Natangaza nia mwaka 2015

Natangaza nia mwaka 2015

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,408
1.baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kutangaza nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 sera zangu.

miundo mbinu: ninapanga kufanya usafiri wa treni kuwa njia kuu ya usafirishaji tanzania. kwa hapa ninapanga kuimarisha reli ya kati kwa viwango vya kimataifa, kuijenga mpaka DRC, ninapanga kujenga reli kutoka bandari ya mtwarakupitia mbeya, rukwa katavi hadi tabora, kuimarisha reli ya tanga musoma. kwa kuanzia ninapanga kuimarisha bandari ya dar kwa kuongeza uwezo wake. ninategemea kuweka treni za kisasa reli ya kati kuanzia dar hadi mwanza na kigoma. ninategemea kuanzisha treni kutoka mtwara kupitia mbeya, rukwa, katavi, kupitia tabora hadi mwanza, kuanzisha treni kutoka dar kupitia tanga kilimanjaro hadi musoma. baada ya kutengeneza mtandao huu wa reli nitaanza kujenga bara bara za lami kuwa feeder za reli.

mategemeo yangu hapa ni kupunguza gharama za usafiri kwa wananchi, kuimarisha usafiri baina ya kanda na kanda, kuongeza kiwango cha mizigo ya nchi jirani inayopitia kwetu hivyo kuongeza pato la taifa. nategemea usafiri wa treni utachochea utalii wa ndani na hivyo kutengeneza ajira. Pia treni kuanzia mtwara kupitia ukanda wa kusini hadi mwanza itafungua soko la mazao ya chakula yanayozalishwa kusini kwa nchi za kasikazini

rasilimali za taifa: sera yangu kuhusu rasilimali za taifa ni kwamba mbia atakaribishwa kuwekeza pale tu serikali itakapokuwa inapata asilimia 50% ya mapato ghafi au zaidi. pungufu ya hapo ni hasara kwa taifa hatutaruhusu mgeni kuja kuvuna hiyo mali bali tutafanya mipango ya kuwawezesha wazalendo kifedha na kiteknolojia waje kuvuna mali hizo.

mategemeo ni kuwa sera hii italinda mali za taifa zisiporwe kupitia rushwa na kutokujua.

Kilimo: nikiingia madarakani ninategemea kulifanya ghala la chakula la taifa kuwa shirika linalonunua chakula wakati wa msimu nchi nzima kila zao linalohifadhika na kuuza wakati wa upungu. nitatoa msamaha wa kodi kwa mazao yote ya chakula yanayosafirishwa nje ya nchi na nitafungua mipaka yote chakula kiuzwe nje. nitahamasisha utengezaji wa bidhaa zitokanazo na mazao ya chakula kwa wingi.

lengo la sera hii ni kutoa soko kwa mkulima na soko la chakula ndilo pekee litakalochochea ukuaji wa kilimo kwa wakulima kuongeza kilimo kila msimu. serikali itajitahidi kwa upande wake kujenga mabwawa ya maji, mifumo ya umwagiliaji. pia itawawezesha wakulima kupata pembejeo kwa urahisi. kutokana na kufungua soko mategemeo ni kwamba kwa kuanzia kunaweza kusababisha upungufu wa chakula jambo ambalo serikali itatenga fungu la dharula kuagiza chakula kutoka nchi zilizokwisha jidhatiti katika kilimo ili kukabiliana na upungufu. ninaamini nguvu ya soko itawasukuma wakulima kuongeza ukulima na kuvutia watu kuwekeza katika kilimo na kufanya tujitosheleze na soko la jirani katika kipindi cha miaka michache.


kandarasi: sera yangu ni kufanya kandarasi za ujenzi kufanywa na wazalendo kwa asilia 75 na wageni kufanya asilia 25 tu. hii nitaifanya kwa kuanzisha kituo cha kuwaunganisha wataalamu wazalendo kupitia kampuni zitakazoanzishwa ama na wao wenyewe au na serikali na kuwauzia watanzania hisa. kila kampuni itayokuwa inakuja kufanya kazi nchini lazima tuweke masharti ya kushirikiana na kampuni za kizalendo ndio wapate kazi.

wafungwa: sera yangu ni kwamba ni naamini magereza ni sehemu ya kumrekebisha mtu tabia hivyo ninaamini kila mfungwa ana haki ya kufanya kazi. nitanya kazi ya kilimo isiyo na mshahara kuwa ndio kazi ya wafungwa. Hapa wafungwa watakuwa wakiishi kila mtu na sehemu yake ya kulala kama maisha ya mtanzania wa kipato cha chini bali anakuwa anafanya kazi isiyokuwa na mshahara na kutengwa na familia yake, tutafungua mashamba makubwa maporini na magereza zote zitahamishiwa maporini. huko watakuwa wakifanya kazi ya kilimo na mazao yatokanayo na kilimo yatauzwa na kuwaboreshea mazingira ya kuishi. iwapo watazalisha sana ziada watakuwa wakitunziwa na kukabidhiwa pale wanapotoka magerezani ili wakaanzie maisha.

nitaendelea kutoa sera zangu kadiri muda unavyokwenda kabla ya 2015
 
Ebu tujuze kwa utambulsho kwanza,jina kamil,uraia,umri,chama kipi unatoke?,nk ili tukusome fresh
 
Ebu tujuze kwa utambulsho kwanza,jina kamil,uraia,umri,chama kipi unatoke?,nk ili tukusome fresh

kwanza nauza sera zikikubalika mtanijua maana mchakato ni mrefu
 
kwanza nauza sera zikikubalika mtanijua maana mchakato ni mrefu

Ni sharti Tukufahamu dnugu! kwa maana SERA HATA ZIWE NZURI VIPI LAKINI ZIKITEKELEZWA NA MTU DHAIFU KAZI NI BURE. Sera na mtu zinacomplement each other ktk wananchi kufanya decission. So jitambulishe, elezea kidogo historia yako, umefanya nini kwa watanzania mpaka hapa, hadi ukaona kuna mambo umeshindwa kuyatekeleza vizuri sharti upate uongozi wa juu kabisa hapa nchini.Nitaendelea kukunyonya kadri unavyofunguka!
 
Mbona haujaongelea elimu? 2015 imekaribia, najua wale vichwa maji watakimbilia hapa haraka kupora sera zako.
 
Jamaa kadesa kila kitu kwenye ilani za chadema, ilani ya 2005 na ile ya 2010 ilisha yaongelea hayo, tena mgombea alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa mfuko wa saruji na mabati yatakuwa elfu 5 ili kuwawezesha watu wa kipato cha chini kumudu gharama za ujenzi.

Na bado, ya mwaka 2015 itakuwa na mengi yenye unafuu kwa mwananchi wa kawaida.
 
Unagombea urais wa kitu gani ? Maana kuna marais wengi sana hata chama cha ngoma vipo vyenye marais wao , au chama cha bao!
 
kwanza nauza sera zikikubalika mtanijua maana mchakato ni mrefu

nimepitia sera zako zote lakini bado zinapwaya kwenye sera mama tuliyonayo "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"
 
Weka jina lako halisi tukujue mapema ili tuifuatilie historia yako!Nia tumeiona ila mtoa nia hajajulikana kwa wapelekewa nia!
 
2.
Ni sharti Tukufahamu dnugu! kwa maana SERA HATA ZIWE NZURI VIPI LAKINI ZIKITEKELEZWA NA MTU DHAIFU KAZI NI BURE. Sera na mtu zinacomplement each other ktk wananchi kufanya decission. So jitambulishe, elezea kidogo historia yako, umefanya nini kwa watanzania mpaka hapa, hadi ukaona kuna mambo umeshindwa kuyatekeleza vizuri sharti upate uongozi wa juu kabisa hapa nchini.Nitaendelea kukunyonya kadri unavyofunguka!

kunifahamu mtanifahamu maana kuwania urahisi lazima ufahamike, ila unaomba hitimisho wakati hotuba yangu ndio iko kwenye utangulizi. usiwe na haraka nikimaliza sera zangu nitajitambulisha mimi ni nani? mpaka sasa nimelifanyia nini taifa hili lakini kikubwa ni ninapanga kulifanyia nini. mipango yangu itaendana na sera zangu ambazo zitahitaji kuungwa mkono na watu maana mimi peke yangu siwezi kufanyia taifa hili chochote. bali kwa kutoa dira ambayo watanzania wote tutashirikiana kulijenga taifa hili mwisho wa siku sote tunakuwa tumefanya jambo.

ki mantiki hakuna mtu dhaifu kwa jinsi mimi ninavyoamini bali mifumo ndio dhaifu au imara. ukiwa na mtu jasiri hata kufikia kukamata wakubwa wake wa kazi na magendo kama mfumo ni dhaifu huyo jasiri ndiye atakayeishia kuonekana dhaifu. kama mfumo ni imara hata yule unayemdhani ni dhaifu mfumo utamlazimisha kuwa jasiri.

kwangu mimi ninategemea kutengeneza mfumo wa utala wa nchi hii kuwa imara. mfumo wa utawala unakuwa imara pale tu unapotengeneza mfumo wa kusimamiana. kwanza ni kuanzia na mihimili mikuu ya utawala wa nchi hii yaani bunge lifanye kazi yake ya kusimamia na kuishauri serikali, mahakama ifanye kazi yake ya kutoa haki, na serikali ifanye kazi yake ya kusimamia rasilimali za taifa na kuwahudumia wananchi. hapa ili kila mmhimili ufanye kazi yake vizuri unahitaji kuwa na uhuru wake kamili usiotegemea mhimili mwingine.

mategemeo yangu ni kuifanya mahakama ijitegemee kwa kupewa bajeti yake moja kwa moja ikitengwa kulingana na pato la taifa, jaji mkuu atakuwa akipatikana kwa kugombea na kuchaguliwa na majaji kulingana na sifa, watendaji wote wa mahakama watatokana na mfumo wa mahakama yenyewe na sio kuteuliwa kutoka serikalini.tutawawekea mfumo wa kuwajibishana wenyewe pale mmoja anapokosea na mwisho wa siku kama mfumo wa mahakama utakuwa hauridhishi majukumu tunayarudisha kwa wananchi kuwajibisha viongozi wakuu na kutoa nafasi ya kuchaguliwa wapya

bunge nalo hivyo hivyo.
 
Jamaa kadesa kila kitu kwenye ilani za chadema, ilani ya 2005 na ile ya 2010 ilisha yaongelea hayo, tena mgombea alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa mfuko wa saruji na mabati yatakuwa elfu 5 ili kuwawezesha watu wa kipato cha chini kumudu gharama za ujenzi.

Na bado, ya mwaka 2015 itakuwa na mengi yenye unafuu kwa mwananchi wa kawaida.

nashindwa kuelewa watanzania mnataka nini? siasa ni kama bidhaa ambazo wengi watapita na kunadi sera zao kazi yenu ni kuchambua ipi nzuri kwa kupima kile kinachowafaa kwa maana kinatekelezeka, kinamwelekeo mzuri kulinganisha na sera nyingine zilizopo.

kuhusu hoja yako kuwa kuna wengi wameenda mbali zaidi nakuhakikishia bado ninachambua sera zangu na hapo baadaye utakuja kujua jinsi gani ninapanga kuimarisha uchumi, kuimarisha huduma za jamii, mfumo wa elimu, jinsi gani ninapanga kuanzisha kitengo cha mahusiano ya ndani kitakachoweza kushughulikia mahusiano ya jamii, kuangalia kila dini ziwe na taratibu, vyama vya siasa viwe na miiko ya kitanzania, vikundi viwe na miiko, vyombo vya habari viwe na miiko, viongozi wawe na miiko na mengine
 
3.
nimepitia sera zako zote lakini bado zinapwaya kwenye sera mama tuliyonayo "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"

maisha bora kwa kila mtanzania ni jambo linalowezekana ila si kwa siku moja ila kanuni yake ni kupunguza fedha zinazotoka nje ya mipaka ili zibaki ndani na kutoa ajira, kuongeza bidhaa zinazotoka nje ya mipaka ili zikachote fedha katika mizunguko ya fedha ya nchi nyingine na kuleta katika mzunguko wetu, kuchochea sekta nyingi zaidi kukua ili fedha inayobaki katika katika mzunguko iwe na mizunguko mingi zaidi maana zikibzki katika mizunguko ile ile zitasababisha mfumuko wa bei, kuchochea uzalishaji wa ndani, kupanga huduma za jamii katika makundi ili huduma muhimu basic needs ziwe na unafuu wa kodi ili kila mtu amudu
 
4. Mpangilio wa miji na ukuaji wa miji: kiukweli miji yetu inakua kwa kasi huku mipango miji wakiwa wamelala. miji inakua na bila kuchukua hatua sasa miji yetu itabaki kuwa shagalabala daima. iwapo nitafanikiwa kuhamia magogoni nitahakikisha upimaji wa miji unapewa kipaumbele. nitahakikisha tunapima viwanja na kuvigawa kwa bei ndogo kabisa ambayo mlalahoi anamudu, tutapiga marufuku ujenzi katika viwanja visivyopimwa, tutahakikisha kwa maeneo ambayo ujenzi unaendelea kwa sasa kila nyumba inafikiwa na barabara.
 
ili kuimarisha uchumi wa nchi
 
5. ili kuimarisha uchumi pamoja na kuimarisha kilimo kama nilivyoeleza nikitegemea katika kipindi cha miaka mitano mauzo ya mazao ya chakula nje ya nchi yataongezeka,uzalishaji katika kilimo utaongezeka, wastani wa pato kwa mkulima litaongezeka na kupunguza umasikini kwa kiasi kikubwa.

ama njia yangu ya kufanya reli kuwa njia kuu ya usafirishaji hapa nchini itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za usafirishaji, kuongeza uhakika wa usafiri na hivyo kuchochea biashara ndani ya jamii yetu na majirani zetu na hivyo kukuza pato la mtanzania kwa ujumla.

pia pamoja na kutumia treni kwa usafirishaji wa mizigo na abiria pia ninategemea kuhamasisha kupitia kodi na elimu matumizi ya gesi asilia katika magari yetu, viwanda vyetu na majumbani. hii itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya mafuta kama petroli na dizeli na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa fedha zilinazopelekwa nje ya nchi kila mwaka kununua mafuta hayo.

tuna tatizo la bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi kumiminika katika soko letu na kuchota fedha zetu kuzipeleka nje ya nchi. ili kudhibiti uchumi kunahitaji balansi usizuie sana lakini usiruhusu sana. matokeo ya bidhaa hizi imekuwa ni watu kumudu vitu vya anasa huku wakishindwa kumudu mahitaji ya msingi ya maisha. unakuta kijana ana simu tatu na zote ziko hewani lakini hawezi kujilisha, utakuta mtu ana magari mawili matatu lakini hana nyumba. kwa hapa nategemea kugawa bidhaa katika makundi mawili kundi la kwanza ni bidhaa muhimu kwa maisha. hapa naongelea chakula, nyumba (pamoja na viwanja) afya na elimu. haya yatakuwa na kodi ndogo sana ama kodi zake kufutwa kabisa ili kumuwezesha kila mtu kumudu. serikali itaweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ya huduma hizi kitaifa. kundi jingine litakuwa ni bidhaa nyingine ambazo haziko katika kundi la kwanza zinazozalishwa ndani. hizi zitakuwa na kodi ya kawaida na kupunguza kodi kwa bidhaa zinazozalishwa nchini na kuuzwa nje ya nchi. lengo kubwa hapa ni kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa hizo kwa hapa nchini. kundi jingine ni bidhaa zisizo katika kundi la kwanza zinazozalishwa nje ya nchi. hizi zitakuwa na kodi kubwa ili kulinda bidhaa zinazozalishwa nchini na kulinda uchumi wetu. bidhaa za nje zitakuwa na madaraja pia kukiwa na bidhaa muhimu zikiwa na unafuu kulinganisha na bidhaa za anasa.

natemea kuimarisha sido ambayo itakuwa na jukumu la kuunda vikundi vya vijana vya uzalizaji katika nyanja za ushonaji nguo, bidhaa za ngozi, usindikaji wa matunda, usindikaji wa vyakula, uzalishaji wa bidhaa za vyuma, na nyingine, sido itaanzisha viwanda vidogo na kuviuza kwa watanzania au kuwauzia hisa na kuwakabidhi ili waviendeshe.

tutahamasisha utalii wa ndani kupitia uanzishwaji wa treni za kisasa
 
6. Sekta ya uchumi ni sekta pana sana ambayo ndiyo uti wa mgongo wa serikali. Huduma zote za jamii zinategemea uwezo wa nchi kiuchumi. Kitaifa tunalotatizo kubwa katika kutambua ni lipi tulipe kipaumbele katika mipango yetu ili tukuze uchumi wetu kwa kasi sana. tatizo hili limeenda mbali zaidi kwa baadhi ya miradi kuanzishwa na kutelekezwa katikati ikiacha fedha zilizowekezwa kupotea. Hapa pia tumekuwa na tatizo la wale waliopewa dhamana kupendelea miradi ya maeneo Fulani na kuacha miradi ambayo ingetupeleka mbele kiuchumi. kutatua matatizo haya nategemea kuunda kitengo cha uchumi sambamba na TRA.Kitengo hiki cha uchumi kitakuwa na jukumu la kubuni vyanzo vipya vya mapato kila mwaka, kupanga vipaumbele vya taifa katika mtizamo wa mda mfupi, kati na mda mrefu. kutoa dira ya mapato na matumizi ya serikali kwa kila mwaka. hapa watakuwa wanabainisha ni asilimia ngapi ya pato ipelekwe katika miradi ya maendeleo na miradi ipi ipewe kipaumbele ili tukue kiuchumi. kitengo hiki kitakuwa kinawajibika kutambua rasimali zote za taifa na kutoa mwongozo kwa kila rasilimali njia ya uvunaji ambayo itakuwa imefanyiwa utafiti kuwa njia njia bora ya kuvuna kwa taifa letu kiuchumi. hapa mfano tunaweza kuongelea rasimali kama madini hapa kitengo hiki kitatafiti iwapo tuvune madini yetu kwa kuwasapoti wachimbaji wadogowadogo au tuchanganye wachimbaji wadogo na makampuni makubwa ya kimataifa au tutumie makampuni ya kimaifa. kigezo kikubwa ni Tanzania mwisho wa siku inapata nini kutokana na rasilimali madini iliyonayo.
 
Utagombea wapi? Tanganyika? Zanzibar? Au tanzania?

hapa cha msingi tusubiri katiba mpya ionyeshe mwelekeo tuangalie ili kuweka mfumo huu ninaopendekeza ni nafasi ipi inatoa mwanya wa kutekeleza haya ninayowaeleza ninapanga kuyafanya
 
7. Sekta ya viwanda ndio seita mama kwa uchumi wa nchi. katika uongozi wangu tutaainisha viwanda katika madaraja matatu. Yaani viwanda vidogovidogo, viwanda vya kati na viwanda vikubwa. nategemea kuweka mazingira bora na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vikubwa hapa nchini kuhudumia soko la ndani na nje. hapa nategemea kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, kuhakikisha upatikanaji wa njia za usafirishaji za uhakika na tatu kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na mwisho ni kuwahamasisha wafanyabiashara wa ndani na nje kuwekeza nchini. sekta hii ya viwanda vikubwa ikikua itawezesha watanzania wengi kupata ajira, pia serikali itapata mapato kupitia kodi na tozo mbalimbali. Viwanda vya kati nitahakikisha tunawahamasisha wafanyabiashara wa ndani na nje hasa hapa tutaweka mazingira mazuri kwa wafanyabishara wa ndani kukopa katika mabenki yetu na kuanzisha viwanda. tutawawekea masharti mazuri ya kuingiza mitambo ya viwanda kwa ushuru mdogo na kuweka masharti nafuu ya kuanzisha viwanda. kwa viwanda vidogo vidogo tunategemea kuanzisha utaratibu wa kuwakopesha vijana wanaomaliza veta na vyuo mikopo midogomidogo, na masharti rafiki ya kuanzia biashara. hapa ninategemea kupitia viwanda vidogo vidogo kwa mtanzania yeyote ambaye kuna bidhaa inatoka nje ya nchi na ina soko hapa nchini la kumuwezesha kufanya biashara na amezisoma bidhaa hizo na kuona anauwezo wa kuzizalisha kwa brand ya kwake tutawawezesha vijana hawa ili wazalishe bidhaa hizo kwa hapa nchini. mategemeo yangu ni sekta ya viwanda kukua kwa kasi ili kupunguza watanzania wanaotegemea kilimo ili tubaki na asilia ndogo katika kilimo lakini inayotumia nyenzo na kuzalisha kwa wingi na kukabiliana na ongezeko kubwa la watu wanaohamia mijini kutoka vijijini.
 
Back
Top Bottom