Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,235
- 4,382
Kufanya kosa sio kosa, ila endapo ukiendelea kukosea baada ya kulitambua kosa lako la awali, hapo yafaa kabisa wewe kuwekwa kwenye kundi la wapumbavu!
Ujumbe huo uwaendee ACT Zanzibar; waliojitumbukiza kwenye chama la wana, wakakutana na kabali ya mwana - ZZK! Mwana ambaye huu mwaka wa 10 sasa ametumia nguvu ya ACT Zanzibar kama dhamana ya kujitengenezea nafasi ya kuibagaza demokrasia kotekote - Bara na Visiwani.
Kwasisi tuliosoma harakati za Maalim Seif Sharif Hamad na namna alivyokuwa anapambania haki kwenye ardhi ya wazanzibari, Zanzibari ambayo ilikuwa, na bado inayo, mgawanyiko mkubwa kwenye jamii yake kati ya Waafrika, Washiraz, Waarab, Wahindi, na Wacomoro; ni wazi, muunganiko wa ZZK na ACT Zanzibar, haujazaa tija ya kupambana na matatizo lukuki kwenye jamii ya wazanzibari, ikiwemo kuzisikiliza sauti za wazanzibari zilizojificha.
Kulingana na aina ya demokrasia ya chama cha ACT Wazalendo, kuna hatari ya kuwafanya ACT Zanzibar kama tawi la CCM huko Zanzibar, ikikinzana kabisa na historia ya mapambano ya haki na demokrasia yaliyopambaniwa kwa jasho na damu na Maalim Seif Sharif Hamad
Kwa mwenendo wa sasa, kuna hatari ya kutozisikia sauti za wazanzibari wanaopigania haki na uhuru wa kidemokrasia.
Ikiwa ACT Zanzibar wanataka kurejesha mapambano ya kweli ya haki, hawana budi kujinasua kwanza kwenye mikono ya vibaraka wa CCM; hawana budi ya kung'oka kwenye kabali ya ZZK!
Walifikirie na hili!
MC