Mkuu nakuhakikishia Hautapata Mteja wa kununua ilo eneo kwa pesa iyo trust me ata Dalali akija ata kwambia.
Apo chamazi kuna Jamaa alijenga nyumba ikamshinda na n bonge la nyumba haswa alianza M70 kuuza imekaa miaka 15 mpaka sasa ameshusha mpaka 25M bado ajapata mteja.
Ebu vuta picha kama maeneo ayo watu wananunua nyumba 20M,15M mpaka 10M na Ni nyumba ya vyumba vitatu sitting, dinning, kitchen na stoo be serious utapata mteja ila acha kuwa na Tamaa za kupata pesa nyingi uku mazingira ya eneo, na ukubwa havirizishi
Maeneo ya Mbagala watu wanaokaa ukanda uo wana pesa za kudunduliza na unajua ni watu wa Kusini kwa 95% sasa M45 akija dalali ata kwambia zangu 5 so atatafuta mteja wauze eneo kwa M50 je mteja atapatikana ?
Ukisema ushushe ilo eneo watakwambia uliuze M20-25 dalali anaweza jitahidi mpata mteja japo pia nikwa mbinde sana so jaribu kutafuta madalali pia kwa ilo