Ustaadh
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 413
- 20
Huwa nakerwa na kundi dogo katika jamii kutaka waitwe "waheshimiwa". Watu hawa hudiriki hata kujitambulisha "Mimi naitwa Mheshimiwa Blah Blah". Hivi ni nani si mheshimiwa? Wana uheshimiwa upi huku wanaendekeza wizi, ubadhirifu na ufisadi? Wana uheshimiwa upi wakati wao hawajiheshimu? Kama wangekuwa wanajiheshimu na kustahili "uheshimiwa" si tungeuona huo uadilifu wao? Tutawaheshimu vipi wakati wao hawatuheshimu? Kwa nini tuwaite waheshimiwa wakati hawana hata chembe ya heshima? Nauliza - kwa nini tusiwaite Bwana blah blah, Bibi blah blah - au uheshimiwa umekuwa cheo?