudaie, yule mtu anakuomba nauli. Eti kwa kujiuliza kwa nini umlipe yule mtu nauli, unaamua kumsusia fedha zote mwenye duka, wakati ilikuwa wazi kuwa mwenye duka alipaswa kurejesha fedha zote za ziada alizokutoza na fidia juu. Hoja ya pili ni kuwa kwa nini serikali haikutumia njia nyingine kuhakikisha haki ya Tanesco haipotei? Ni wazi uamuzi uliochukuliwa ni uzembe na ufisadi.

Wakati wa Bunge la Bajeti mwaka huu, Muhongo, Werema (mwanasheria mkuu wa serikali) na Pinda (waziri mkuu), kwa nyakati tofauti walisema fedha za Tegeta Escrow ni za wanahisa wa IPTL, na kwamba akaunti hiyo ilifunguliwa kutokana na mgogoro wa wabia wa IPTL.

Leo, Muhongo amekubali kuwa akaunti ya Tegeta Escrow, ilifunguliwa kutokana na Tanesco kulalamika kuwa IPTL inaitoza tozo kubwa la capacity charges. Utetezi wote wa Muhongo umeshindwa kujibu hoja kuwa fedha za Tegeta Escrow Account ni za umma, na kwamba zilichotwa kifisadi.

Hajajibu pia kwa nini katika Bunge la Bajeti, kwa kushirikiana na Werema pamoja na pinda, walilidanganya bunge na umma kuwa akaunti ya Tegeta Escrow, ilifunguliwa kutokana na mgogoro wa wabia wa IPTL?

Kuhusu Mwanasheria wa Tanesco aliyefukuzwa kazi kwa kutoa ushauri wa kuikataza serikali isimuamini Sethi (Singasinga), Muhongo ametetea, lakini hajajibu hoja ni kwa nini bodi ya Tanesco na wizara ya nishati na madini, hawakufanyia kazi ushauri ambao mwanasheria huyo alitoa kwamba uuzaji wa hisa kutoka Piper Links kwenda PAP ni magumashi kwa sababu katika mauziano, makampuni hayo mawili yaliwakilishwa na mtu mmoja ambaye ni Sethi. Kwa nini hili hawakuzingatia?

Muhongo hajajibu hoja ya Kamati ya PAC kuwa Piper Links ni kampuni hewa, usajili wake hautambuliki kwenye nchi yoyote duniani, sasa serikali iliiamini kwa ushahidi upi ikiwa ni kampuni hewa?

Muhongo hajajibu hoja kwa nini serikali iliruhusu PAP ichukue fedha za Tegeta Escrow wakati hukumu ya Jaji Utamwa haitamki popote kuwa kampuni hiyo ipewe fedha hizo? Na kwamba Jaji Utamwa aliridhia PAP ikabidhiwe mitambo ya IPTL tu. Kwa nini fedha zimetoka? Hajajibu.

Hajatoa majibu ni kwa nini PAP iliaminiwa na serikali wakati haikuwa na hati halisi za hisa 7 (asilimia 70) ambazo mmiliki wake halali ni Kampuni ya Menchmar ya Malaysia?

Muhongo hajajibu pia serikali itafanya nini endapo Menchmar wataishtaki serikali kwa kuikumbatia PAP na kuipa rasilimali zake wakati haijaiuzia hisa zake saba (asilimia 70).

Muhongo amejitetea kuwa yeye si dalali aliyeyakutanisha makampuni ya PAP na VIP. Ila hajamkana MD wa VIP, Rugemalira aliyeiambia kamati ya PAC na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali (CAG), kuwa Muhongo ndiye aliyewakutanisha Sethi na Rugemalira kisha kusimamia mauziano ya hisa tatu (asilimia 30) za VIP kwenda PAP.

Muhongo hajajibu ni kwa nini mtu mwenye mtaji wa shilingi milioni 500, anaweza kupewa shilingi bilioni 321 bila kuzifanyia kazi?

Hajajibu ni kwa nini PAP ililipwa fedha za Tegeta Escrow kwanza kisha ndiyo ikapata uwezo wa kununua hisa asilimia 30 za VIP?

Muhongo hajawafanya Watanzania wafunge midomo yao, maana tangu jana Ripoti ya PAC kuhusu Tegeta Escrow Account Scandal iliposomwa, wamebaki midomo wazi kwa mshangao, iweje hisa asilimia 30 zinunuliwe kwa dola milioni 75 (karibu shilingi bilioni 124) wakati hisa asilimia 70 za Menchmar, eti PAP ilizinunua kwa shilingi milioni sita tu (6,000,000)? Uwiano hapo upo wapi kama si wizi?

Muhongo akasema issue ya kukwepa kodi na kuikosesha mapato serikali katika tukio zima la uchotwaji fedha za Tegeta Escrow, eti PAP ipo, inaweza kudaiwa kodi wakati wowote na italipa.

Muhongo anajifanya hajui kama kesi ya kukwepa kodi si ya kudaiwa kodi. Ukwepaji kodi ni uhujumu uchumi na adhabu yake ni kifungo jela na hata kufilisiwa. Muhongo hajui hili? Au analeta sanaa kwenye jumba la sanaa?

Kamishna wa TRA na CAG, wamesema kwa hoja za kitaalamu na kimahesabu kama walivyohojiwa na Kamati ya PAC kuwa fedha za Tegeta Escrow Account ni za Watanzania, Muhongo anakuja na blah! Blah!

Kwa kifupi Muhongo hajajibu hoja za msingi, isipokuwa alijitahidi kuupaka sukari utetezi wake ili uwe mtamu kwa wasikilizaji lakini imeshindikana.

Ila salute kwa Muhongo; Tofauti na wanasiasa wengi ambao wanaposhambuliwa au kubanwa kwa hoja hupaniki, hupayuka na hata hutukana, Muhongo ni tofauti sana, ana uwezo mkubwa wa kujieleza bila jazba, tena kwa utulivu. Ndiyo maana mara nyingi huko nyuma, wabunge waligeuka mashabiki wake, hata pale alipodanganya au kukashifu wenzake kwa sababu ya kipawa hicho alichojaliwa. Huongea kwa upole na ni rahisi kuteka wasikilizaji kuamini na kushangilia kila anachokisema.

Hata leo, wabunge licha ya kumzomea mara nyingi, alikuwa imara kuzungumza. Hiki hasa ni kipaji cha Muhongo.

By Luqman Maloto (The Gladiator)

Huyo Muhongo asituzuge bado anajikanyaga maswala ya msingi yote hajajibu
 
:boxing:
Fedha za escrow siyo mali ya umma.

Mheshimiwa spika, Ili kuthibitisha kwamba fedha hizi siyo za Umma, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukaguzi wake wa Hesabu za TANESCO wa tarehe 31 Desemba 2012, alielekeza kutoa fedha za Escrow kwenye Vitabu vya Hesabu vya TANESCO na kupunguza deni kwa kiasi hicho hicho kwa maelezo yafuatayo:

“As a result, the deposit balance in Escrow account does not meets the definition of an asset of the Company and therefore an adjustment has been made to de-recognize the asset and related liability to the tune of the amounts available in the Escrow account”.

Ntakusaidia kuelewa kama utapenda.

Una mkataba wa mafuta say from kampuni XYZ kwa sh. 120 kila mwezi(vat inclusive).

Kisha ukagundua malipo ya sh.120 ni ya kinyonyaji. Unaomba msuluhishane lakini uendelee kulipia huduma kwa sh.120 (kwenye account maalum).

Suppose baada ya miezi 10 kwenye account zimefika sh.1,200. Mdhamini wa account yenu akamlipa XYZ pesa yote kiujanja wa kisheria.

Tafasiri yake ni kwamba XYZ kachukua na kodi ya (VAT) ambayo ni pesa ya umma.

Lakini pia amechukua na chenji yako endapo bei ingeafikiwa kuwa pungufu ya sh.120 kwa mwezi.

Kumbuka Tanesco amelipa tozo ikiwa va VAT ndani yake, ni jukumu la mlipwaji kuwasilisha VAT itokanayo na mauzo.

Sasa VAT imepigwa na uwezekano wa chenji kwa Tanesco umepigwa pia.....Hiyo ndo mali ya UMMA.
 
VAT italipwa ndio maana serikali ilisisitiza kuwe na kitu hiki;

"IPTL do hereby agree to INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all present and future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or all losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the Tegeta Escrow Account or part thereof to IPTL pursuant to the Agreement for Delivery of Funds".

Leo mmelowa mnadai chenji na sio mabilioni yake mliokuwa mnayatamka, teh teh teh teh! Hakuna chenji wala hakuna fedha ya umma kwenye escrow account na TANESCO bado INADAIWA na IPTL.

hashki majinuni nyie!!
:boxing:
 
Ntakusaidia kuelewa kama utapenda.

Una mkataba wa mafuta say from kampuni XYZ kwa sh. 120 kila mwezi(vat inclusive).

Kisha ukagundua malipo ya sh.120 ni ya kinyonyaji. Unaomba msuluhishane lakini uendelee kulipia huduma kwa sh.120 (kwenye account maalum).

Suppose baada ya miezi 10 kwenye account zimefika sh.1,200. Mdhamini wa account yenu akamlipa XYZ pesa yote kiujanja wa kisheria.

Tafasiri yake ni kwamba XYZ kachukua na kodi ya (VAT) ambayo ni pesa ya umma.

Lakini pia amechukua na chenji yako endapo bei ingeafikiwa kuwa pungufu ya sh.120 kwa mwezi.

Kumbuka Tanesco amelipa tozo ikiwa va VAT ndani yake, ni jukumu la mlipwaji kuwasilisha VAT itokanayo na mauzo.

Sasa VAT imepigwa na uwezekano wa chenji kwa Tanesco umepigwa pia.....Hiyo ndo mali ya UMMA.

Mkuu hichi ulichokisema ndio msingi mkubwa wa sakata lote la Escrow.
Hapa mtu asitake kufahamu lakini ni swala ambalo lipo wazi kabisa.
 
VAT italipwa ndio maana serikali ilisisitiza kuwe na kitu hiki;

“IPTL do hereby agree to INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all present and future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or all losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the Tegeta Escrow Account or part thereof to IPTL pursuant to the Agreement for Delivery of Funds”.

Leo mmelowa mnadai chenji na sio mabilioni yake mliokuwa mnayatamka, teh teh teh teh! Hakuna chenji wala hakuna fedha ya umma kwenye escrow account na TANESCO bado INADAIWA na IPTL.

hashki majinuni nyie!!

Watu kama nyinyi ndo inayoifanya nchi hii kuonekana inalaana..ila ipo siku hata kama itapita miaka mingi ukweli utajulikana tu siku zote ukwel ujitenga na uongo..shame on you.....!!
 
Hatuongelei pumba onyesha documentation kama alivyofanya muhongo hapa sio kijiwe cha kahawa

Vp bwana Ngwilimi alijipeleka mwenyewe Malaysia? Yaani mtumishi ''anajipeleka'' mwenyewe nje ya nchi.
 
Attachments

  • 1417129743190.jpg
    1417129743190.jpg
    74.1 KB · Views: 90
  • 1417129771722.jpg
    1417129771722.jpg
    97.6 KB · Views: 93
:boxing:
Fedha za escrow siyo mali ya umma.

Mheshimiwa spika, Ili kuthibitisha kwamba fedha hizi siyo za Umma, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukaguzi wake wa Hesabu za TANESCO wa tarehe 31 Desemba 2012, alielekeza kutoa fedha za Escrow kwenye Vitabu vya Hesabu vya TANESCO na kupunguza deni kwa kiasi hicho hicho kwa maelezo yafuatayo:

“As a result, the deposit balance in Escrow account does not meets the definition of an asset of the Company and therefore an adjustment has been made to de-recognize the asset and related liability to the tune of the amounts available in the Escrow account”.
......msijichanganye kuhusu definition of an asset na ownership to the Company. Report ya CAG haijasema kuwa the deposit is not owned by the Company bali can not be defined as an asset.
 
Back
Top Bottom