VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,800
Ingawa si rahisi sana, kiukweli natamani kuwa kama Godbless Lema. Ingawa yeye amezaliwa Arusha na mimi Pwani, haijalishi. Pamoja na kuvuliwa Ubunge wa Arusha Mjini haonyeshi kutetereka.
Anaendelea na mkakati wake wa ukombozi wa Taifa hili.Anaendelea kupigania utu na heshima ya watu wote.Mwenzangu Lema ana mizizi ya kibiblia na mimi yakisheria.
Alikuwa mmoja wa Waanzilishi wa Taasisi ya Kijamii iliyojulikana kama 'Msaada wa Haraka toka kwenye Biblia' pale Arusha.
Godbless Lema husema kile anachokiamini na kukisimamia. Mwenzangu Lema ni mtii kwa viongozi wake wakuu wa chama chake.Si mropokaji nje ya vikao. Amejaliwa sauti 'ya ushindi'. Nilibahatika kuisikia kipindi chote cha kampeni ya Ubunge 2010 pale Arusha nilipokuwapo. Amethubutu kumwambia ukweli hata Rais wa nchi.
Nina shaka na uwezo wangu. Nitaweza kweli? Lakini najipa moyo...