Nauli mpya za Ndege za ATCL, ni ofa lakini zitadumu muda gani?

1475829765443.png
panda fast jet kama vio
 
Baada ya Rais John Pombe Magufuli kuzindua ndege mbili mpya zitakazotumiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) mwezi uliopita, shirika hilo limeatangaza rasmi maeneo ya safari za ndege hizo ikiwa na pamoja na nauli.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa shirika hilo waliandika kuwa nauli ya safari ya ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ni shilingi laki moja na sitini (160,000/=).

ATCL wameeleza kuwa nauli za safari kwenye mikoa mingine bado hazijapangwa ila wapo kwenye mchakato.

Baada ya kumalizika kwa ofa iliyokuwa imetangwa na ATCL, Nauli halisi zitakuwa kama ifuatavyo;-
  • Dar es Salaam – Mwanza kwenda ni shilingi 160,000 hivyo kwenda na kurudi ni shilingi 320,000.
  • Dar es Salaam – Kigoma kwenda ni shilingi 395,000 hivyo kwenda na kurudi ni shilingi 610,000
  • Dar es Salaam – Arusha kwenda ni shilingi 160,000 hivyo kwenda na kurudi 320,000
  • Dar es Salaam – Mtwara kwenda ni shilingi 226,000 hivyo kwenda na kurudi 452,000
  • Arusha – Zanzibar kwenda ni shilingi 249,000
  • Zanzibar – Dar es Salaam ni shilingi 123, 000
  • Dar es Salaam – Hahaya (Comoros) kwenda ni USD 253

Nauli zote hizi zitaanza kutumia Oktoba 20, 2016.

Hawajani shawishi bado mwee yaani nisafiri hapahapa Tanzania kwenda na kurudi laki sita ? Wakati nina uwezo wa kwenda kwetu na kurudi kwa sh 80, 000 nikatoa vijizawadi na hela ya matumizi ya hapo nyumbani laki mbili hapo nimebakiwa na laki tatu na ushehe niko zangu bongo kiuswazi uswazi hiyo bakshishi nakula mie na familia milo yetu ya uswazi miezi miwili msinipe stress.
 
Very strange.

Kama one way ticket ni 160,000 kwa nini return tciket isiwe chini ya 320,000?

Kwa nini wana encourage watu kukata one way ticket? Hawajui wanaongeza gharama za uendeshaji?

Mtu anayekata return ticket lazima awe na punguzo. Nadra kukuta reurn ticket inakuwa double ya one way ticket.
 
Dar to mtwara 226000
Wakat dar to mwanza ni 160000
HIV wapi ni mbali
wanaangaliaaa accessibility ya abiria inawezekana dar -mwanza kuna uwezekano wa kupata abiria wengi zaidi kwa kila trip kuliko dar-mtwara kwa kila trip
 
kama mtu unaona nauli kubwa unaacha unapanda yenye nauli ndogo. kama huipendi tu ndege unaacha unapanda unayopenda. simple usilazimishe chaguo lako ndio liwe la wote. tunatofautiana kiuchumi na kiakili pia katika kupenda na kuchagua vitu.
 
Daah wkt Ethiopia airline wametangaza nauli ya kutoka Dar to Dubai return ticket kwa usd 340 kama 684,000 hivi za kibongo, kumbe bongo hapa hapa kutoka Dar to kigoma tu ni 610,000.
Washamba wa safari za ndege utawajua tu. Wao wanafikiri gharama za kusafiri na ndege ziko kama za mabasi i.e. Sehemu ya karibu ni lazima itozwe nauli ndogo na sehemu ya mbali ni lazima ilpiwe nauli kubwa. Gharama za usafiri wa ndege zinakuwa determined na factors nyingi sio umbali....
 
Hahah asee we mjanja panda ya kwenda KIGOMA mi naenda zangu DUBAI asee, usisahau kuja na MIGEBUKA na MAWESE kutoka Kigoma ili niendelee kukuona mjanja wa town. LEKA DUTIGITE kigomaaaa awe kigoma weeee hahah eti mjanja wa KIGOMA.....
 
na bado hii nchi inamaajabu chungu nzima na likitoka hili la mapanga shaaa! tutarajie kituko kingine.
 
Baada ya Rais John Pombe Magufuli kuzindua ndege mbili mpya zitakazotumiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) mwezi uliopita, shirika hilo limeatangaza rasmi maeneo ya safari za ndege hizo ikiwa na pamoja na nauli.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa shirika hilo waliandika kuwa nauli ya safari ya ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ni shilingi laki moja na sitini (160,000/=).

ATCL wameeleza kuwa nauli za safari kwenye mikoa mingine bado hazijapangwa ila wapo kwenye mchakato.

Baada ya kumalizika kwa ofa iliyokuwa imetangwa na ATCL, Nauli halisi zitakuwa kama ifuatavyo;-
  • Dar es Salaam – Mwanza kwenda ni shilingi 160,000 hivyo kwenda na kurudi ni shilingi 320,000.
  • Dar es Salaam – Kigoma kwenda ni shilingi 395,000 hivyo kwenda na kurudi ni shilingi 610,000
  • Dar es Salaam – Arusha kwenda ni shilingi 160,000 hivyo kwenda na kurudi 320,000
  • Dar es Salaam – Mtwara kwenda ni shilingi 226,000 hivyo kwenda na kurudi 452,000
  • Arusha – Zanzibar kwenda ni shilingi 249,000
  • Zanzibar – Dar es Salaam ni shilingi 123, 000
  • Dar es Salaam – Hahaya (Comoros) kwenda ni USD 253

Nauli zote hizi zitaanza kutumia Oktoba 20, 2016.

Hilo la usd limeniuma sana ndege za Tz Usd za nini?????? Shilingi
 
Very strange.

Kama one way ticket ni 160,000 kwa nini return tciket isiwe chini ya 320,000?

Kwa nini wana encourage watu kukata one way ticket? Hawajui wanaongeza gharama za uendeshaji?

Mtu anayekata return ticket lazima awe na punguzo. Nadra kukuta reurn ticket inakuwa double ya one way ticket.
Point ya umuhimu sana. Atcl ni taasisi ya serikali inayotoa huduma ya usafiri lkn pia ndani yake kuna kipengele cha biashara japokuwa wanasema serikali haifanyi biashara. Ni vyema nauli zikapangwa kulingana na umbali, idadi ya wasafiri katika route.
 
Back
Top Bottom