mwakatojofu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2008
- 326
- 227
Marekani inadaiwa na Wa-china Dollar Trilioni Mbili, ukiangali bidhaa ambazo zinauzwa USA, asilimia kubwa ya bidhaa hizo ni za kutoka kwa Wajamaa wa Kichina. Statistics zinaonyesha kuwa Chinise Food Store zimezidi Marekani kuliko jumla ya Mikidee na Burger King.
Wachina wakigoma kuleta bidhaa Marekani itakuwa sawasawa na Waarabu kugoma kuiuzia Marekani mafuta.
Wakuu, hali ndio hiyo hapa USA. Obama ameamua kununua karibu kila Benki na Insurance Companies.
Huu ni ujamaa.
hebu angalia mambo haya yafuatayo;
1. nchi tajiri zilizobobea katika 'capitalism' zinatingisika. hali si shwari tena (watu kwa maelfu wanapoteza kazi, makampuni yao yanapata hasara, serikali zinalazimika kukopa na kuingilia 'free market')
2. lakini wakati huohuo tunakumbuka kuwa: ujamaa wa rusia ulishindwa (iliparanganyika, haikuendelea sana kiviwanda kama marekani na ulaya magharibi), na ujamaa wa tanzania chini ya nyerere ulishindwa (kuadimika kwa bidhaa na nk.)
sasa katika hali kama hii kwanini china inaendelea kusonga mbele? yenyewe si inafuata ujamaa kama nchi zingine za iliyokuwa ulaya mashariki ambako kulikuwa hamna maendeleo? au china imechanganya capitalism na ujamaa? au ujamaa wa china una vionjo tofauti?
..........Shati liloshonwa hapa USA bei yake ni Dollar 80 na kuendelea, Shati la kampuni hiyo hiyo lilishonewa Bangladesh au Uchina linauzwa dollar 12 mpaka 19.....................
Wachina ni wajanja na wana moyo na nchi yao, wao wakija kusoma ni wanasoma kweli na wanarudi kwao kuendeleza mambo, yaani huwa wanajua wanachofanya. Ni kweli vitu vingi sana ni vya China, yaani kwa mfano Computer ukiifungua ndani karibu vitu vyoote ni vya China kasoro Box tu lililobeba nje ndio limeandikwa Made in America.hapa napata picha kuwa marekani kutabaki kukiwa na upungufu wa ajira na watakosa kodi fulani kutokana na kuwa production haifanyiki kwao.
lakini kama kampuni inayozalisha china ina labda ofis/makao makuu katka marekani ni wazi marekani watakuwa wanapata kodi fulani kutokana na ufanyaji kazi wa hiyo kampuni nje ya marekani
hapa naona tofauti na tz. vitu vingi vinavyouzwa madukani vinatoka kenya na sehemu zingine. lakini sio kampuni za kitz zinazofanya productions hizo nje
na majuz juzi nimesoma kuwa marekani imewekeza a lot in research. wakati huohuo china haijawekeza sana katka research. hii inanipa picha kuwa china inategemea technology kutoka nje - ama kwa kuinunua au kwa kuiba (miezi/miaka kadhaa nyuma niliwahi kusikia habari za mchina aliyepatikana na hatia ya kuiba technology katka marekani na kuipeleka china).
Maswali yako ni matamu sana na yanahitaji majibu ya kifanisi.
Kwasasa Wamarekani ni consumers na sio producers. Shati liloshonwa hapa USA bei yake ni Dollar 80 na kuendelea, Shati la kampuni hiyo hiyo lilishonewa Bangladesh au Uchina linauzwa dollar 12 mpaka 19, electronics karibia zote hazitengenezwi hapa.
Juzijuzi nilikuwa kwenye duka la ujenzi, chakushangaza nikuwa, hata mbao za ujezi zilikuwa zimetoka China na Sweden.
Swali lako linabakia palepale, je Wachina wanafuata mfumo gani, au ujamaa wao unavionjo tofaudi?