Nawaonea wivu wakenya

Wapinzani hawawezi kupinga mtu anapofuata taratibu za manunuzi. Kwa hiyo unadhani Kenya asingefuata taratibu wangemchekea kwa kuwa ananunua ndege tu.

Tatizo ndugu zetu ccm akili mnatunziwa Lumumba.
 
Huwezi kutufananisha na wakenya hata siku moja Tanzania ubabaishaji mwingi kwa mambo ya kawaida (nitayaeleza baadae)

Nadhani ungeishi Kenya ungefaham vizuri zaidi..unadhani kenya walificha ficha mambo yao kwa wananchi? Waliwaficha bei halisi za ndege? Waliwaficha kama ni mtumba au mpya? Waliwaficha kwanini wamezipata kwa wakati? Waliwaficha kama wanadaiwa na nchi husika deni lililosababishwa kwa uzembe wa kiongozi? Waliwaficha wananchi wao kuhusu nini wamefanya ndege ikaachiwa, je walilipa faini ya fedha ambazo ni kodi zetu??

Usikubali kupelekeshwa na kuonwa kama mjinga flani hivi kwamba usipate taarifa sahihi bali ukae utulie kuona mambo mazuri tu
 
Hivi unaanzaje kuilinganisha Kenya na Tanzania ktk maendeleo? KENYA NI HABARI NYINGINE KABISA.

Umeanza vizuri thread yako ila umaliziaji wako umebainisha wewe ni mtu wa aina gani.

KENYA IACHE ILIVYO, ulishawahi kujiuliza ni jinsi gani inasurvive mbele ya Alshabab?

Ulishawahi kujiuliza jinsi gani inasurvive mbele ya ukabila mkubwa?

Kenya ina maadui hawa, ugaidi wa alshabab na ukabila mkubwa ambao Tanzania haina lakini wanatuzidi kimaendeleo kila kukicha.

Hatahivyo Kenya inakimbilia ubepari uliokomaa lakini Tz haieleweki inakimbilia ubepari mchanga au inarudi kwenye ujamaa kwa kuimarisha serikali na kudhoofisha sekta binafsi.
 
Kenya kila jambo linalofanyika linafanywa na serikali yawananchi wa Kenya na si serikali ya Kenyatta au ya Jubilee. Wakenya wanaheshimu sana katiba ya nchi ndivyo sababu mambo yao hayatekwi na vyama, tatizo hapa kwetu maendeleo hayaletwi na wananchi yanaletwa na CCM! Wakati kodi ni yetu sote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…