Nilikuwa napita kwa Web ya Wizara ya Fedha na Uchumi ghafla nikakutana na hiki kitu. Kiumri inaonekana kama imepitwa na wakati lakini kimantiki inaweza kuwa na msaada na mahali pazuri kuanzia pa kuelewa jinsi (kama taifa/nchi) tunachomiliki na kudaiwa. Sikuwa naelewa vizuri sana na hivyo sikuweza kuchambua kwa undani. Naomba wataalamu wa mambo hayo watuchanganulie maana ya haya majedwali na mustakabali wetu katika kizazi hiki na kijacho.