Nauli mpya za kivuko KIgamboni Mbunge Ndugulile asema (Zigo kwa wananchi wasio na hatia) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nauli mpya za kivuko KIgamboni Mbunge Ndugulile asema (Zigo kwa wananchi wasio na hatia)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mkomatembo, Dec 31, 2011.

 1. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Salaam wana Jamvi,

  Leo kwenye gazeti la Uhuru na Jambo Leo kuna habari inayosema "Mbunge afichua UFISADI Kivukoni. Katika kupitia habari ndani nikaona kuwa kuna bei mpya za kivuko zimeelezwa katika habari hiyo ambayo kwa kweli ni mzigo mkubwa kwa mwananchi wa kawaida na hata yule ambae anamiliki ama gari ya kawaida au gari ya biashara. Bei hizo zilisomeka kama ifuatavyo ukilinganisha kuwa zimepanda kwa asilimia 100 katika kila upande.


  Watu wazima Tsh 200
  Baiskeli Tsh 300
  Bajaj Tsh 1,300
  Pikipiki Tsh 500
  Gari ndogo ya kawaida Tsh 1,500
  Pick up (pia huwekwa katika kundi hili station wagon, gari aina ya LAnd cruiser , n.k) Tsh 2,000
  Basi Dogo Tsh 3,500
  Magari ta tani mbili na trekta tsh 7,500

  Ndugulile ameiambia Uhuru kuwa, kuna ufisadi mkubwa upo pale ikiwemo wafanyakazi wa plae ambao ni wanaokata ticket huchapisha vitabu aina mbili tofauti. Hutumia vitabu vyao hivo feki kukatia ticket watu na matokeo yake pesa nyingi kuishia katika matumbo yao!

  Kwa siku wanadai inakusanywa Tsh million 4. tofauti na ilipokusanywa siku alipoingilia katika waziri magufuli na kuweka watu kutoka wizarani ambapo ilikusanywa Tsh Million 13.

  Aidha amedai kuwa kuna mchezo mchafu wa kuuza mafuta unaofanywa na wafanyakazi wa kivuko hicho cha kuuza mafuta kwa wenye maboti.

  Mbunge amekemea vikali ongezeko hilo na kudai kuwa kwanza serikali idhibiti wizi huu na baadae ifikirie kupandisha nauli huku ikiwashirikisha wakaazi wa Kigamboni.

  Source : Uhuru.

  Maoni yangu,

  Kama serikali iliwahi kuweka watu wake wa wizara na kukusanywa Tsh Mil 13. iweje serikali iwatoe watu hao? ina maana serikali inajua fika kuwa kuna wizi pale kwa sababu wanajua fika habari hizi.

  Kuna wakati wakuu hawa wa kivuko walitaka ruzuku kutoka serikalini wakidai kuwa kivuko kimeshindwa kujiendesha kumbe wanajua fika kuwa pesa yote inaishia katika matumbo yao!

  NAsikitika kusema haya ni ya kuwatwsha mizigo wananchi kama tunavotaka kutwisha msigo wa kulipa DOWANS kwa Tanesco kupandiha gharama kwa asilimia 155.

  KIla mwananchi anawajibika kulipia deni la dowans na ndio maana leo Tanesco imeamua kupandisha gharama zake kwa asilimia 155 ili tukamuliwe wananchi kulipa deni hilo.

  Kwa mtindo huo huo wananchi wa Kigamboni wakamuliwe kulipa gharama mara mbili ya sasa hivi, ilhali pesa ile hainedi katika mfuko wa serikali bali inaingia katika matumbo ya watu binafsi NA SERIKALI INAJUA FIKA !

  Serikali amkeni msimamie watu wenu !
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Bila bei kupanda asinge sema,ah
  aende zake huko
   
 3. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Ndio maana yake, kama angefungua mdomo wake kabla nina hakika serikali ingeweka watu madhubuti wala wasingeweza kuthubutu kupandisha nauli ! sasa tumuone atafanya nini
   
 4. B.O.G

  B.O.G Senior Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nina uhakika haukai huku kwetu , ila kiukweli tunaenda kuanza mwaka na mzigo mkubwa. Na kibaya zaidi ni huu utahira wakupandisha vitu bei kwa asilimia 100% .Nakingine ni kwamba mtu aliye pandisha ni Wakala wa ufundi na umeme kwa niaba ya wizara ya ujenzi. ambapo moja kwamoja unaona kuwa huu ni usani wa wazi wazi.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mimi kwel ckai huko ila ni mjaji wa huko,na cjafurahia ongezeko la ada ya kivuko,juz nilitoa thread kuhusu ongezeko la ada ya kivuko kabla ya hli gazet kuripot,nachojiuliza mbunge huyu alikua wapi kuelezea huo ufisadi?hadi aliposkia naul zimepanda?hapo ndo napowachukia hawa wawakilish huwa WANAFKI
   
 6. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Ina maana kwenda KIGAMBÖÑI ISHAKUWA BALAAA
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  tizo,kuanzia kesho safar za kg ziwe za ulazima tu
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Imeshakuwa anasa kuvuka kwenda kigamboni........
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  kazi ipo!
   
 10. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Nadhani kuna haja ya wana Kigamboni kugoma kwa nguvu zote ili kuonesha kuwa tunaweza!, inasikitisha sana kuona watu wanafanya mambo wajitakiavo! kwa kweli inasikitisha! kwa MSHAHARA GANI? imagine mtu wa hali ya kipato cha chini,! akitoka alikotoka anapanda basi kwa tsh 350 aunganishe na kivuko tsh 200 tayari tsh 550, akifika mjini apande basi kumpeleka mahali pake pa kazi another 350 mpaka 500 jumla 1050, na kurudi ni hivo hivo jumla mtu huyu at minimum atatumia 2,100 fanya mara 27 anazokwenda kazini jumla tsh 56,700..

  Fikiria pesa hiyo anatumia kwa ajili ya nauli tu, hajakula mtu huyo bado! hajaacha pesa mezani kwa mkewe au kwa manamke watoto nyumbani ! loooh! mtu huyu wa hali ya chini serikali inamuangalia namna gani jamani?

  Njoo kwa wale wenye magari 3,000 kwa siku na kwa mwenzi 81,000 mh! kweli tutafika ? bad hapo kibano cha umeme 155% rise mwakani jamani tunakwenda wapi?
   
 11. heshima5

  heshima5 New Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayu Ndungulile na hao anaowaita mafisadi wote ni wamoja kilichotokea ni ile hali tu yakuwa fungu linalopatikana kwenye kivuko yeye halimfikii! Hizo ml .10 ambazo kila siku zinachakachuliwa c pesa ndogo kiasi ambacho siku zote asiseme na aseme wakati huu!
   
Loading...