Natamani nisikie POLISI wamewakamata CCM kwa hujuma za kiuchaguzi, natamani sana!

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,956
3,832
Yaani nisikie tu kuwa Polisi wamewakamata vijana au wanachama wa CCM wakihusika na hili na lile katika heka heka za uchaguzi,Polisi mnaweza kujificha hata kuwakama wale wanaoshusha bendera za vyama pinzani,angalau mkaonekana na kujikosha.

Kuna masanduku yalio na kura zilizopigwa yanahangaika Zanzibar hili nalo halihitaji tochi,kama mnavyojisifu mna makachero waliobobea kwa nini hamwavuti pembeni waliosema habari hizi kwenye mikutano wakawapa information na kuyakamata masanduku hayo?

Watu wanshusha bendera,wanabandua picha mbali ya wale mbuzi wale mbuzi walitumwa na Mungu kwani mgombea yule ni padri, Mungu amemuonyesha kuwa asigombee sasa ni yeye na ufahamu wake, Gwajima anajitoa ufahamu ila meseji kutoka kwa Mungu ameipata.

Nazungumzia CCM wanaochana na kubandua bendera na picha basi hata hawa mnashindwa kuwakurupusha angalau mkaficha mengine.
Natamani sana mkayasake masanduku ya kura zilizopigwa Zanzibar jamaa wanahangaika nayo kama waliorogwa, sijui kama hawakumtumia yule mganga wa Uganda. Nina wasiwasi mwisho watagandishwa nayo kwenye mabega.
 
Wanaccm wanapewa semina kabla ya kempeni kuanza
Sio kule Chadema mnalokota watu tu
 
Back
Top Bottom