Nauli bila pesa: Mfumo mpya Kenya

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,573
Reaction score
53,599
[h=1]Nauli bila pesa: Mfumo mpya Kenya[/h]
1 Julai, 2014 - Saa 15:04 GMT



[h=2]Media Player[/h]
Cheza katika media player





Serikali nchini Kenya imeanzisha mfumo mpya wa kulipia nauli ya usafiri.
Katika mfumo huo unaoidhinishwa taratibu, badala ya kulipa kwa pesa taslimu, abiria analipa kwa kutumia kadi ye kielektroniki wanapoabiri matatu au kwa jina jingine daladala.
Mfumo huu mpya una maana kwamba serikali inaweza kuwatoza kodi wafanyabiashara, wa sekta hiyo, inayokadiriwa kuwa na faida ya dola bilioni 2 na nusu kwa mwaka.
Lakini wakosoaji wanasema watu wengi hawajnunua kadi hizo na hawaelewi jinsi zinavyofanya kazi.

Nauli bila pesa: Mfumo mpya Kenya - BBC Swahili - Medianuai

 
E bwana da Taratibu Tu Mtafika bora yenu serikali inatafuta vyanzo vingine vya mapato,Huku sisi ni JUISI,SIGARA NA POMBE
 
Hii serikali ya Uhuru Kenyatta ina vision ya hali ya juu sana, naamini baada ya miaka mitano Kenya itakuwa class nyingine tofauti na Tanzania na Uganda. Keep it up muamshe tuliolala, only kodi itaendeleza Afrika mashariki sio kutembeza bakuli kwa wazungu.
 
hapo safi sana, ila elimu itolewe kwa watumiaji isije kuwa kama hapa tz kuhusu mashine za tra
 
Na sisi tuna mashine za TRA madukani. Lol...ingawa wafanyabiashara walizigomea; sijajua kama zinaendelea or not....

Lakini ni nzuri kwa kudhibiti ukwepaji kodi; na rushwa za watu wa TRA...
 
nalia sana na serikali yetu kwani usafiri wa daladala endapo abiria watalipia kodi direct serikalini naamini serikali itapata fedha nyingi za kupindukia + na mabasi ya mikoani/badala ya matrafiki kunufaika/bure kizembe
 
Na sisi tuna mashine za TRA madukani. Lol...ingawa wafanyabiashara walizigomea; sijajua kama zinaendelea or not....

Lakini ni nzuri kwa kudhibiti ukwepaji kodi; na rushwa za watu wa TRA...

EFD tumekuwa nazo kwa kipindi sasa, hawafai kuzigomea, ni muhimu kulipa kodi.
 
Kweli lazima tuwe na utamaduni wa kulipa kodi; na tukiona uchungu ndio tutakuwa na sababu za kuwajibisha serikali zetu pale wanapotumia vibaya kodi yetu (no representation without taxation).

Hapa Tz tulokuwa tunalipa kodi sana sana ni watumishi wa sector rasmi...wananchi wa kawaida wanalipa indirect tax kwenye bidhaa hivyo wanakuwa less aware...na wakusanyaji (wauza maduka) hwapeleki hiyo pesa TRA....makampuni makubwa ni full rushwa....


EFD tumekuwa nazo kwa kipindi sasa, hawafai kuzigomea, ni muhimu kulipa kodi.
 

wangekuwa na vision, GDP isingeporomoka kutoka 5.2 to 4.1....wakati Tanzania ikiwa 7
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…