Natumaini (na naomba) wazo la serikali kununua korosho liwe ni mkwara tu kwa wafanyabishara

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,636
8,774
...nimemsikia Rais Magufuli akisema kuwa ikifika Jumatatu saa 10 jioni wafanyabishara ambao hawajasema kiasi cha korosho watakayo ( au kukusudia) kununua hawataruhusiwa tena kununua korosho hata kama ni kilo 50 na kuwa serikali itanunua korosho zote na kutafuta masoko nje ya nchi. Na amesema kuwa atawapigia simu marais wa nchi zinazonunua korosho ili kuhakikisha soko linapatikana.
Well; ushauri wangu wa bure ni huu:

HUO MKAKATI UMEFELI HATA KABLA YA KUANZA. Kwa nini?
1. Hao atakaowapigia simu hawataweza kuwalazimisha wafanyabishara wao wanunue korosho kama soko haliwahakikishii faida unless serikali zao zitawapa fidia.
2. Kama soko linalonunua korosho kwa bei kubwa lingekuwapo hao wafanyabishara wanaoshindwa kununua korosho leo wangekuwa wanalijua leo hii (na wasingeshindwa kununua korosho zote zilizopo).

Ushauri wangu ni huu:
Serikali iachane na dhana kuwa inaweza kufanya biashara na ikapata faida ila iwaachie private sector.
 
Back
Top Bottom