Navumilia mateso ya moyo kwaajili ya mtoto wangu

Kweli we kilaza,,karud anaishi na jini au wewe?kurud yeye sio ishu ishu ni wewe kukubali yeye arud ndio ukilaza wako ulipo,,subir sindano zikuingie ili siku nyingine demu akikuambia naondoka,pigana kiume asiondoke ila akilazimsha mwache aende na akirud usimkubalie kwa machoz hata ya damu usimkubalie asilan,, soma uelewe
Mwenye wewe unavimba na kujiona una punch za maana... Sawa Godzila kafanya nn tena leo? Naona ndo kitu naweza kupata kutoka kwako....
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Baada ya pilika zangu za kutafuta mkate wa kila siku nakutana na rafiki yangu wa kike baada ya kunipigia tuonane.

Nakutana nae na moja kati ya ombi lake ni NDOA anahitaji nimuoe maana amechoka mateso na kusimangwa kutoka kwa mama yake.

Baada ya kama wiki mbili nikaridhia ombi lake baada ya kujifikilia sana, niliwaza mengi sana hasa hasa ilikuwa ni umri wangu kusogea na sina hata mtoto mmoja wa kusingiziwa hivyo nikamtuma mshenga kupeleka posa na taratibu za nyingine.

26/12/2014 nikafunga ndoa na binti, maisha yakaendelea na inshort yalikuwa mazuri namshukuru Mungu, baada ya mwaka mmoja tukabahatika kupata mtoto mmoja wa kike.

Baada ya miezi mitatu tangu huyu binti ajifungue nikapata kesi moja mbaya sana na kunusurika kwenda jela lakini nilipoteza vitu vingi katika hiyo kesi ikiwemo connection zangu zote za kuingiza mtonyo.

Binti akadai talaka baada ya mazingira kubadilika na mtonyo kupiga chenga katika meza, silaha yangu kujitetea ilikuwa ni mtoto kwamba siwezi kukumpa talaka wakati mtoto wetu ni mdogo sana asubili mtoto akue then ataenda. Binti kaja juu kajaza watu mtaani hawezi kuishi na mimi tena anataka talaka yake aende aanze maisha yake.. Pamoja na watu kumsihi ikashindikana ikabidi nitoe talaka akaenda zake yeye na mtoto "Tena usijaribu kunipigia simu, mtoto wangu ntalea mwenyewe "

Kauli yake ya mwisho kabla hajaondoka kwangu, pamoja na kumsihi asiongee maneno mengi sana abakishe akiba ya baadae maana mtoto anahitaji malezi yangu pia kama baba.

Baada ya wiki nikapokea barua ya wito nahitajika serikali ya mtaa, binti anataka Asset tulizochuma hasa hasa vitu vya ndani (Furniture). Shauri likaisha Baada ya mimi kukubali kumpa kila kitu na mjadala ukafungwa.

Nikajichanganya na maisha ya kuishi gesti baada ya mwezi nikapanga chumba na maisha yakaendelea.

Baada ya miezi tisa binti karudi na mtoto akiwa katika hali mbaya sana, hakuwa amejipanga na maisha wazazi wake hawakumpa support Ananiheshimu sana kwa sasa na sikuona jinsi ya kumwambia aende na ikiwa mtoto bado hajaacha kunyonya.

Naishi nae nikiwa na chuki sana katika moyo but najitahidi nisimuoneshe wakati mwingine nashindwa kujicontrol. Nahitaji mtoto wangu akue vyema na apate malezi yangu.

NI VIPI NITAWEZA KUTOA CHUKI NILIYONAYO DHIDI YA HUYU BINTI ILI LENGO LA KULEA MTOTO WANGU LITIMIE?
Hiyo kesi moja mbaya ya kunusurika kwenda jela ni ipi mkuu..sijakuelewa
 
Nimekuelewa... Nilichokushauri ni kuondoa hiyo chuki uliyonayo moyoni ili maisha yarejee kama mwanzo... SAMEHE na SAHAU. Tumeshasuluhisha ndoa nyingi zenye matatizo makubwa kuliko iyo yako na wanandoa hao sasa wanakaa pamoja kwa amani... You are not an exception... Iwapo kwa hiyo miezi tisa hukuweza kuoa tena, its clear kuwa bado ulikuwa unamuhitaji mwenzako... Sasa kwa kuwa amesharudi, it means you got what you wanted... Au sio?
Mhm jamani moyo wa kusamehe...... naombeni mnifundishe pia niweze kuondokana na kinyongo
 
Sijaeleza vitu vingi kwakufupisha story.. Kwa sasa hakitoka kwangu hana mahali pa kuishi alishafukuzwa na mzazi wake nyumbani
Vumilia tu aisee....aah life is complicated anyway....maana hapo kuna issue ya mtoto mchanga na binti hana kazi...no way.....omba Mungu akupe wepesi moyoni ili usiumie zaidi
 
Mtoto ana Mwaka 1 na miezi 5 wakati nahitaji afike atleast miaka 3 hivi then naweza kumwambia atoke akafanye mambo yake... Najisikia vibaya sana mtoto wangu kuishi maisha yakukaa mgongoni kuzururishwa ovyo ovyo... Huyu mwanamke amepoteza tumaini mpaka la kuishi, Ntawezaje kuondoa chuki niliyonayo dhidi yake kwa kipindi hiki ili anilelee huyu mtoto wakati nasubiri kutimka na mtoto wangu, sina lengo la kumrudia huyu..
Hilo ndio la msingi...lea mtoto akikua kidogo move on....otherwise Aaaah utapasuka moyo tu bure...
 
Maamuzi yangu ninayo ndio, nimeuliza ntaweza vipi kucontrol hali ya kuwa na chuki nae ili anilelee mtoto wangu, kumbuka anaishi kwangu kwaajili ya malezi ya Mtoto, mtoto akikua kidogo anasepa huyu... Nafikili watu wengi hawajanielewa sijui kwa sababu nimeandika kwa jazba
Mi nimekuelewa sana,sema watu wengi wanaona kuwa ni ngumu kuishi na mtu pamoja bila kurudisha mahusiano ya kimapenzi...

Shikilia msimamo wako kama kweli umeamua toka moyoni....ishi nae kwa ajili ya kulea mtoto tu mpaka umri fulani,but ishi kwa tahadhari maana moyo ni kiza kinene
 
Malezi ya mtoto yanahitaji ushirikiano wa karibu wa wazazi wake. Akimfukuza huyo mwanamke atakuwa amefanya hivyo kujipa amani yake huku akimnyima furaha mtoto ya kuishi pamoja na wazazi wake. Ni bora yeye akabeba mzigo huo aumie moyoni lakini mtoto afurahie uwepo wa wazazi wake kwa sababu migogoro yao haimuhusu mtoto. Kama ni kosa limeshafanyika na jamaa anaweza kuvumilia na kusamehe kwa faida ya mtoto au akahakikisha wanakuwa na ukaribu tu kwa ajili ya mtoto huku kila mmoja akifanya mambo yake ingawa uamuzi huo pia utamuathiri mtoto kisaikorojia. Kama anaweza lusamehe basi asamehe maana huenda mwanamke huyo akawa amejifunza. Jambo la msingi ni kwamba jamaa ameshajua hulka ya huyo mwanamke hivyo anaweza kubadili namna ya kuishi naye.
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom