Nauliza tiba ya Moyo figo na mkono wa kulia kukakamaa na kuuma sana nisaidieni

Wavizangila

Member
Jun 3, 2011
33
2
Wakuu heshima mbele. Mzazi wangu ana umri wa miaka 70, hivi karibuni kafanyiwa uchunguzi wa afya yake kwa kupigwa x-ray na kukutwa na tatizo kwenye moyo na mapafu baada ya kutumia dawa kwa muda wa miezi miwili mfululizo akaanza kuumwa figo na mkono wa kulia joint za viganja zinauma sana na hazikunji zinakakamaa na moyo unauma kama kidonda naomba msaada jamani
 
Dawa ya Ugonjwa wa Moyo. unaweza kabisa ugonjwa wa moyo na kuzuia makusanyiko wa mtando wa mafuta kwenye mishipa ya damu, kwa kula asali na mdalasini yaani asali vijiko vitano na unga wa mdalasini vijiko vitatu kwa kijiko kidogo cha chakula kutwa mara tatu miezi miwili. na kijiko kidogo cha chai unaweza kupaka kifuani na sehemu nyingine wakati Asubuhi na usiku kila siku Inshaallah utapona.

Dawa ya Figo Achukue ndevu za mahinda mabichi achemshe kisha achuje maji yake yakishapowa anywe ujazo wa kikombe cha kahawa mara tatu kwa siku kwa muda wa mwezi moja kwa Uwezo Wa Allah Atapona

Dawa ya Kukakamaa vidole Upate karafuu gram 50,pilipli mtama gramu 50, Tangawizi kavu gramu 50, Bizari nyembamba gramu50,Habbati soda gramu50,na Haltiti ya unga gramu10 utwange hizo dawa Uchekeche kisha uchanganye na mafuta ya zaituni au Mafuta ya Ufuta kiasi cha kuweza kuwa kama uji uwe unamchuwa chuwa Mzazi wako asubuhi,Mchana na usiku kwa muda wa siku 21 hayo matatizo ya kukamaa

Na hizi dawa Zingine za kula Upate karafuu gram 50,pilipli mtama gramu 50, Tangawizi kavu gramu 50, Bizari nyembamba gramu50,Habbati soda gramu50,na Haltiti ya unga gramu10 utwange hizo dawa Uchekeche kisha uchanganye na Asali Safi mbichi ya nyuki Asali yenyewe iwe kipimo cha chupa ya fanya. Matumizi Kula kwa kijiko kikubwa cha kulia wali awe anakunywa hiyo Dawa kuta mara 3 kabla ya kula kitu awe anakula hiyo Dawa asubuhi,Mchana na usiku. Atumie hiyo Dawa ya kula kwa muda wa siku 21 inshallah Mzazi wako Kwa Uwezo wa Mwenyeezi Mungu atapona tumia kisha unipe feedBack.
 
Back
Top Bottom