Ushauri wangu kwa Serikali kuhusu vitambulisho vya NIDA

Author

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
1,709
8,007
Niende moja kwa moja kwenye mada,

Tumeona kero kubwa sana kwa Wananchi wakati wa ufuatiliaji wa namba za utambulisho kwa ajili ya kupata vitambulisho cha taifa.

Foleni ndefu sana na NIDA wanasuasua sana kwenye kukamilisha zoezi hili kama walivyoplan. Huku msukumo mkubwa ukiwa kwa wananchi kupata vitambulisho vya taifa kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za Vidole (mwisho ikiwa Desemba 31, 2019).

Wapo wananchi wengi walioamua na wanasema "liwalo na liwe. Wafunge tu hizo laini tutatumia simu zetu kwa matumizi ya tochi, kusikiliza nyimbo na Radio". Kiuhalisia NIDA wameshindwa kukamilisha zoezi hili.

Na hili linathibitishwa mambo kadhaa ambayo wananchi tunayatumia kama ushahidi

1. Namba ya kutumia kupata namba ya utaambulisho (kwa kutumia simu) kutofanya kazi na kutokuwa na uwezo wa kuwapatia wananchi namba za utambulisho.

2. Website ya NIDA kutokufanya kazi

3. Foleni ndefu zisizopungua kila siku kwenye vituo vya NIDA na muda mrefu unaotumika mpaka mwananchi kupata kitambulisho.

4. Wananchi wachache kuwa wamepata vitambulisho mpaka Desemba, 2019 (tofauti na waliopata wakiwa vyuoni)

5. NIDA kuwa inatoa taratibu mpya kwa wananchi kupata namba ya utambulisho tofauti na mpango walioanza nao.

MAPENDEKEZO KWA SERIKALI

1. NIDA na NEC (Tume ya taifa ya uchaguzi) ziunganishwe kukamilisha zoezi hili; Ubora wa vitambulisho vya taifa na vya kupigia kura ni ule ule tena zaidi cha taifa kina taarifa nyingi zaidi za raia kuliko cha kupigia kura.

2. Vitambulisho vya taifa vitumike wakati wa kupiga kura; Kupata kitambulisho cha taifa sharti mojawapo uwe 18+ (kigezo pia kwa kupiga kura). Raia asajiliwe kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwa kutumia kitambulisho chake cha taifa.Hii itapuguza gharama za kutengeneza vitambulisho na muda wa wananchi kupanga foleni tena kwa ajili ya kupata kadi za kupigia kura.

3. Muda wa kusajili laini kwa alama za vidole uongezwe kuendana na ukamilishaji wa zoezi hili. Serikali iombe tathmini kutoka kwenye makampuni ya simu na NIDA kufahamu Watanzania wangapi wameshapata vitambulisho ili kufahamu ni kwa muda gani zoezi hili litakamilika. Ni vyema ofisi husika kufahamu inaweza kuhudumia watu wangapi kikamilifu kwa siku.

Wadau mnaweza kuongeza mawazo yenu kwenye mada hii.

Nawasilisha.
 
Mkurugenzi Wa nida unajitahidi kuchapa kazi lakini lakini kama usipibadilika hao watumishi wako watakuponza wewe kuna watu wanakuangusha hii ni kutokana na upole wako na kushindwa kuchukua hatua mapema.
Mfano ma RO sio wote ila kuna baadhi wanakaa na taarifa za vtambulisho muda mrefu sana bila sababu za msingi zaidi ya kufinya hela za kuajiri watu wengi zaidi wa kukagua application forms na document hii ni moja ya mambo yanayochangia wewe kuonekana una utendaji mbovu.

Makosa ya waandikishaji na uzembe,haiwezekani muandikishaji anaona form ya mtu haina sahihi au mihuri inayotakiwa yeye anaichukua na kuingiza kwenye system hivyohivyo huo ni uzembe na kuwapa mzigo usiostahili watu wanaoenda kuhakiki .

Upunguzaji wa wafanyakazi wa data center bila tathmini ya athari zinazoweza kujitokeza hii ilijitokeza mnamo mwezi August mwaka 2019 ambapo mlipunguza zaidi ya vijana 100 wanaofanya kazi data center ingawa walikua si wafanyakazi wa kudumu hiyo ilikua ni mistake kubwa mliyoifanya.

Ukosefu wa teknolojia za kisasa,vituo vingi vya data kuanzia RO level mpaka makao makuu vina shida sana ya upakiaji na uhakiki wa taarifa labda kutokana na ukosefu wa mitambo ya kisasa lakini system zenu kwenye vituo vya uandikishaji,Data center mpaka makao makuu system zinafanya kazi slow sana ni vyema mkaziboresha kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi na kufanya update ya mfumo

Mtawanyiko wa mnyororo,mnyororo wenu wa uandikishaji umekuwa na mawanda mapana
Yaani **uchukuaji form ==>ofisi ya mwenyekiti ==>ofisi ya mtendaji==> ofisi ya uhamiaji(hapa pana usumbufu pia) ==>kujaziwa taarifa kwenye mfumo** hawa wadau wote wangekuwa wanakuwa sehemu moja ingekuwa rahisi kidogo(kwa sasa baadhi ya maeneo wameanza kufanya hivyo.

Ntaendelea
 
Mkurugenzi Wa nida unajitahidi kuchapa kazi lakini nahisi kuna watu wanakuangusha hii labda ni kutokana na upole wako na kushindwa kuchukua hatua mapema.
Mfano ma RO sio wote ila kuna baadhi wanakaa na taarifa za vtambulisho muda mrefu sana bila sababu za msingi zaidi ya kufinya hela za kuajiri watu wengi zaidi wa kukagua application forms na document hii ni moja ya mambo yanayochangia wewe kuonekana una utendaji mbovu.

Makosa ya waandikishaji na uzembe,haiwezekani muandikishaji anaona form ya mtu haina sahihi au mihuri inayotakiwa yeye anaichukua na kuingiza kwenye system hivyohivyo huo ni uzembe na kuwapa mzigo usiostahili watu wanaoenda kuhakiki .

Upunguzaji wa wafanyakazi wa data center bila tathmini ya athari zinazoweza kujitokeza hii ilijitokeza mnamo mwezi August mwaka 2019 ambapo mlipunguza zaidi ya vijana 100 wanaofanya kazi data center ingawa walikua si wafanyakazi wa kudumu hiyo ilikua ni mistake kubwa mliyoifanya.

Ukosefu wa teknolojia za kisasa,vituo vingi vya data kuanzia RO level mpaka makao makuu vina shida sana ya upakiaji na uhakiki wa taarifa labda kutokana na ukosefu wa mitambo ya kisasa lakini system zenu kwenye vituo vya uandikishaji,Data center mpaka makao makuu system zinafanya kazi slow sana ni vyema mkaziboresha kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi na kufanya update ya mfumo

Mtawanyiko wa mnyororo,mnyororo wenu wa uandikishaji umekuwa na mawanda mapana
Yaani **uchukuaji form ==>ofisi ya mwenyekiti ==>ofisi ya mtendaji==> ofisi ya uhamiaji(hapa pana usumbufu pia) ==>kujaziwa taarifa kwenye mfumo** hawa wadau wote wangekuwa wanakuwa sehemu moja ingekuwa rahisi kidogo(kwa sasa baadhi ya maeneo wameanza kufanya hivyo.

Ntaendelea
Utakuwa mtu pekee kumpongeza mkurugenzi wa NIDA na tena kubainisha hapohapo jinsi NIDA wanavyofanya mchakato wa kupata kitambulisho kuwa mrefu mno. Unamwonea huruma wakati maelfu wanateseka kwa mchakato mbovu wa NIDA?
 
Upole wake ndo unasababisha watu wa chini yake wanamuangusha
 
Back
Top Bottom