Natangaza rasmi kuwaunga Mkono CHADEMA na UKAWA

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Ndugu zangu,

Kwa muda mrefu nimekuwa nikiitetea CCM na kuipinga CHADEMA na UKAWA kwa kila jambo. Nilikuwa ninafanya hivyo bila ya shinikizo lolote. Ni mapenzi yangu kwa CCM na chuki yangu kwa CHADEMA.

Siku zimeenda na siasa imebadilika. Nimeona sasa nianze na mwelekeo mpya wa siasa zangu jukwaani. Si kila kitu cha CHADEMA nitakuwa nakipinga. Nitawaunga mkono pale nitakapoona wanafanya mambo ambayo yana mantiki.

Kwa leo naanza kuwaunga mkono kwa huu uamuzi wao wa kutoka Bungeni. Hakika ilikuwa inanikera sana kila Naibu Spika anapoingia wabunge wa UKAWA wanatoka nje ya Bunge. Niliona kuwa huo ni utoto wa hali ya juu sana na kukosa uzalendo. Baada ya kutafakari sana, nimeona kuwa kumbe nilikuwa napotoka. CHADEMA na UKAWA wapo sahihi kwa suala hili la kutoka nje.

Dr Tulia Akson ni Naibu Spika Makini kuweza kutokea hapa nchini. Hakika anasimamia sana sheria na kanuni bila kupindisha. Freeman Mbowe baada ya kuona hawezi kushindana na cha Dokta, akabuni mbinu hii ya kumkimbia Tulia kila aongozapo Bunge.

Pia, wabunge wetu wa CHADEMA hakika wameshindwa kujibehave wanapokuwa bungeni. Wanaropoka hovyo na kila wakifanya hivyo wanakumbana na rungu la Naibu Spika na kwa hakika adhabu wanazopata wamekuwa wakistahili. Kuonesha kuwa wanakubaliana na adhabu hizo, wameshindwa kukata rufaa kupinga maamuzi ya Bunge licha ya kupewa fursa hiyo.

Hivyo natangaza rasmi kuwaunga Mkono CHADEMA na UKAWA katika hili.

Mniwie radhi kwa wale niliowakwaza.
 
Umeshindwa kusafisha jiji unatuletea upupu humu,nyie si ndio mnataka binadamu wenzenu waishi kama mashetani?.

Mnakera sana nyie Lumumba
 
kwa ana makinda alikuwa hajui kanuni na sheria za nchi kuliko tulia?
Jibu lake alishatoa James Mbatia. Kuwa yule mama alikuwa na uvumilivu sana na wabunge wa CHADEMA wanapokosea, alikuwa anawaandikia vimemo vya kuwaita ofisini kwake, wanazungumza huko na wanayamaliza bila kutoa adhabu. Dr Tulia ni tofauti
 
Dah! Niliingia kwenye huu uzi nikiwa na hasira tele nikadhani kaka yangu Chabruma tumempoteza. Ahsante nimekupata
 
Back
Top Bottom