josephwaara
JF-Expert Member
- Jun 18, 2016
- 304
- 641
Sawa mkuu ila shida yangu kubwa ni watoto kupata haki ya kutambulika kama mimi ni baba yao, ndo nawaza pengne lile jina lirasimishwe kama jina langu hata kama sitobadili hili la sasa.Nenda Rita Kule watakupa mwongozo. Ila nadhani lazima upite mahakamani uapishwe na hakimu kuwa majina yote ni ya kwako. Baada ya hapo Kule Rita wanafanya mabadiliko. Ila sasa:
1. Kwenye vyeti itabidi ufatilie upya upate vyeti vebye current name.
2. NIDA pia lazima upite.
3. Kwenye voters ID
Kama utaona kazi kubadilisha la kwako. Basi mtoto kama hujampatia cheti Cha kuzaliwa Inakuwa rahisi. Kama anacho inabidi upite mahakamani na Rita.
Ushauri mzuri ni kuwa badili ya mtoto kwako una vyeti vingi kazi itakuwa kubwa. .
Sasa unaweza kuwa na vitambulisho viwili?Sawa mkuu ila shida yangu kubwa ni watoto kupata haki ya kutambulika kama mimi ni baba yao, ndo nawaza pengne lile jina lirasimishwe kama jina langu hata kama sitobadili hili la sasa.
Kwani siwezi kumiliki majina mawili??
Mkuu, kesho ndio "Last Seen/Comment" yangu humu jamiiforums. Tutaonana tena October 2024 (Miezi 23 kutoka mwezi huu).Sawa mkuu ila shida yangu kubwa ni watoto kupata haki ya kutambulika kama mimi ni baba yao, ndo nawaza pengne lile jina lirasimishwe kama jina langu hata kama sitobadili hili la sasa.
Kwani siwezi kumiliki majina mawili??
Dah yaani changamoto yako kama yangu aseeWakuu heshima kwenu, naomba msaada katika suala hili.
Nilipofikisha umri wa miaka 10 niliugua sana, katika kutafuta tiba mzazi wangu akakutana na ushauri wa mimi kutumia jina jingne (nimefupisha story).
Sasa ishu hilo jina nikaja kusajiliwa nalo shule na kutumika kwenye vyeti vyote vya shule na cheti cha kuzaliwa. Hivyo ninafahamika kwa majina mawili tofauti kulingana na maeneo, sasa nimekuwa na nimepata mtoto na katika kumsajili nimetumia jina langu la awali ambalo linafanya sasa huyu mtoto aonekane siyo wangu kwa kuwa jina la baba ni tofauti.
Ninaweza kufanya nini ili niweze kumpatia bima ya afya? Solution ninayowaza ni mimi kubadili jina lirudi awali. Je itakuwaje wakati vyeti vyangu vyote vya taaluma na cha kuzaliwa vinasoma jina tofauti na lile la kuzaliwa?
Naomba mwongozo mkuu hili suala linantesa mno.