.
KakaKiiza;
Kwa uzoefu mdogo nilionao, mara nyingi vinavyodumu huwa havinunuliwi mara kwa mara (mzunguko mdogo).
Kwa uzoefu wa miaka sita sasa nimetumia CRESTA GX100; 1997 Model kama hiyo inayouzwa. Sijawahi kupata tatizo kubwa la kiufundi zaidi ya service, kubadili tyres, bulbs (taa) za mbele na moja ya nyuma. hiyo gari nimeiuza mwezi March 2012 kwa shs 6.8m. Aliyenunua yupo hapa hapa mjini DSM na anaitumia vizuri tuuuu.
Kusema kuwa nayo ni kufunga nayo ndoa ya maisha nadhani unaweza kuwa sawa kwa kuwa huna haja ya kuiuza wakati haikusumbui.
Ni gari yenye nguvu,
Inahimili mikiki kuliko gari zingine za aina hiyo,
"Engine" yake haitetereshwi na vitu vidogovidogo kama mafuta yaliyo chakachuliwa, etc,
Ukitaka kusafiri nayo ndio utafurahia zaidi - kwa wanao yatumia watakubaliana na mimi --hili dude barabarani linatulia.
Sifa zaidi zipo nadhani ukitafuta utafahamu.
Wanaopenda kununua gari la aina hii wasisite. Hili hapa jamvini sifahamu hali yake, sifa nilizotoa ni za ujumla wa Toyota Cresta GX100 ya mwaka 1997.
Asanteee