Kuna wakati nilishawahi kuuliza kama "kuwa rais ni kazi ngumu au rahisi?" Kwa bahati mbaya alinijibu mtu mmoja tu. Nafikiri kuifikisha nchi huko unakofikiria siyo sawa na mbili kutoa moja. Ni complicated process. Itakulazimu utumie nguvu sana ambazo zinaweza kuwa risk kwako pia. Watanzania walio wengi ni maneno mengi zaidi kuliko utekelezaji. Usitarajie watafanya kama unavyoagiza, na ukitaka kudeal na individual person unaweza kujikuta unapoteza hicho kiti cha Urais. Si ajabu ukajikuta unafanya kazi ya kuwakandamiza watu wa hali ya chini huku ukiwainua watu wa karibu yako ili wakulinde, kama alivyofanya Mkapa au anavyofanya Kagame. Namna pekee ya kuibadilisha Tanzania ni kuwa na idadi kubwa ya wabunge wasiokubali rushwa wala wasiokubali kudanganywa kwa vitu vidogo vidogo.