Nauza mti wa Mvule

Nauza mti wa Mvule

Huo mti si wako kabisa halafu kama utaamua uuchane ww, gharama utakazoingia zitakuwa kubwa kuliko utakachopata. Wewe chukua 300+ fanya yako. Pia ikitokea Kijiji wana mradi wao, wanaweza kujenga hoja wautumie huo mti na huwezi kuuzuia. SIWA WAKO. Hiyo nchi sheria zake mbovu za kuwabana raia wake ndio chanzo cha umaskini wake.
Hapana ni wake kabisa, ila ili kuwa salama na kupata haki yake stahiki atafute Kibali cha kuuvuna. Anzia na ofisi ya kijiji / mtaa, maana hao ndio wanaujua mti na wewe wanakujua. Watakuandikia barua kupeleka ofisi ya maliasili halmashauri. Hao maliasili watakuelekeza zaidi ikiwa pamoja na malipo unayopaswa kulipa.
 
Nimekupata mkuu wangu. Wacha nichacharike kuupiga bei fasta
Utapata hasara, Mvule ni mti wa mbao ngumu na nzuri sana. Bei yake ni nzuri sana pia. Uchane wewe mwenyewe.
Angalizo: kama uko kwenye chanzo cha maji, au kwenye mteremko hautaruhusiwa kuuvuna. Kwa sababu utakuwa unahifadhi chanzo au utakuwa unazuia mmomonyoko wa udongo.
 
Hapana mti haupo kwenye chanzo cha maji wala mtemko ni eneo tambarare.

Sasa kuchana mbao si gharama tena mkuu? Na uuzaji wa mbao zenyewe kuanza kuzunguka mjini kutafuta wanunuzi?
Gharama ya kuchana haitakuwa kubwa kuzidi mauzo. Wateja ni hao wenye karakana za seremala. Patana nao kabisa. Ukiwa na vibali haraka sana watachukua. Mbao za Mvule ni nzuri sana, "hazigongwi" na wadudu. Jaribu kuulizia mlango wa Mvule usikie bei yake.
 
Fuata kwa tahadhari ushauri wa hawa watu. Ukibisha endelea. Wewe sio mfanyabiashara wa mbao na itakuwa too cost kukata vibali kwa mti mmoja tu. Hao wafanyabiashara wakikuta umeshachana watatoa kasoro mia kidogo;kwani watakuwa wanajua huna ujanja huku ushaingia gharama kibao. Watakwambia mvule maji, mvule mvua mvule matope nk nk.
 
Hapana mti haupo kwenye chanzo cha maji wala mtemko ni eneo tambarare.

Sasa kuchana mbao si gharama tena mkuu? Na uuzaji wa mbao zenyewe kuanza kuzunguka mjini kutafuta wanunuzi?
Mkuu huo mti ukiwa hapo shambani utaathiri shughuli zako zozote au unakukera ukiwa hapo? Kama hauathiri basi uache ukae hapo sababu hiyo thamani uliyonayo kama unatunza mazingira. Tujaribu kutunza mazingira na vyanzo vyake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom