Nauli za kwenda mikoani zapandishwa kinyemela.

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za mabasi wamepandisha nauli za mabasi kinyemela, licha ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kuwapiga marukufu. abiria mbalimabali wamekuwa wakitozwa kiwango cha juu tofauti na kile kilichowekwa na SUMATRA na kusababisha usumbufu kwa abiria. Uchunguzi ulifanywa na kugundua kuwa nauli kutoka Dar kwenda Mwanza imefikia kiasi cha sh 50,000/= badala ya sh 40,000/=, kwenda Iringa imepanda hadi sh 25,000/= badala ya sh 18,000/=, kwenda Masasi imefikia sh 25,000/= badala ya sh 22,000/=, Tunduma nauli kwa sasa ni sh 40,000/= badala ya sh 35,000/=. Imeelezwa kuwa wafanyakazi wa kampuni mbalimbali za mabasi wanakuwa na vitabu viwili vya kakatisha tiketi, abiria AKILALAMIKA KUWA NAULI KUBWA HUBADILISHA KITABU NA KUMKATIA TIKETI NYINGINE KWA BEI HALISI (ukiwabana wanakutoza nauli halisi) ila kama hujui viwango vya nauli hizi utatoa kiasi wanachotaka wao. Kwahiyo kuweni macho wadau mnaotumia usafiri huu muhimu wa mabasi yaendayo mikoani, hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka. NAKUTAKIENI SIKUKUU NJEMA "X-MAS NA MWAKA MPYA".
 
Nadhani usiwe na hoja ya jumla. Labda uwe specific na basi fulani. Mimi nimekata tiketi leo ya kwenda mwanza kwa bei ya Tshs 40,000/-. Kwa hiyo inawezekana unayosema ni kweli lakini kwa baadhi ya mabasi na siyo yote!
 
Back
Top Bottom