Endelea kupotezea mkuu, ya kawaida sana hayo, kama huyo dada alikubali uwe unachati naye mapaka mnavuka mipaka ya kutaniana as afriend alitegemea nini? Imekuala kwake, we piga shule
wasichana wengine wehu...lol
Jina lako na mambo yako yanashabihiana endelea tu kujifunza ndo malovee hayo mkuu angalia wasijekukukameruni..:confused3:
Tatizo msg yenyewe ukiisoma unahisi ka umebakiza saa kadhaa b4 hujafa..
Kwa ninavyowajuapolisi wetu, ukienda huko ni kama umewapelekea mlo, wengine wataanzisha urafiki na wewe, watakuomba "kitu kidogo". Mwisho wa habari hawana watalofanya. Ukija kufa itakusaidia nini polisi?Huyo kaka nae mjinga tu, kwanini asimdhibiti mpenzi wake, si ajabu hata kupendwa halipendwi ila linalazimisha tu!! Kama una wasiwasi sana mkuu, nenda na wenzako kituoni ukatoe maelezo yako, then piga shule kama kawa mengine huwa ni mkwala tu!!!
Ukute dada na boyfriend wake wanamsoma hapa wanachekaaaa alafu wanamtumia message ingine, anapanick, anazileta hapa wanacheka tena and so on.Kwa jinsi ulivyoandika hapa, inaelekea huyo 'mtu mkubwa serikalini' akikuona tu atakuonea huruma. Usiwajali,soma baba kijiji kinakutegemea urudi ukagombee ubungo. Bahari imechafuka hiyo dogo, utavamia papa nyangumi,tena wale wa hatari
Wadau naomba mawazo yenu.
Kuna binti tuko nae chuoni,ila nilifahamia nae zaidi baada ya kuattend conference pamoja hivi karibuni.
Tukabadilishana namba na tumekuwa tukichat tu mara kwa mara.saa zingine tunaflirt na yeye ndio mwanzilishi.na saa zingine namtupia jokes nnazozitoa humu ndani basi tunaenda.
Chaajabu leo niko klas nkaona simu zange nyingi zinaingia,nkawa sipokei koz pindi linasonga.
So ndio akatuma msg kuwa jamaa yake amekuja chuo na kaona msg zangu so ana hasira na kumruhumu kuwa na uhusiano namm. Sikujibu msg yenyewe.kisha akatuma nyingine kuwa nisimtafute tena wala kumusms.sijajibu tena.nlikuwa shocked na nlifadhaishwa sana nkawa nshaamua sitamtafuta tena yani nampotezea.akawa anapiga sipokei..akatuma sms ati nipokee niolngee na jamaa nimhakikishie kuwa sina uhusiano naye.nakapotezea tena.
Cha ajabu usiku huu kantumia msg kuwa ni bora ningepokea tuu simu koz jamaa wake ni mtu mkubwa sana mjini hapa amechkua namba yangu na atanitafuta na atanipata,na tena amedai atanifanyia kitu mbaya sijawahi kuona.
Sa hapa ndo nawaza na kuwazua nafkiria nimjibu nini au nifanyeje..
Naomba ushauri wenu wadau..ni hayo tu.