Sr. Magdalena
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 803
- 472
Sr. Magdalena,
Jambo haliwi mpaka limekuwa, na ijapokuwa mawingu ni dalili za mvua, mvua haijanyesha bado na inavyoelekea huenda ikanyesha ndivyo sivyo.
Kumradhi Shark,Acha kuongopea watu mkuu,
Vitu vingine unaweza kuamua kuving'ang'ania vikakugeuka baadae,
We mwenyewe uliona huko kamatini "sio" ukaamua kujiweka kando,
Sasa unatetea nini tena?
Meneno aliyotumia Sr. Magdalena yanarejea katika ukweli wa historia ya NCCR-Mageuzi (chimbuko lake)Mkuu umekosea kidogo. NCCR -Mageuzi haikuwa na nia ya kudai katiba mpya na hata kirefu chake umekikosea kidogo. hiyo inaitwa National Committee for Construction and Reform -Mageuzi na sio Consitution kama ulivyoandika. Lengo lao ilikuwa ni kudai mabadiliko katika mfumo wa siasa na katiba ilikuwa ni kipengere kidogo tu ndani ya madai yao ya mabadiliko. Lakini ulicho sahihi ni kwamba ilikuwa ni kamati tu ya kudai mabadiliko ya mfumo wa siasa na baada ya mfumo kubadilika kamati ikajigeuza na kuwa chama cha siasa.
Hizi kamati za arusi mwisho wake 2015 tu.
Kumradhi Shark,
sijakuongopea wewe wala awaye yeyote. Hiyo habari ya kujiweka kando ilipotoshwa. Mimi ni mwanachama hai wa NCCR, na usitarajie iwe vinginevyo. Baada ya NCCR kubadilishwa kuwa chama, neno Committee liliachwa, badala yake neno lililoko kwa msajiri ni Convention.
Ilipotoshwaje tena mkuu??
Nakumbuka wewe ndie ulietuambia kua unang'oka uongozi (sio uanachama),
So kama ni issue za kupotoshana basi wewe ndie ulietupotosha!!!
Ndugu yangu Shark,
Aking'oka mtu uongozi wa chama hatakiwi kusema lolote kuhusu chama ambacho yeye anaendelea kuwa mwanachama hai?
NCCR sio chama,
Ni kamati tu kama kamati zingine za msiba, harusi, kitchen party, n.k
Ndio maana hawaeleweki eleweki
Sr. Magdalena,Heshima mbele sana mkuu Kahangwa.
Mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yamepitishwa leo na bunge la JMT, je bado hamuoni ni wakati muafaka wa kubadili jina la chama, napendekeza kama lingekuwa la kiswahili, na hakika wanachama wengi wa NCCR hawajui kirefu chake na wala kinasimamia nini...