Natatizwa na hili la kuweka vikao vya mazishi kwenye mabaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natatizwa na hili la kuweka vikao vya mazishi kwenye mabaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngekewa, Mar 5, 2009.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Watanzania wenzangu nimekuwa nikitatizwa na mawazo kila nikisikia kipindi cha matangazo ya kifo kuwa mipango ya mazishi inafanyika BAA FULANI. Natatizwa na moyo wangu hasa nikiangalia jinsi mahusiano ya vitu viwili hivi yalivyo tofauti kabisa.
  Nikiiangalia Baa na namna Watanzania tulivyoifanya kuwa ni sehemu ya machafu yote na baadae nikiangalia ile safari ya yule anaeandaliwa kuenda naona kuwa kama yule maiti hatendewi haki. Kupenda kwetu kote kwa mastarehe naamini moyoni kuwa unapofika umauti mambo hayo yote huwa hayana faida kwa maiti bali swala na dua ndio kitu kinachomfaa.
  Dini zote hata za kuabudu mizimu inajali safari ya mwisho sasa tunapoamuwa kuijadili na kuitayarisha safari hiyo pahala panapofanyika machafu ndio tunajali safari hiyo? Tukumbuke kuwa Waswahili walisema 'muosha nae huoshw√°'na kama tunaamini dini zetu basi na sisi utakapofika wakati wetu safari zetu zitapangwa kwenye vilabu vya pombe, sijui kama safari za namna hiyo zitakuwa za kubarikiwa?
   
 2. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,559
  Likes Received: 1,325
  Trophy Points: 280
  Ngekewa

  Binafsi huwa natatizwa na hili suala na nilijaribu kuuliza katika msiba fulani
  nilijibiwa kama ifuatavyo
  1. sababu ya kwanza kufanywa kwenye sehemu ya baa ni either mfiwa kutokuwa na sehemu yake rasmi ama kutokua na nafasi ya kutosheleza sehemu aliyokua anaishi marehemu.

  2. Niliambiwa pia kuna sehemu nyingine wanaishi watu ni vigumu kumwelekeza
  mtu yeyote anayependa kushiriki aweze kufuka so sehemu za bar inakuwa rahisi.

  3. Marehemu kutokuwa na ndugu wa karibu ambao wangependa msiba ufanyike kwao so mipango ya mazishi inafanyika bar na wakati wa kuaga mwili unafanyikia hopitalini, kanisani au sehemu itakayoamualiwa.

  4. Niliambiwa pia sababu ingine marehemu alikua mpenda ulabu so wanaenzi aliyokuwa anayafanya enzi za uhai wake

  pamoja na sababu hizo bado mimi sijaridhishwa na kufanyia taratibu za mazishi kwenye bar.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  WACHAGGA HASA HASA ndio zao.Na huu utaratibu upo sana huku mijini!

  Lakini Hakuna tatizo na hilo,kwa sisi great thinkers tunakwambia IT IS THE SIGN OF TIMES!ni muda wa kizazi cha aina nyingine kabisa.times have changed,and so IS THE LIFE STYLE
   
 4. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2009
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Pia kuna hili la matumizi makubwa ya pesa kwa ajili ya mazishi,wakati mwingine marehemu amekufa kwa ugonjwa wa kutibia kwa elfu kumi au ishirini,tunashindwa kumchangia ili kuokoa uhai,akisahakufa ndo tunachanga na kua na moving camera kwenye mazishi,,nashindwa kuelewa
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ngekewa nadhani unatatizwa na tafsiri ya baa na sio kufanyika mikutano kwenye baa flani, kwa mujibu wa tafsiri yako baa ni mahala ambapo uchafu wote hufanyika. Ukiangalia msimamo huo kwanza sio sahihi kabisa kwani baa si lazima kila baa mambo machafu yanafanyika pia hata kama yanafanyika sio baa inayofanya mambo hayo bali ni watu.Na ndio maana hata maeneo yaliyowahi kuwa baa au nyumba za starehe leo hii ni sehemu za ibada(silent inn, ruaha galax n.k). Sidhani kama umeangalia mazingira yanayosukuma watu kufanya mikutano ya maandalizi ya mazishi huko kwenye mabaa. Miongoni mwa mambo machache ni pamoja na kufuata huduma kama viti meza na eneo linaloweza kubrba watu wengi kwa wakati mmoja bila kuleta usumbufu. Pia kwakuwa shughuli ya maandalizi inawahusu baadhi ya wahusika tu,hivyo ni muhimu zoezi hili likafanyika sehemu mbali na msiba. Na kuna wenzetu wengi ambao huishi mbali na nyumbani kwao kwa asili hasa mijini kwa kupanga chumba kimoja au kwenye flats zenye wapangaji wengi. Katika hali kama hii wakati mauti inapomfika mtu huyu mwili wake huhifadhiwa hospitali huku taratibu za kumhifadhi zikifanyika bila kuingilia utaratibu wa wapangaji wenzake. Mfano mwingine ni jamii za wachaga ambao wengi wao ni wafanya biashara mijini na kimila kwao ni lazima wakazikwe kwenye viwanja vya familia huko kwao.Katika hali kama hii wafiwa hutafuta njia za kupunguza kuwa na misiba sehemu mbili(yaani nyumbani kwa marehemu na kijijini kwao) na hivyo hufanya vikao vya maandalizi baa na sio kwa marehemu.Kulingana na mazingira na hali ya uchumi utaratibu huu unasaidia sana kupunguza gharama na mzigo usio wa lazima kwa wafiwa. Nadhani ni utaratibu mzuri kuigwa na jamii nyingine ilikupunguza shughuli zisizokuwa na tija kwa familia ya wafiwa, pia ni vyema bila kuathiri sheria,kanuni na taratibu au imani ya wahusika jamii nyingine zingebuni utaratibu kama huu. Hii inamaana kama wewe imani yako hairuhusu uende baa ni vyema mikutano ya maandalizi ikafanyika kwenye baraza za kahawa au mighahawa au nyumba za ibada. Na kwa jinsi hii tutapunguza msululu wa watu nyumbani kwa wafiwa na kuachana utaratibu wa matanga ambao huongeza uchungu(kwa kununua vyakula,kusafisha mazingira yanayo haribiwa na kundi la watu bila sababu za muhimu)
   
 6. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180

  hata kama una point za maana siwezi kusoma maana hilo picha lako huwa linaondoa stimu kabisa. Yaani huwa naruka haraka sana posti zako. Sorry about that.
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sehemu tu Inayojulikana na Rahisi Kufikika na Wengi!

  Kwani Baa sii lazima tu ulevi..kuna soda, viburudisho, maji, viti n.k

  Halafu Bar hakuna kulipia ukumbi..mkinunua hata maji tu tosha!

  Ndo mambo ya mjini hayo haswa Bongo ..vijijini ni tofauti!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Sioni tatizo lolote la kufanyika vya vikao katika baa! Aidha tamaduni nyingi hapo bongo maziko uendana na ulabu...
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sijababaishwa na baa bali ni mahusiano kati ya matendo ya pahala panapoitwa baa na heshima ya safari inayokusudiwa kuzungumzwa. Juu ya sababu zote za kupunguza gharama lakini bado suala langu basi hatuwezi kutafuta sehemu nyengine?
  Dini zetu zote zinakataza shughuli muhimu zinazofanya kuwekwa baa na hata maisha yetu ya kawaida tunapaona baa si pahala pa kwenda mtu yeyote na ndio maana tunashituka tukiona watoto wetu wanaonekana huko. Dini ni imani na imani hizo ndio zinatufanya tuhisi kuwa mtu aliefariki anahitaji nafasi maalum iliyo karibu na muumba na iwapo muumba amekataza baa basi si heri kwa yule ambae anaelekea kwake tumuhusanishe na makatazo.
   
 10. 3

  3 kids Member

  #10
  Mar 6, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata mie huwa naogopa sana hilo picha nikifika hapo huwa nasikia kuchefuka,sory
   
 11. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Picha ya kutisha na kutoweka nafasi kati ya wazo moja na lingine (paragraphs) kunafanya hata nini nishindwe kusoma michango ya Burn. Rekebisha tafadhali.

  Baa si lazima iwe kitu kibaya. Kuna wengine hazipandi mpaka tutulie na marafiki zetu baa.
   
Loading...