OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,075
- 114,594
Wabunge wetu hakika hawajielewi, nadhani kujua kwao kusoma na kuandika ndio matokeo ya yote haya. Katika mazingira ambayo serikali imefeli sana katika utekelezaji wa bajeti iliyopita unapata wapi ujasiri wa kuinuka na kushangilia kuwasilishwa kwa bajeti?
Uwasilishaji wa bajeti kama huu ulishangiliwa sana katika bunge la bajeti lililopita. Yalitajwa mengi sana mengine ''hewa'' lakini yakashangiliwa. Sasa mwaka wa fedha unaisha June mwaka huu huku
Uwasilishaji wa bajeti kama huu ulishangiliwa sana katika bunge la bajeti lililopita. Yalitajwa mengi sana mengine ''hewa'' lakini yakashangiliwa. Sasa mwaka wa fedha unaisha June mwaka huu huku
- Bajeti katika sekta muhimu kama kilimo na viwanda imetekelezwa chini ya asilimia 18%, lakini bado watu wanashangilia. Na sio kuishangaa serikali na kuiwajibisha kutoa majibu ya haja kivipi imeshindwa kutekeleza na inataka iaminiwe inaweza kutekeleza
- Bajeti iliyopita serikali ilitenga bilioni 59 kwa ajili ya kugawa milioni 50 kila kijiji. Zilitekelezwa?Ajabu katika hotuba ya Dr.Mipango sio tu halijazungumziwa utekelezaji bali hata katika bajeti ijayo serikali ipo kimya. Mabashite hawa wa CCM wanashangilia ujuha.
- VAT katika huduma za miamala ilivyoadhiri wananchi wa kawaida. Katika bajeti iliyopita serikali ilijikanganya sana katika kukusanya VAT kwenye miamala ya fedha. Inalipwa na kampuni au mtumiaji?Lakini mwisho wa siku ikalipwa na mtumiaji. Wabunge wetu wanashangilia
- Ruzuku katika Halmashauri za Wilaya na Sekretariati za Mikoa ni duni. Wabunge hawa wanafahamu kabisa jinsi halmashauri zao zilivyopigika katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma. Hata fedha za kufanyia service za magari na mitambo hawana
- Usanii wa punguzo la PAYE. Serikali ilisema katika bajeti iliyopita itapunguza PAYE kutoka 11% mpaka 9% matokeo yake wakapunguza shs.2,000 tu. Wabunge wanashangilia
- Serikali ilitenga 2.4b kwa ajili ya kujenga miundombinu ya makazi kwa ajili ya wazee na mahabusu za watoto. Wapi wamejenga?
- Ruzuku kwa wachimbaji wadogo wadogo. Katika hotuba ya Dr.Mpango bajeti iliyopita aya 64 alisema serikali itawapa ruzuku wachimbaji. Mchimbaji aliyepewa ruzuku anyooshe mkono. Mbunge yeye anashangilia tu
- Polisi wetu kutokana na uduni wa makazi na ofisi zao waliahidiwa kujengewa makazi na ofisi. Mpango akawasilisha kwa mikwara aya ya 65 ya hotuba. Lakini wapiii, polisi wanaishi makazi duni na ofisi zao zimechoka licha ya kutokupelekewa hata fedha za kuendesha ofisi tu. Kama mnabisha mwiteni Mwigulu hapa aseme Mkuu wa Kituo cha Polisi Iramba mara ya mwisho alipelelekewa fedha za mafuta lini.