Natamani siku zingerudi nyuma

jembe afrika

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,604
3,753
Hili basi limenikumbusha siku naenda kumuona mama yangu mkubwa nikiwa na mfuko wa Marlboro nimewekea nguo zangu!na ndani ya mfuko niliwekewa na bibi karanga na mihogo ya kula njiani!

Kilometa 40 tunatumia masaa 4 Hadi matano.halafu konda ndo mjanja kila abiria anajipendekeza kwake ili tu akupunguzie gharama ya mahindi yaliyoko kwenye carrier.

Halafu chini nimevaa ndala za skyway! shati lenyewe limenivaa oversize eti nikue nalo, kaptula yenyewe ya material ya nylon haiishi mpaka miaka mitano daah! ImageUploadedByJamiiForums1447041412.489591.jpg
 
Unatamani siku zingerudi nyuma ili usafiri tena kilomita 40 kwa saa 4 na uweke nguo zako kwenye mfuko wa Marlboro?! Mbona hueleweki Mkuu?!
 
Nakumbuka nilipanda basi kama hilo mwaka 90 naelekea singida kijijini ilikuwa saa 7 mchana.Yaani ilikuwa imejaza abiria mpaka wengine wamekaa juu ya "keria".Na muda huo mchana ulikuwa unapigwa wimbo flani hivi wa Afro 70 unaitwa Afro.Siwezi sahau hilo tukio kila huo wimbo ukipigwa.Hilo basi lilikuwa linaitwa kinanda.
 
Ha ha ha haaaa..... Afrooooooo....
 
Nakumbuka nilipanda basi kama hilo mwaka 90 naelekea singida kijijini ilikuwa saa 7 mchana.Yaani ilikuwa imejaza abiria mpaka wengine wamekaa juu ya "keria".Na muda huo mchana ulikuwa unapigwa wimbo flani hivi wa Afro 70 unaitwa Afro.Siwezi sahau hilo tukio kila huo wimbo ukipigwa.Hilo basi lilikuwa linaitwa kinanda.

Kinanda Ni Yale mabasi yanatokea singida kwenda itigi na sanjaranda kupitia manyoni?
 
Hahahahaaaaa umenikumbusha mabasi hayo tuliyatumia kusafirishia wanajeshi wetu wakati tunamchapa nduli IDD amini dada hahahahaaaaa
 
Hii inanikumbusha enzi hizo tupo Ilboru na hii kitu ilikuwa nicknamed 'the school Katara'.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom