Nauliza Nimfanyeje huyu mwanamke ili aweze kanirudishia pesa zangu?

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,508
99,297
Wakuu,
Tangu xmass sijafungua kabisa Duka langu, niliamua kujipa mapumziko ya hiari mpaka sikukuu zote za xmass na mwaka mpya zipite ndo ntaendelea na biashara.

Siku ya Jana tulikua na miadi ya mtoko mida ya jioni na mpenz wangu maana xmass na boxing day zote hatukutoka tulikua kwny ugomvi mkubwa Sana.

Sasa kwasababu balance yangu ilkua ndogo na ATM kadi iko dukani, ikanibidi niende dukani kufata cash ili tukatoke out na mpenz wangu tukafurahi.

Nikiwa njian naelekea dukani Kuna mteja kanipigia anaulizia mzigo flani, nikamjibu upo. Akasema anamtuma kijana aje kuchukua, nikamwambia Kuna mahali naenda,sitoweza kumsubir uyo kijana wake Hadi afike, Kama inawezekana anielekeze alipo nimpitishie Moja kwa Moja niende zangu,. Kweli kanielekeza, na nmepaelewa.
 
Nmefk dukani, nikabeba cash 150,000 pamoja na mzigo wa yule mteja. Nmempelekea mteja mzigo mpaka kwake na kanilipa cash 325,000 nikatia mfukoni nikaelekea kwa mamaJ na kumkuta sebleni anakunywa bia, nikamsisitiza akajiandae tuondoke MDA sio rafiki Sana. Kasema sawa na kuelekea chumbani kwake.

Sasa mamaJ akiwa chumbani kwake anaoga anajiandaa tutoke,nami Niko sebleni, nikawaza sio vzur kwenda maeneo ya starehe za ulevi na hela zote hizi, likanijia wazo la kuziacha baadhi mule mule ndani kwa mamaJ, Basi nikachukua zile 325,000 alizonipa mteja nikazificha juu ya vent ya mlango wa sebleni bila mamaJ kujua.

Mamaj Alipomaliza kujiandaa, katoka na kufunga milango kisha tukaenda zetu kiwanja kuenjoy na washakaji. Uko kiwanja mamaJ, round ya tatu tu tayar mwenzangu keshaanza fujo zake, jamaa zangu wakauliza vipi,mbona mapema mno? Nikawaeleza kua alikuja tayar keshakunywa uko nyumbani, nahs ndo maana.
 
Sasa nmetoka nmeenda toilet,narud nakuta keshaanza kumix bia na bapa, nikaona uyu pombe zishampanda kichwani, na hili bapa analomix kwenye bia achelewi kunitia aibu mbele za jamaa zangu. Nikachukua maamuz ya kumwondoa pale nimpeleke nyumbani.

Tumefika nyumbani nmemlaza kitandani, akawa anataka tufanye mapenz, nimwambia subir nikafunge geti vzuri. Baadaya kufunga geti narud wazo likanijia niangalie balance yangu mfukoni, nikajikuta nmebakiwa na 112,000, Kisha nikaangalia kwenye vent ya mlango Kama pesa nilizoacha bado zipo, nikajiridhisha kweli bado zipo.

Basi naijua vema tabia ya mamaJ kunisachi mifukoni akishajuaga nimelewa pombe, kwenye ile 112,000 nilotoka nayo kiwanja, nikabakiza elfu 2 tu mfukoni, afu Nikachukua 110,000 na kuiunganisha na zile 325,000,ikawa jumla 435,000 Kisha zote nikazipachika juu ya vent ya mlango na kuelekea zangu chumbani tukafanye ya kufanya.
 
Kule chumbani tumefanya ya kufanya, tulipochoka wote tukapitiwa kijiusingizi flani Cha uchovu mzito. Nmekuja kuzinduka usngzin,naangalia saa Ni saa 7:15 usiku, nmeoga chap chap nmevaa na mbio mbio nmeondoka zangu pale kuelekea kwangu.

Njiani nikakumbuka kwamba kule mamaJ nmesahau zile pesa zangu juu ya vent ya mlango, Basi nikajipa moyo hawezi kuziona ntaenda kuzichukua ata kesho yake jioni.

Asbh Kulipokucha natakiwa kwenda zangu dukani, nikakumbuka funguo za dukani nazo kumbe nizilisahau kwa mamaJ, hivyo ikanilazimu asbh hiyo hiyo breki ya kwanza niende kwa mamaJ.

Nmefika kwa mamaJ,namkuta ndani hayupo, ila mapazia yote madirishani na milangoni yametolewa na kulundikwa pamoja na nguo chafu kwenye beseni nje kibarazani.
 
Kuona vile kichwa kikapata Moto,
breki ya kwanza kwenye vent kuangalia Kama pesa zangu zipo, nikakuta hazipo, nmetafuta Sana pesa zangu sizioni. Ghafla naendelea kutafuta nae mamaJ anaingia kashikilia nyama,mche wa sabuni pamoja na sabuni ya unga.

Akanishangaa, nikamwambia natafta pesa zangu niliziacha juu ya vent ya mlango pamoja na funguo za dukani. Akasema funguo ziko Kwny dressing table ila khs pesa yeye hajui Chochote na hajaziona.

Nikamuuliza "ujaziona kivipi wkt Jana tulikua wawili TU humu ndani na Wewe ndo umetoa mapazia na kufanya usafi juu ya hizi vent, Unanambiaje ujaziona Ela zangu" akakataa kata kata hajaziona.

Sasa kwa jins anavozid kukana kwa Nguvu ikawa Kama anazd nipandisha hasira, nikaona nichukue funguo niondoke zangu dukani, maana nisije jikuta nmepasua mtu vibao.

Hapa nmekaa dukani ila akili yangu haiko sawa kabisa, Najiuliza uyu mwanamke kaamua kunitapeli pesa zangu au Ni kwamba anajizima data.

Hapa nawaza sijui nimfanyeje hata sipati jibu sahii

Naombeni ushauri wenu wakuu,
Mnamuelewaje uyu mwanamke, Maana kama sio dhulma Basi huu kiuhalisia Ni wizi kabisa.

NIMFANYEJE HUYU ILI AWEZE KUNIRUDISHIA PESA ZANGU.

Nawasilisha
 
Kuwa na mwanamke mlevi anayekusachi tu tayari ushabugi, kabla ya kuibiwa hela.

Hicho kitendo cha kuibiwa hela kilikuwa lazima kitokee kama si leo kesho.

Sasa mkuu, kusoma hujui, hata picha huoni?

Au ndiyo ushalishwa vya kulishwa?
 
Ila kwa hapo kitu chochote kilicho ndani ya nyumba yake ambacho umiliki wake hauwezi kuwa na maswali ni mali yake halali isipokuwa tu vile ulivyomkabidhi.

Hivyo uache kumtafutia matatizo maana unataka umtapeli hela zake hizo 425,0000 ambazo huwa anazihifadhi muda mrefu tu hapo mlangoni.
Ni zake hizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom