Nauliza: Kubana matumizi kwa serikali ya Pombe Magufuli kuna faida Kwa Watanzania?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,441
Salaam wana JF
Mada tajwa yahusika
Wakati serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na rais Magufuli ilipoingia madarakani iliingia na Sera ya kubana matumizi
Akaanza Kwa kuondoa watumishi hewa
Akaja kutumbua wenye vyeti feki
Akafuta safari zote za nje ya nchi
Akazuia ajira zote
TRA wakatutangazia kwa mbwembwe makusanyo ya kodi tukajua mambo yatakua mazuri
Cha ajabu pamoja na hii Sera ya kubana matumizi kutumika lakini hali kitaa imekua mbaya zaidi
Maisha ya Watanzania wengi yamekua magumu zaidi,bidhaa zimepanda bei
Ajira hajatoa za kutosha na katimua wenye vyeti feki lakini bado mtaani hela ni ngumu
Mimi nafanya kazi private sector lakini malipo ni shida kutokana na ofisi kukosa fedha
Sasa najiuliza hii Sera ya kubana matumizi imemnufaisha vipi mtanzania wa kawaida hadi sasa
Kitaa hali mbaya ,wale Kula kunya kulala bure hawawezi jua hali ngumu tunayokumbana nayo sie tunaojitegemea
Nlijua hii kubana matumizi pesa itakua nyingi mtaani lakini ni vice versa hela hakuna
TRA vipi Siku hizi mnatangaza yale makusanyo yenu
Sielewi elewi hii Sera ya kubana matumizi faida yake ni ipi hadi sasa Kwa mtanzania kama Mimi.TUAMBIANE
 
Parsimonious is not a function of economic policy, it rather an enemy of development and welfare.

Haven't you heard that jealous people never win?
 
Lengo anabana matumizi ili hela inayoptikana aipeleke kwenye shughuli za maendeleo. Vinginevyo maendeleo anayoyataja taja kwenye majukwaa hawezi kuyatekeleza kwa style ya ufisadi kama awamu iliyopita. Vuta subira utazoea tu hiyo hali inayokukabili ni ya muda mfupi.
 
Subira yavuta kheri Mkuu..lakini wakati huo huo Haki huinua taifa...
 
Ndio, zimepatikana faida nyingi kwa watanzania baada ya Rais Magufuli kubana matumizi. Baadhi ya faida ni kupunguza kodi ya 2% kwa watumishi wa umma, kununua ndege zimezopelekea usafiri huo kuwa wa uhakika kuliko awali, amefanya watu tuheshimiane mtaani adi maofini, ameongeza uwajibilaji kwa watumishi wa umma na hivyo kupelekea wananchi kupata unafuu na urahisi katika kupatiwa huduma za kijamii kama vile afya, maji n.k.
 
Ubinafsi wa kiongozi ni hatari sana kws maendeleo y a Taifa changa kama Tanzania, tatizo la pombe ni kujisafisha jukwaani lakini kiukweli matendo yake ni sawa na gugu liliota katika ngano, matarajio ya mtanzania yeyote ni kuona kwamba anapata serikali inayogusa maisha ya mtanzania wa kawaida na si vinginevyo!
 
Shida yenu ni kubwa. Elimu. Elimu elimu na kuelimika. JPM unampimaje kwa mwaka na Robo tatu. Unapoingia madarakani. Unakuta Mengi. Kama huwezi kuanzia kufikiria kama familia huwezi kujua ugumu wa madaraka. Watz. Ndo sisi wote tunajijua tunavyopenda vya njia ya mkato. Sisi ndo tunakwamisha. Uvivu maneno Mengi. Siasa Tu. Wapiga domo sana. Wanaopandisha bidhaa ni sisi. Lakini mwisho wa siku tunataka JPM atusaidie mpaka style za Ndani. he is but a Human Being not GOD. TZ ni maskini sana. 50,mill people ni wengi sana.
 
Serikali ya Magufuli haijabana matumizi.

Watu wote wanaotumbuliwa kwa style ya "kupangiwa kazi nyingine" hawafanyi kazi lakini wanalipwa mishahara.
 
Ndugu, is too early to discuss that issue now, kwani Rais wetu mpendwa Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza alipolihutubia Taifa kupitia Bunge aliongea yafuatayo akituuliza sisi Watanzania kupitia Bunge, nanukuu "mnataka tuanze na kulia halafu tucheke au tuanze kucheka halafu tulie"? mwisho wa kunukuu, maana kubwa ya msamiati ule ni kwamba ili kuyafikia maendeleo (mafanikio) na hasa katika sehemu yenye matatizo lukuki kama UFISADI, VYETI FAKE, WAFANYAKAZI HEWA, WANAFUNZI HEWA, WIZI WA MADINI, WIZI WA MALI ZA MISITU NA WANYAMA PORI, WAPIGA DILI Nk. ambayo ni mambo yanayo weza kuangamiza Taifa lolote kiuchumi na ili tuondoke kutoka hapa ni lazima vipa umbele vyetu viwe ni kupambana na mambo ambayo Mh. Rais anapambana nayo hivi sasa. Hayo makundi hapo juu ndio yalikuwa yameikamata Nchi kiuchumi hivyo kupambana nayo sio rahisi ni lazima kutokee msuguano (reaction). ndio maana ya tuanze kulia au kucheka. Watanzania tumuunge mkono Rais wetu katika kupambana na Wabinafsi, Wachumia Tumbo, Wababaishaji nk.
Mimi naamini kwa haya yanayotendeka Iko siku kilio kitaisha na kutatawala kicheko kisicho kikomo, hata kama sio kwetu sisi lakini kwa watoto, wajukuu, vitukuu, vilembwe, vining'ina nk.
Kumbuka usemi usemao "ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA"
 
Magufuli anafanya maigizo tu.

Unaelewa hilo?
 
Back
Top Bottom