Nawaomba sana TANROAD

Dereva Suka

Senior Member
Sep 25, 2014
176
289
Naiomba hii mamlaka husika katika maswala ya barabara waweke kibao kinachoelekeza speed limit ya 50KPH katika barabara ya kuelekea Mbagala eneo la mtongani kwa mbele ambapo kuna daraja la treni.

Eneo hili lina bonde ambalo linaishia maeneo yenye mto unaoingiza maji baharini.

Bonde hili madereva wengi hasa wa daladala huwa wakitokea mtongani wanashuka na speed kubwa sana na gari ikiwa na mzigo ambao ni abiria kwa mwendo ambao sio mzuri endapo zitatokea hitilafu zozote za kiufundi.

Kuna kipindi Traffic Police walikuwa wanakaa maeneo ya kituo cha Msikitini na tochi ambayo kidogo ilisaidia kuzuia tabia hii ya kushuka bonde lile ambalo sio zuri kwa speed kubwa.

Naomba TANROAD muweke alama inayoonesha speed limit niliyotaja hapo juu kwa sababu kwa magari haya ya daladala mengi yao najua kabisa hayapo vizuri sana kwa kukimbiza speed kubwa yakiwa na abiria wamejaa mpaka wamesimama.

Ni hayo tu.
 
Hiyo sehemu ni mbaya sana!! Kibaya zaidi pale msikitini ile kona unapokuwa unapandisha. Misheni ni hatari san!! Tena kama uwe umepanda mabasi yale ya mchina una hisi kuwa mnadondoka!!!
 
Naiomba hii mamlaka husika katika maswala ya barabara waweke kibao kinachoelekeza speed limit ya 50KPH katika barabara ya kuelekea Mbagala eneo la mtongani kwa mbele ambapo kuna daraja la treni.

Eneo hili lina bonde ambalo linaishia maeneo yenye mto unaoingiza maji baharini.

Bonde hili madereva wengi hasa wa daladala huwa wakitokea mtongani wanashuka na speed kubwa sana na gari ikiwa na mzigo ambao ni abiria kwa mwendo ambao sio mzuri endapo zitatokea hitilafu zozote za kiufundi.

Kuna kipindi Traffic Police walikuwa wanakaa maeneo ya kituo cha Msikitini na tochi ambayo kidogo ilisaidia kuzuia tabia hii ya kushuka bonde lile ambalo sio zuri kwa speed kubwa.

Naomba TANROAD muweke alama inayoonesha speed limit niliyotaja hapo juu kwa sababu kwa magari haya ya daladala mengi yao najua kabisa hayapo vizuri sana kwa kukimbiza speed kubwa yakiwa na abiria wamejaa mpaka wamesimama.

Ni hayo tu.
Kibao kitasaidia kupunguza speed au una maanisha nini?kuwepo kwa askari hapo nahali nafikiri ndio njia bora.
 
Back
Top Bottom