Natamani sana Mtanange kati ya Mnyika na Zitto jimbo la Ubungo

Mnyika asahau kura yangu ubungo...simpi hata akishindana na nan..ame prove fail
 
Mwambieni asijaribu!!!

Wana Ubungo tuna hasira kweli na wasaliti kama Zitto!!
 
Zitto kazima ashinde kwasababu jimbo la ubungo wachaga wengi wako ubungo, kimara na mbezi maeneo mengine yote yaliyobaki hakuna wachaga (magomeni, manzese, sinza, mabibo, chuo kikuu etc kote huko zitto atafunika)

umeludi kwenye ukabila tena yale yale ya south africa ila huku kwa mtindo tofauti
 
Kura za JF ziko ngapi? Ni member wangapi humu wanaenda kwenye mikutano?
 
Zitto mkongwe kwenye siasa na anajua kujieleza,mbaya zaidi anaijua vema sana hii serikali kwasababu amekuwa kwenye kamati za wizara nyingi na alishiriki kikamilifu kukusanya data katika kamati hizo,mnyika uwezo wake mdogo wa kuchambua na kuelezea mambo.

Siongelei ushabiki ila kama we ni mfatiliaji wa mambo ya siasa na bunge kwa ujumla utaelewa point yangu
 
Nakubaliana na hoja yako, Zitto yupo juu ya Mnyika, ana uweza zaidi wa kushawishi. Tuombe tu hili lisitokee.
hata pale UDSM kuna team kubwa ya ACT ya akina Prof Kitila Mkumbo nk wenye influence kwa Dar hivyo akigombea majimbo kama Kawe, Ubungo, Segerea nk ni uhakika atapita kirahisi tu
 
Zitto kazima ashinde kwasababu jimbo la ubungo wachaga wengi wako ubungo, kimara na mbezi maeneo mengine yote yaliyobaki hakuna wachaga (magomeni, manzese, sinza, mabibo, chuo kikuu etc kote huko zitto atafunika)

Mbona Mnyika ni Msukuma ilikuaje wachaga walimpigia kura?
 
kitakachomwangusha zitto ni huu uzandiki wake wa kutaka kuvuruga upinzani basi.rangi yake halisi sasa inaonekana
 
mkuu uma memo dawa chungu......Dsm hatuna upuuzi huo wa kuwa vumilia watu kama mnyika shule imemshinda anakuja kufanya udalali kwenye maisha ya wana ubungo. ..mwambieni aage kabisa maana sisi ndo wapiga kura wake hatumtakiiiiiii.

Mkuu naomba unisamehe ila kiukweli kabisa ndani ya moyo wangu wewe ni juha tena zumbukuku namba moja,, post zako za mwanzo umesema mnyika atashinda kwasababu katika hilo jimbo kuna wachaga wengi na sasa unasema hatarudi bungeni, hivi unajua unachoandika kweli??

Na ukiongelea kuhusu swala la elimu kupitia comment zako tu inaonesha hata wewe mwenyewe shule ulikimbia maana post zako zimejaa utumbo mtupu, kwakifupi kiongozi naweza sema hujui unachochangia nakama unajua waliokutuma hawajui wanachokifanya
 
Wanajamvi,

Kiongozi wa ACT-Wazalendo amewahi kusema kuna baadhi ya maeneo amekuwa akiombwa aende kugombea.Mimi ningependa kumshauri agombee Ubungo au kama vipi Arusha Mjini.
au akagombee kwa wakwe zako
 
Hata Ikulu nzima ikihamia hawataweza kumtoa Mnyika pale Ubungo ... Watanzania wa leo si wa kuwadanganya eti ACT na CCM wako tofauti... nani asiejua kuwa ACT ni project ya CCM ? ...
Wanajamvi,

Kiongozi wa ACT-Wazalendo amewahi kusema kuna baadhi ya maeneo amekuwa akiombwa aende kugombea.Mimi ningependa kumshauri agombee Ubungo au kama vipi Arusha Mjini.
 
Back
Top Bottom