Aisee kiongozi, hukunijibu issue yangu ya deferred taxation
Mkuu niwie radhi, nilidhani nilishakujibu.
Ngoja nikujibu kuhusu deferred tax liability
Kabla sijasema deferred tax liability inavyotazamwa katika macho ya sheria ya kodi ya mapato wacha kwanza nieleze deferred tax liability ninini.
International Accounting standard 12 (IAS 12) imeeleza namna na jinsi deferred tax liability inavyotokea na jinsi ya kurecord kwenye vitabu.
Mtaniwia radhi maana sina utaalamu sana wa kutafsiri Kiswahili. Nitakuwa nachanganya lugha.
Maana ya deferred tax liability according to IAS 12 is any temporary difference that in reversing itself causes taxable income to be higher than the financial (book) income. Yaani kwa kawaida kuna kitu kinaitwa financial accounting na kingine kinaitwa tax accounting. Financial accounting are governed by International Accounting Standards na Tax Accounting are governed by Tax laws.
Kampuni inatakiwa kwa mujibu ya sheria za makampuni (kwa Tanzania the Companies Act, 2002 Cap 212) kutengeneza mahesabu ya mwaka kwa ajili ya kupeleka return kwa registrar wa makampuni na pia kwa ajili ya kodi (returns kupelekwa kwa Kamisha wa Mamlaka ya mapato).
Kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 mahesabu hayo yanatakiwa kutengenezwa chini ya kifungu cha 80 na kifungu cha 91. Mahesabu hayo yanapomfikia Kamisha wa Mamlaka ya Mapato anatakiwa ayafanyie uhakiki kwa kufanya adjustment ili yaendane na sheria za kodi ya mapato. Amepewa mamlaka hayo chini ya kifungu cha 94(3) na au 96(1) cha sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 sura namba 332.
Sasa wakati wa kufanya "adjustment" kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato, ni lazima itapatikana tofauti ya kodi kati ya mahesabu kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato na mahesabu yaliyotengenezwa kwa kufuata International Accounting Standards. Kwa kawaida deferred tax liability inatokea pale kodi (tax payable)iliyopatikana kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato (Tax accounting) ni kubwa kuliko kodi iliyopatikana kwa mujibu wa mahesabu yaliyotengenezwa kwa kufuata International Accounting Standards (IAS) ama Generally Accepted Accounting Practices (GAAPs).
Hebu tuone accounting treatment ya deferred tax liabilities.
Dr. Deferred Tax Liability…………xx(Tofauti kati ya kodi kwa mujibu wa tax accounting na ile inayotokana na financial accouting-kama tulivyoona deferred inapatikana ikwa tax as per tax accounting is higher than tax as established by Financial Accounting).
Dr. Tax Expense………………………xx(Iliyopatikana kwa mujibu wa mahesabu ya uhasibu)
Cr. Tax Payable…………………………………….xx(Iliyopatikana kwa mujibu wa sheria ya kodi)
Nini husababisha kodi itofautiane?
Vipo vitu vingi lakini kikubwa ni depreciation! Kwa mujibu wa mahesabu yatengenezwayo kwa mujibu wa International Accounting Standards ikiwa kubwa wakati ile depreciation inayopatikana kwa mujibu wa sheria za kodi ikiwa ndogo then tax payable itakuwa kubwa kwa hesabu zilizotengenezwa kwa kufuata sheria ya kodi. Kwa hiyo kodi iliyopatikana kwa mahesabu ya kihasibu itakuwa ndogo kuliko kodi iliyopatikana kwa mahesabu ya sheria za kodi. Ile tofauti ndiyo ijulikanayo kuwa ni "Deferred Tax Laiability….."
Kinyume cha deferred tax liability ni deferred Tax Asset
Sheria ya kodi ya mapato inasema nini kuhusu deferred tax?
Kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato sura ya 332 haisemi chochote kuhusu deferred tax liability ama deferred tax asset.
Kamishna amepewa mamlaka ya kurekebisha mahesabu ya mlipa kodi yaendane na sheria za kodi, kwa hiyo that income iliyokuwa deferred ama kodi iliyokuwa deferred ataiona wakati anahakiki mahesabu ili akokotoe kodi yake. Therefore, deferred tax liability ama assets au deferred income ataihakiki uhalali wake na mwisho wa siku atakokotoa kodi yake.
Kama nimekujibu ama kama nimeanzisha mjadala mwingine nawakaribisha nyote kuniuliza maswali.
NB. Mnisamhehe kwa Kiswahili kibovu ama kiingereza kibovu. Stick to the points ili twende sambamba.